ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 6, 2014

NGUMI ZA NELSON MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP ZAFUNGULIWA KAWE.

Bondia Fabian Gaudence kushoto akipambana na Hussein Mnimbo  wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela  yabayofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaamGaudence alishinda mpambano huo kwa pointi.
Bondia Rashidi Samvu kutoka Kigoma  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde naHafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindani ya wazi ya Nelson Mandela  yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam
Bondia Part Kimweri kutoka Tanga  kushoto  akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Saidi Jabir wa Ngome Dar wakati wa mashindano ya wazi ya Nelson Mandela  yaofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam, Kimweri alishinda mpambano huo kwa pointi picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya viongozi wakifatilia mashindano hayo
Mgeni wa heshima katikati Diwani wa Kata ya Kawe Othumani Kipete akiwa na viongozi wa Shilikisho la mchezo wa ngumi za Ridhaa nchini kulia ni Rais wa shilikisho hilo Mutta Rwakatare  makamu wa raisLukelo Willilo na Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis.
Marefarii , mabondia na Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Mjumbe wa bft Antony Mwangonda akiwa na makamu wa rais Lukelo Willilo

Na Mwandishi Wetu
MASHINDANO ya mchezo wa Ngumi yanayokwenda kwa jina la Nelsoni Mandela Open ChampionShip  yameanza kutimua vumbi katika Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe  jijini Dar es salaam

Akizungumzia mashindano hayo yalivyo na ubora wa ali ya juu Makamu wa Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo Willilo 'amesema mashindano hayo kwa sasa yameboleshwa kwa kufuata taratibu za chama cha ngumi za ridhaa Dunia kwa sasa mabondia awavai kofia ngumu wanakuwa vichwa wazi hivyo wapenzi wa ngumi weje waone mabadiliko makubwa katika ngumi za ridhaa ndio ambazo ni msingi wa maendeleo ya mchezo wa masumbwi nchini;'

Zamani mabondia walikuwa wanavaa kofia lakini kutokana na mabadiliko sasa awavai kofia wanapigana vichwa wazi  ambapo kwa kuanzia tumeamua kuweka mashindano haya kwenye viwanja vya wazi na ni bule tu akuna kingilio ili kila mtu ajionee mabadiliko ya ngumi mashindano hayo yanayo husisha mikoa mbalimbali nchini

Mashindano haya yatakuwa ya siku tano kuanzia jumatano mpaka jumapili na ngumi zinanza kupigwa saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku ngumi ndio zitakuwa zikisha

Katika ufunguzi huo bondia Patrck Kimweri wa Tanga alishindwa kufurukuta mbele ya Said Jabir wa ngome na Rashidi Samvu wa Kigoma alipigwa kwa pointi na Hafidhi Kassimu wakati Fabian Gaudence  akimsambalatisha Hussein Mnimbo  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.