ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 9, 2014

MADIWANI WA JIJI LA MWANZA WAMGOMEA MKURUGENZI WAO:BAJETI IMEJAA UBABAISHAJI,VIWANDA VYA SAMAKI VINALIPA LAKI 1 KAMA KODI KWA MWAKA ILEHALI VINAINGIZA MABILIONI.





Na PETER FABIAN
G.SENGO BLOG.

MADIWANI wa Jiji la Mwanza leo wamegomea kujadili Rasimu ya Bajeti ya mwaka 2014/2015 iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, kwa madai kuwa haijakidhi na ina ubabaishaji katika mpango mkakati wa makusanyo ya Kodi kupitia Vyanzo vyake vya ndani.

Rasimu hiyo liyowasilishwa na Mchumi Msaidizi Joseph  Kashushula kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji hilo ilionekana kuwakera sana waheshimiwa Madiwani wote bila kujali wanatoka vyama gani vya siasa na kuanza kuchangia hoja ambazo zimepelekea kutolewa azimio la kurudisha Kamati ya Fedha kufanyiwa marekebisha upya na kuja na majibu ya msingi kabla ya kuwasilishwa tena na kuanza kujadiliwa.

Akizungumza wakati wa kuendesha kikao hicho Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula alisema kwamba kutokana na hoja za waheshimiwa Madiwani walizochangia na kuwepo mapungufu huku Mkurugenzi na timu yake ya wataalamu kukosa majibu ya kina kuhusiana na hoja za mpango mkakati za ukusanyaji mapato kuonyesha kukusanya bilioni 9 tu kupitia vyanzo vyake vya ndani.

Meya Mabula alisema kamwe hawako tayari kukaa na kupoteza muda wa kujadili Rasimu hiyo kutokana na mapungufu hayo yaliyojitokeza huku hoja za madiwani zikidai kuwa kupitia vyanzo vya mapato ya Halmashauri hiyo ya Jiji vilivyopo vinaweza kukusanya kiasi cha zaidi ya bilioni 13 huku hoja zingine zilizochangiwa ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuwa kidogo.

“Mkurugenzi na timu yako tunaomba mrudi mkajipange upya kwa rasimu hii hatuko tayari kukaa na kujadili haiwezekani viwanda vilivyopo hapa Jijini vikawa vinalipa Kodi ya laki moja kwa mwaka wakati vinaingiza mabilioni ya fedha kwa mwaka hili halikubaliki na Bajeti hii siyo rafiki kwa mustakabali wa kuwatumikia wananchi wa Jiji hili na inaonyesha tumekuja hapa kufanya mchezo wa kuigiza” alisema

Aliongeza kuwa kufatia wajumbe ambao ni waheshimiwa madiwani kwa umoja wao na kwa masilahi ya wananchi ambao wanawawakilisha kuamua kuweka tofauti zao za kisiasa na kuungana kuikataa rasimu hii kujadiliwa kutokana na kutokidhi ni vyema mkajipanga kuanda na kurekebisha kasoro hizo ili kujadiliwa kuletwa na kuwasilishwa ili kuwapa mwanya wa kujadiliwa.

Meya Mabula aliahilisha kikao hicho kwa kumtaka Mkurugenzi Alfa Hassan Hida kuitisha kikao cha dharula cha Kamati ya Fedha (FINENCE) kesho asubuhi majira ya saa 3:00 na mchana majira ya 6:00 kuwe na kikao cha dharula kuipitia baada ya kufanyiwa marekebisho kwenye ukusanyaji wa mapato,kujiandaa kulipa madeni ya wakandarasi utekelezwaji wa miradi katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu ya Barabara kupitia fedha za Mapato ya ndani. mengineyo.

Kufatia hatua hiyo baadhi ya wananchi wamempongeza Meya Mabula,Wabunge na waheshimiwa Madiwani kwa kuungana pamoja na kuweka tofauti zao za kisiasa (Vyama vyao) ili kuhakikisha Bajeti watakayopitisha inakuwa suluhisho kwa wananchi wa Jiji hili na mwarobaini kwa wanohujumu mapato ya Halmashauri ya Jiji kupitia vyanzo vyake vya ndani.

“Huyu ndiye Meya, wananchi wa Jiji hili tunaona amekuwa ni mtu asiyetaka sifa na amekuwa mtu wa kuchukua maamuzi sahihi na kusikiliza kilio cha wananchi kwani hali ya miundombinu kwa sasa huko kwenye mitaa na kata inatisha, madeni ya malipo ya fidia ya maeneo yaliyochukuliwa na Jiji ni muda sasa na huduma za Jamii zinazorota, tunaomba Kamanda awabane kweli kweli” walisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.