ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 29, 2014

BIA YA SAFARI LAGER YASHINDA TUZO LA UBORA KIMATAIFA 2014.

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha moja ya tuzo za dhahabu ilizowahi kupata wakati wa mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa Dar es Salaam.
 BIA YA SAFARI LAGER YASHINDA TUZO LA UBORA KIMATAIFA 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam, Alhamisi 29Mei 2014;Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza ushindi wake wa tuzo la Ubora wa Kimataifa 2014 maarufu kama ‘International High Quality Trophy 2014’ katika mashindano ya Monde Selection. Safari Lager itapokea tuzo hiyo Jumatatu tarehe 2 Juni, mjini Bordeaux, Ufaransa.

Tuzo ya Ubora wa Kimataifa au ‘International High Quality Trophy’ ni tuzo ya heshima linalotolewa kwa bidhaa ambazo zinashinda tuzo za ‘Gold’ au ‘Grand Gold’ kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo. Safari Lager inepewa tuzo hiyo ya heshima kwa kuweza kushinda ‘Gold’ na ‘Grand Gold’kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo.

Akizungumuza na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Bw. Oscar Shelukindo,  alisema, “Safari Lager ni bia ambayo siku zote nia yake ni kuridhisha wateja wake na kwa miaka yake yote…Tunaishukuru sana Monde Selection kwa heshima waliyotupa nahii inatupa motisha ya kuendelea kuwapa wateja wetu bia bora zaidi”.

Bw. Fimbo Butullah, Maneja Masoko wa Safari Lager aliongezea kwa kusema, “Tungependa tena kuishukuru Monde Selection kwa heshima waliyotupa, wateja wetu na kwa Watanzania kwa ujumla. Sisi Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager  kwa kufika hapa tulipo sifa hizi si za TBL peke yake ni za Watanzania kwa ujumla na haswa wateja wtu wanaotumia bia ya Safari Lager”.

Fimbo alimaliza kwa  kutoa wito kwa wateja wa Safari Lager kuendelea kutumia bia hiyo kwani ndio bia namba moja kwa ubora na kwa mauzo Tanzania na pia ni bia namba moja Afrika na leo hii tunapozungumza imepata heshima ya pekee ya ubora wa kimataifa.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.