ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 16, 2014

IRINGA YAPATA MABINGWA WA SAFARI HIGHER LEANING IRINGA MBEYA

Meneja mauzo wa Tbl Iringa, Philip Kubecha(kushoto) akimkabidhi kikombe nahodha wa timu ya chuo cha RUCCO, Said Mohamed mara baada ya kutwaa ubingwa wa mkoa wa mashindano ya Safari Pool Higher Learning Competition 2014 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.Katikati ni Meneja mauzo msaidizi Tbl Iringa, Christopher Kifunda.
Meneja mauzo wa Tbl Iringa, Philip Kubecha(kushoto) akimkabidhi pesa taslimu shilingi 500,000/= nahodha wa timu ya chuo cha RUCCO, Said Mohamed mara baada ya kutwaa ubingwa wa mkoa wa mashindano ya Safari Pool Higher Learning Competition 2014 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.
Shangwe.
Meneja matukio wa TBL Mbeya, Abubakari Masori(kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Mzumbe, Steven Mussa fedha taslimu shilingi 500,000/= mara baada ya kutwaa ubingwa wa mkoa wa mashindano ya Safari Pool Higher Learning Competition 2014 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo.Wengine ni baadhi ya wachezaji na mashabiki wa timu hiyo.
Mabingwa Safari Pool Higher Learning wapatikana Iringa Mbeya.
Na Mwandishi Wetu.
MIKOA ya Iringa na Mbeya imefanikiwa kupata mabingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool unaoshirikisha Vyuo vya Elimu ya juu yajulikanayo kama “Safari Pool Higher Learning Competition 2014” mwishoni mwa wiki katika viwanja tofauti na hivyo kupata waakilishi wa kila mkoa watakokwenda kushindana kitaifa mkoani Kilimanjaro May 4,2014.

Mkoa wa Iringa, Chuo kilichofanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa ni chuo cha RUCCO ambacho kwa ubingwa huo kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 500,000/= na nafasi ya kupeperusha bendera ya Mkoa wa Iringa kwenye mashindano ya kitaifa mkoani Kilimanjaro. 

Nafasi ya pili ilichukuliwa na chuo cha Tumaini ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/=, nafasi ya tatu ilichukuliwa na Chuo cha Mkwawa ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na chuo cha CDTI ambacho kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/=.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Mbaraka Godfrey kutoka chuo cha Mkwawa alitwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= pamoja na tiketi ya kuwalikisha mkoa wa Iringa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwenye fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro. Upande wa wakinadada, Betrice Madafu alifanikiwa kutwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha wakinadada mkoa kwenye fainali za kitaifa.

MkoaniMbeyachuokilichofanikiwakutwaaubingwawaMkoani Chuo cha Mzumbe ambacho pia kilizawadiwa fedhata slimu shilingi 500,000/= pamoja na nafasi ya kuwa kilishajiji la Mbeya katikaf ainali za kitaifa mkoani Kilimanjaro. 

Nafasi ya pili ilichukuliwa na chuo cha MUST ambacho kilizawadiwa Shilingi 300,000/=, nafasi ya tatu ilichukuliwa na chuo cha TIA ambacho kilizawadiwa Shilingi 200,000/=  na nafasiya nne ilichukuliwa na chuo cha Tumaini ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 100,000/=.

Upande wamchezaji mmoja mmoja wanaume, Steven Kyasi kutokachuo cha Mzumbea litwaa ubingwa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 150,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Mkoawa Mbeya upande wawachezaji mmoja mmoja kwenye fainali za kitaifa Mkoani Kilimanjaro na upande wa wakinadada, Amina Mhina kutoka chuo cha Mzumbe pia alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na hivyo kuzawadiwa fedhata slimushilingi 100,000/= pamojanakuwakilishajiji la Mbeya upande wamchezaji mmoja mmoja katika fainali za kitaifa May 4,2014. Mkoani Kilimanjaro.

Fainali za Kitaifa zitashilikisha mikoa na neambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na wenyeji wa mashindano wa mwaka huu wa 2014,Mkoawa Kilimanjaro.
Mabingwa watetezi wamashindano hayo ya Pool vyuo yanayo dhaminiwa na TBL kupitia Bia yake ya Safari Lager ni Dar es Salaam, ambacho ni chuo cha CBE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.