ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 18, 2014

TABORA, KAGERA, ARUSHA, KILIMANJARO NA ILALAZAPATA MABINGWA SAFARI POOL.

Diwani wa Kata ya Vingunguti, Asaa Simba(kulia) akimkabidhi nahodha wa klabu ya Mashujaa, Said Miraji(Babu Jee) pesa taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya uibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofanyika Ilala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Katikati ni Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
Wachezaji wa timu ya klabu ya Mashujaa wakishangilia na kitita cha pesa taslimu Shilingi 800,000/= /= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofanyika Ilala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kulia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Asaa Simba na Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
Tabora, Kagera, Arusha, Kilimanjaro na Ilala zapata Mabingwa Safari Pool.
Na MwandishiWetu.
FAINALI za mashindano ya Safari Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”, mikoa ya Tabora , Kagera, Arusha, Kilimanjaro na Mkoa wa kimichezo wa Ilala zimefanikiwa kupata mabingwa wa mikoa zilizomalizika mwishoni mwa wiki katika mikoa hiyo.

Mkoa waTabora mabingwani Tiptop Pool Klabu, Kagera ni Bilele Pool Klabu, Arusha ni Ngarenaro Pool Klabu,Kilimanjaro ni Mboya Pool Klabu na Mkoa wa Kimichezo wa Ilala ni Mashujaa Pool Klabu ambavyo kwa kutwaa ubingwa huo walizawadiwa pesa taslimu kila klabu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume, Taborani Omary Hassan, Kagerani Roberth Butasigwa, Arushani Richard Daudi, Kilimanjaro ni Baraka Jackson naIlalaniYasin Athuman ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila mmoja katika mikoa yao pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanawaake, Taborani Happiness Morgan, Kagerani Sajida Saidi, Arushani Merry Gumbo, Kilimanjaro ni Reticia Kileo, na Ilala ni Recho Kihupi ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/=.

Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo niTabora, Shinyanga, Dodoma Mbeya, Iringa, Morogoro,Mwanza, Kagera, Manyara, Arusha, Tanga, Pwani, Ilala, Lindi, Temeke, Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.