ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 31, 2014

GEORGE TYSON HATUNAYE TENA.

Msiba mwingine umeikumba tasnia ya Filamu nchini (BONGO MOVIE) baada ya Director aliyeleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia hiyo George Tyson, kufariki dunia kwenye ajali iliyotokea jana usiku ikitokea mjini Dodoma alikokwenda kwaajili ya kazi ya kutengeneza kipindi cha 'The Mboni Show'.


George Tyson amefikwa na mauti katika ajali mbaya baada ya gari aina ya Noah walilokuwa wakisafiria kupinduka mara kadhaa kutokana na kupasuka tairi.


Ajali hilo ilitokea majira ya saa moja eneo la gairo mkoani Morogoro.  Watu wengine wanne waliokuwa kwenye gari hilo walikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro kwa matibabu kutokana na kuumia sehemu mbalimbali mwilini.

Tutaendelea kuwapa taarifa kadri zinavyotufikia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.