ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 28, 2014

WATEJA WA AIRTEL KULIPA MIKOPO YA MASOMO KUPITIA HUDUMA YA AIRTEL MONEY.

Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde
Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma itakayowawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kurejesha mikopo yao kupitia huduma ya Airtel Money kulia pichani ni  Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja
Wateja wa Airtel kulipa mikopo ya masomo kupitia huduma ya Airtel Money

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imeanzisha mapinduzi ya malipo ya kielectoniki kwa kuwawezesha watumiaji wa huduma ya Airtel Money kulipia mikopo ya elimu ya juu  kupitia huduma ya Airtel money

Ushirikiano huo kati ya Airtel na HESLB unawawezesha wahitimu wa masomo ya juu katika vyuo mbalimbali nchini kuweza kulipia mikopo yao kwa urahisi kupitia huduma ya Airtel Money na hivyo kuongeza ufanisi katika  ukusanyaji wa mikopo hiyo

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” tumewawezesha kupitia huduma yetu ya Airtel money wateja wetu kuweza kulipia mikopo yao ya elimu ya juu inayotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu kirahisi wakiwa majumbani mwao. Tunawahakikishia wateja wetu huduma bora, salama, ya uhakika yenye viwango vya gharama nafuu  na inayopatikana mahali pote nchini kupitia mawakala zaidi ya elfu 35,000 walionea nchini.

 Huduma hii ni ya haraka na nirahisi kutumia, sasa wateja hawana haja ya kusubiri kwenye mistari muda mrefu kufanya malipo, wanachotakiwa ni kufanya muamala rahisi kwa kupitia simu zao  kulipa na kupata uthibithisho wa malipo ndani ya sekunde chache

Ili kupata huduma hii mteja anatakiwa kupiga *150*60#  na kuunganishwa na orodha ya Airtel Money kasha kuchagua namba 5 kufanya malipo, alafu chagua namba 8  kupata huduma zinginezo kisha kuandika neno HESLB , ingiza kiasi cha pesa, kumbukumbu namba na namba ya siri kufanya malipo  aliongeza mmbando

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Bwana Juma Chagonja alisema”hii imekuja wakati muafaka ambapo baadhi ya waliofaidika na mikopo hii muda wao wa kurejesha malipo ya mikopo yao umekwisha,  kwa kupitia huduma hii ya kulipia kwa Airtel Money hakutakuwa na haja ya watu kutembea umbali mrefu na kupanga foleni katika mabenki ili kulipia, tunaleta kwa wateja wetu urahisi wa malipo na njia mbadala ya kurejesha mikopo yao kwa wakati na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mikopo hiyo.

Chagonja aliongeza kwa kusema kwa kupitia huduma hii ya Airtel Money sasa wateja wetu wataweza kulipa mikopo yao kirahisi wakati wowote mahali popote masaa  24 siku 7 kwa wiki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.