ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 23, 2014

HUZUNI KUBWA YATAWALA FAMILIA YA METRO FM 96.4 MWANZA.

Simanzi kubwa imewakumba watangazaji, wanahabari na wasikilizaji wa kituo cha radio Metro Fm ya jijini Mwanza mara baada ya kuondokewa na mmoja kati ya mfanyakazi mwenzao  aliyetambulika kwa jina la DJ Alex.
 Dj Alex alifariki dunia juzi akiwa ni mmoja kati ya abiria wa basi la 
kampuni ya Luhuye lililokuwa likitokea Sirari Mkoani Mara Kwenda Kahama kupata ajali katika eneo la Masanza Kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu. 
Meneja wa Metro Fm Alex Ngusa (kulia) ameongoza kikao cha watumishi wa kittuo hicho kutoa taarifa na utaratibu wa jinsi ya kujipanga na kwaajili ya kushiriki taratibu zote hata kumpumzisha katika nyumba ya milele mtumishi mwenzao.
Safu ya baadhi ya wafanyakazi wa Metro Fm ndani ya kikao hicho.
Kutoka kulia ni Dj Victor, Tommy Alphonce na Jackob Usungu ambaye alikuwa akishirikiana na marehemu kufanya kipindi kimoja cha muziki wa Afrika kilichokuwa kikiruka majira ya jioni kikitikisa hasa.
Marehemu Dj Alex anatarajiwa kuzikwa leo (jumatano) nyumbani kwao wilayani Bunda mkoani Mara.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.