ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 19, 2014

AJALI MBAYA YATOKEA MKOANI TABORA BAADA YA MABASI YA SABENA NA A.M. DREAMLINE KUGONGANA USO KWA USO.

 Watu zaidi ya watano wanasadikika kufariki dunia hii leo majira ya alasili leo katika ajali iliyotokea eneo la Mkolye, takribani km 4 toka Mjini Sikonge baada ya basi la Sabena lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza na basi la A.M. toka Tabora kwenda Katavi kugongana uso kwa uso. 
 Kwa mujibu wa wapenyeza habari ambao walikuwako kwenye tukio wanasema kuwa madereva wote wa mabasi hayo wamefariki hapo hapo, mmoja wao akiwa katika hali mbaya ya kukatika kichwa.
Hali si shwari, mabasi nyang'anyang'a.
Msaada ukiendelea kufanyika kuwanasua abiria walio ndani ya mabasi hayo.  
Aidha inatajwa kuwa abiria kadhaa wakiwa wamenasa katika mabasi hayo, baadhi wamekutwa wakiwa wamekatika mikono na miguu. Abiria wapatao watano wamefariki hapo, na majeruhi zaidi ya 30 wamepelekwa katika Hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge mkoani Tabora. Taarifa hii itaendelea kuboreshwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.