ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 24, 2014

USIKU WA LEO JEMBE BEACH NI KAMA LISBON VILE

Kama uko jijini Mwanza hii leo (jumamosi 24/05/2014) basi ile Fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Uropa kati ya Real Madrid na Atletico Madrid tutakwenda kuitizama pale JEMBE BEACH.
Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo na mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa zaidi duniani Gareth Bale watakuwepo katika timu ya Real Madrid itakayochuana na Atletico Madrid katika fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Uropa hii leo jumamosi.
Ronaldo, 29, alikuwa amekosa kucheza mechi mbili akiuguza jereha sawa na mshambulizi Gareth Bale, 24, ambaye hakushiriki katika mazoezi siku ya jumanne.
Wawili hao kwa ushirikiano wamiefungia Real Madrid mabao 68 msimu huu.
Kocha Carlo Ancelotti, ambaye anapania kuwa mkufunzi wa pili katika historia ya mchuano huu kuwahi kushinda taji la ubingwa barani Ulaya mara tatu amethibitisha kuwa nyota hao wawili wakali kwa mashambuli watakuwepo
Real Madrid inapania kutawazwa mabingwa wa Uropa iwapo watawalaza washindi wapya wa ligi kuu ya Uhispania Atletico Madrid mbali na kusitisha ukame wa miaka 12 wa kombe hilo lenye umaarufu barani Uropa.
Atletico wamechuana dhidi ya Real Madrid mara nne msimu huu ,Real ikishinda mechi za kuwania kombe la Spanish kwa mabao 5-0 huku Atletico ikiibuka na ushindi katika mechi za ligi ya Uhispania .
Wakati huo huo nyota wa Atletico Madrid Diego Costa amerejea mazoezini leo kujifua tayari kwa fainali ya kombe la mabingwa bara Uropa dhidi ya Real Madrid baada ya kudaiwa kuwa alizuru Belgrade kupata utabibu kutoka kwa Muuguzi mmoja anayetumia kondo la nyuma kwa utabibu wake.
Costa aliumia mapema katika mechi ya kuamua mshindi wa ligi kuu ya Uhispania la liga ambayo Atleticoilitoka sare ya 1-1 na Barcelona na kutawazwa mabingwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.