ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 6, 2014

ASILIMIA 25 TU YA KAYA NCHINI HUTUMIA VYOO BORA VYA KISASA

Waziri wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid.
WAZIRI  wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid (MB) amesema kwamba Wizara yake ilifanya utafiti katika Halmashauri 112 nchini mwaka 2013 ambapo matokeo yanaonyesha asilimia 25 tu ya Kaya kutumia vyoo bora.

Dkt. Rashidi alisema hayo jana wakati wa kilele cha Siku ya Maadhimisho ya Mazingira Duniani yaliyofanyika jijini Mwanza kitaifa, ambapo utafiti huo matokeo yake yanaonyesha kuwa ni asilimia 29.6  hazina vyoo kabisa huku asilimia 9 kuna vifaa maalum kwa ajili ya kunawa mikono jambo ambalo ni hatari kubwa kwa afya kutokana na wananchi wengi kuwa na mwitikio mdogo wa kujenga vyoo vya bora vya kisasa.
Hakuna matengenezo pale uharibifu unapotokea.
“Takwimu hizo ni kielelezo cha kuwepo kwa magonjwa ya kuhara  na vile vile zinaonysha kuwa bado tupo nyuma ikilinganishwa na lengo la kitaifa tulilojiwekea la kufikia asilimia 53 ya kaya zenye vyoo bora ifikapo mwaka 2016,”alisema .

Rashidi alisema pia Wizara hiyo  ilizindua Kampeni ya kitaifa ya usafi na mazingia ya miaka minne  iliyozinduliwa na mwaka 2012 iliyolenga kuwezesha kaya milioni 1,520,000 kupata huduma bora za vyoo nchini ifikapo mwaka 2015 ambpo hadi sasa kampeni hiyo imefanikisha kaya 312,528  kujenga vyoo bora sawa na asilima 56.4 ya lengo hilo.
Hakuna milango kwaajili ya kujisitiri, hakuna dawa wala usafi siyo suala la kuzingatiwa ni hali ya vyoo kwa baadhi ya shule zetu nchini.
Choo si sehemu inayopewa kipaumbele na huchukuliwa kama sehemu chafu hivyo huwekwa mbali na makazi.
Aidha kaya 204, 213 zina vifaa maalumu vya kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kwamba  vitongoji  9,120 vimesaini makubaliano ya kuboresha hali ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ikiwa ni utekelezaji wake.

Waziri Dkt. Rashid alitangaza washindi wa tuzo za mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2014, kundi la kwanza lilihusisha Halmashauri za Majiji manne ya Tanga, Mbeya, Mwanza na Dar esalam ambapo Jiji la Mwanza limeibuka kuwa mshindi kwa asilimia 75 ikiwa ni mara ya tisa mfurulizo, Halmashauri za Mikoa mshindi ni Manispaa ya Kinondoni ilibuka kwa asilimia 55.7 kwa mshindi mmoja.

Kundi jingine la tatu lilishirikisha Halmashauri za Manispaa 15 ambapo mshindi wa kwanza ni Manispaa ya Iringa kwa asilimia71.3, mshindi wa pili Manispaa ya Moshi kwa asilimia 68.1 na mshindi wa tatu ikichukuliwa na Manispaa ya Morogoro kwa asilimia 67, kundi la nne ni Halmashauri za Miji ambapo washindi asilimia zao kweny mabano kuwa ni Mji wa Njombe (67.1), Kahama (63.2)  na Mpanda (60.2).

Wito wangu ni kuikumbusha jamii juu ya ungonjwa hatari wa Dengue ambao umetokea mlipuko wa wagonjwa 1,119 kupatwa na kutokea vifo vya watu wanne, kufatia kuumwa na mbu aina ya “Aedes” ambaye hupata mazalia katika maeneo ambayo si safi akitolea mfano vifuu vya nazi , makopo, vyungu vilivyotupwa hovyo, matairi ya magari na maji ya bafuni hivyo kuwataka kuchukua hatua ya kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.