ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 28, 2014

WANAJESHI 11 WAUAWA NA BOKO:H NIGERIA

Taarifa kutoka mjini Buni Yadi katika jimbo la Yobe Kaskazini mwa Nigeria, zinasema kuwa watu 24 wakiwemo wanajeshi 11 wameuawa katika shambulizi dhidi ya kambi za wanajeshi.
Inaarifiwa kuwa kundi la Boko Haram ndilo linashukiwa kufanya mashambulizi hayo.

Waliwaambia wanakijiji kutokuwa na hofu kwani nia yao haikuwa kuwadhuru raia bali maafisa wa usalama.Wakaazi wanasema washambuliaji waliwasili katika eneo hilo kwa magari kumi ya kawaida na gari moja la kijeshi.
Wanajeshi 11, polisi 13 akiwemo mwanamke mmoja waliuawa.
Pia waliteketeza majengo na magari ikiwemo makazi ya kiongozi mmoja wa kijadi na kituo kimoja cha polisi.
Taarifa zaidi bado zinajitokeza pole pole hasa kwa kuwa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana na miundo mbinu mibovu.
Jimbo la Yobe ni moja ya majimbo matatu ambayo serikali imeweka sheria ya kutotoka nje usiku. Licha ya sheria hiyo mashambulizi ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhudiwa mengi yakifanywa na Boko Haram. CHANZO:BBC SWAHILI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.