ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 21, 2014

TABAKA LA WASIONACHO NA WALIONACHO HUKOSESHA ELIMU BORA.

Afisa habari wa TASAJA akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokutana nao jana jijini Mwanza kuzungumzia kuwapeleka wanafunzi zaidi ya 20 kutoka vyuo vikuu vya China vijijini katika Wilaya za Misungwi, Magu na Ukerewe na maeneo matatu ya mipakani ya Tarime, Mtukura na Namanga ili kujifunza.
Afisa habari wa TASAJA, Bituro Kazeri, (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kulia na kushoto wapo baadhi ya wanafunzi kutoka China na mtumishi wa ofisi ya TASAJA wakimsikiliza jana.
Afisa habari wa TASAJA, Bituro Kazeri, (wa tatu kutoka kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kulia na kushoto ni  wanafunzi kutoka China na watumishi wa ofisi ya TASAJA wakimsikiliza. Peter Fabian.
NA PETER FABIAN, MWANZA.

TAASISI ya Sayansi ya Jamii (TASAJA) inayoundwa na wahitimu wa Chuo Kikuu cha St. Agustine (SAUT) jijini Mwanza wa Sosiolojia imebaini kuendelea kuwepo tabaka kubwa la wasiokuwa nacho na walionacho nchini.

Akinzungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Afisa Habari wa TASAJA, Bituro Kazeri alisema hali hiyo imesababisha ya maeneo kuwepo tabaka kubwa la baadhi ya wanafunzi kushindwa kupata elimu bora kutokana na kukithiri kwa umasikini wa kipato katika familia zao.

“Kuna tabaka kubwa linazidi kuongezeka la walionacho (matajiri) na wasiokuwa nacho (masikini) katika familia hali hii ikiachwa iendelee ni hatari ya ustawi wa taifa kutokana na baadhi ya matajiri wengi kuupata kutokana na kushamiri kwa rushwa,”alisema.

Kazeri alisema hali hii pia imesababisha jamii iliyo masikini kuibua chuki kwa familia zilizo na kipato kizuri na matajiri kwa kutoheshimiana baina ya matabaka hayo jambo ambalo si vyema likaachwa na badala yake serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilitafutie ufumbuzi wa haraka.

“Kilimo ndiyo uti wa mgongo ambapo asilimia kubwa wapo vijijini ambayo ni nguvu kazi, lakini huko vijijini kwa sasa hali ni tofauti na zamani kutokana na vijana wengi kukimbilia mjini kutpata mabadiliko ya haraka na kuacha kilimo kuwa cha wanawake ambapo utafiti unaonyesha asilimia 75 wanaotekeleza kilimo vijijini ni wanawake,”alisema.

Aliongeza kuwa, tunaiomba serikali sasa ikaangalia uwezekano wa kupanua zaidi kilimo, kusaidia sekta hii kwa njia ya umwagiliaji badala ya kutegemea zaidi mvua hili litasaidia kurejesha hata vijana kushiriki kilimo na kuacha kukimbilia mjini kutokana na kupata harasa baada ya ukosefu wa mvua za kutosha kuathiri mazao yao ya biashara na chakula.

“Taasisi za kilimo zitoe huduma ya afya udongo ili kuhuisha ardhi iliyochuja na kuwapa mwanga wakulima kujikita kutumia mbolea zinazofaa kulingana na ushauri wa kitaalamu, maafisa ugani wawe karibu na wawasaidie wakulima ,”alisisitiza.

Alisema kwamba raslimali tulizopewa na mwenyezi mungu hazitoshi kama hatutaweka ukomo katika utashi , tama, matamanio na matarajio yetu ni vyema kukumbushana kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kutumia kwa uangalifu rasilimali zetu sote kwa lengo la kutunufaisha watu wengi huku tukitoa kipaumbele kwa kizazi kijacho.

Aidha alisema, vijana wemekuwa wakihitaji njia rahisi naza mkato katika kufauru maisha hali ambayo imepelekea vijana wengi kuacha kujishughulisha na kilimo kwa kuwa kilimo kinahitaji uvumilivu wa muda mrefu na mjini wanakimbilia kufanya biashara na baadhi kujitumbukiza kufanyabiashara zisizo lasimi na zilizo kinyume na maadili na vitendo vya uharifu.

Kazeri alisema kuwepo kwa matabaka hayo ndo kumesababisha sasa kuibuka hoja za wazee na vijana, wanawake na wanaume katika siasa nchini na ikiendekezwa basi taifa hili litaingia kwenye dhambi kubwa ya kuanza kubaguana na hata kupelekea kumomonyoka zaidi kwa maadili na hata kupelekea kuanza chokochoko za kila aina. 

Afisa huyo pia alieleza kuwa TASAJA kupitia mradi wa ISEK umefanikiwa kuwapeleka wanafunzi zaidi ya 20 wa vyuo vikuu kutoka China kujifunza mira na utamaduni za makabira ya mikoa ya Kanda ya Ziwa katika Wilaya za Misungwi, Magu na Ukerewe ili kuishi na familia hizo za kawaida vijijini kujifunza na kuona utofauti ili kuwasaidia katika utambuzi.

Kazeri alisema TASAJa inatoa wito kutambua binadamu wote ni sawa, tunategemeana hakuna aliyebora kuliko mwingine, utu ndo msingi wa kuheshimiana, kushirikiana na kusaidiana hali hii itaondo tabaka moja kufikia fursa za maisha, hatua ya kupanda mbegu za kuharibu jamii yetu na kudumisha mbegu za chuki na kusababisha kuwa chanzo cha mafarakano na umoja na amani ya taifa letu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.