ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 22, 2014

WAZIRI ASEMA SHERIA HAIRUHUSU UVUVI WA SAMAKI WACHANGA, NYAVU HARAMU NA BIASHARA.

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani amewaonya wananchi wanaovua na kufanya biashara ya samaki wadogo wasiotakiwa kuvuliwa , kuacha na hakutakuwa na huruma kwa watakaokamatwa kwa uhalifu huo.
Alisema kwamba wanaotengeneza, kuingiza na kuuza zana haramu za uvuvi, nao watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa serikali kupitia Wizara yake itaendelea kulinda rasilimali zilizopo kwenye Bahari, Maziwa, Mito na Mabwawa ambayo baadhi ya wananchi wanatumia zana hizo haramu kufanya vitendo vya uhalifu huo.
Dkt. Kamani alieleza kwamba Sekta ya Uvuvi nchini hawezi kuwaletea manufaa watanzania wa leo na kizazi kijacho, iwapo uvuvi haramu utaachwa uendelea hivyo serikali haitawavumilia, itaendelea kuwakamata na kuwafikisha kwenye mkondo wa sheria kwa kukiuka sheria ya Uvuvi endelevu ya mwaka 2002.
“Hata mfugaji huwezi kuendelea iwapo unachinja ndama, nawaomba wananchi muwe walinzi wa rasilimali za majini na zilizopo kwenye maliasili zetu, wafichueni wote wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu, uuzaji wa samaki wadogo na ujangiri.” Alisema Kamani wakati akihutubia wananchi wa kijiji cha Jisesa na Busami wilayani Busega mkaoni Simiyu juzi.
Mbunge huyo alieleza kwamba, sheria hiyo ya uvuvi pia hairuhusu mfanyabiashara yoyote kuingiza au kuuza nyavu zenye matundu yasiyotakiwa hivyo wauzaji wa nyavu, samaki na wavuvi haramu wote wanapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walisikika katika mikutano hiyo, wakilalamikia maafisa Uvuvi wa wilaya ya Busega wamekuwa wakiwakamata baadhi ya wafanyabiashara wa samaki wanaokutwa wakiwa na samaki wadogo na hivyo kumuomba Waziri huyo wasikamatwe kwa kuwa wao hawavui ama kutengeneza nyavu zilizo pigwa marifuku.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.