ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 27, 2014

MALAIKA BAND WAWASILI MWANZA TAYARI KUVUNJA JUNGU LEO DHIDI YA KIDUMU.

Mwanamuziki ambaye pia ni repa hatari wa kundi la Malaika band Totoo Ze bingwa akiwasili katika uwanja wa Airport Mwanza kwaajili ya kujumuika na wenzake kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza hii leo katika Usiku wa Vunja Jungu Villa Park ambapo kundi hilo litapambanishwa na Bodaboda Band ya mwanamuziki Kidumu.
 Msikilize Cristian Bella.


Akisalimiana na Meneja wa Villa Park Mwanza ambaye ni mwenyeji wao pichani kulia ni Mwanamuziki mpiga kinanda wa kundi la Malaika band Andrew Sekedia akiwasili katika uwanja wa Airport Mwanza kwaajili ya kujumuika na wenzake kutoa burudani kwa wakazi wa Mwanza hii leo katika Usiku wa Vunja Jungu Villa Park.
Andrew Sekedia (L) akiwa na mtangazaji wa Star Tv Abdalah Tilata katika uwanja wa Airport Mwanza alipowasili leo asubuhi akiwa yeye na wanamuziki wengine wote wa Malaika Band.
Hawa hapa Malaika Band wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Villa Park Mr. Ramma.
Totoo Ze Bingwa (L) akiwa na mpiga bass wa Malaika Band uwanja wa ndege wa Mwanza walipowasili leo asubuhi.
The angle.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.