ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 22, 2014

AIRTEL ‘MIMI NI BINGWA’ YAZIDI KUWAPA WATANZANIA WENGI FARAJA

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akisisitiza jambo wakati akiwatangaza washindi wa droo ya wiki ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa jana na kuwapata washindi wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 na kumpata Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa aliyejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mmbando (kulia) akimpigia simu Bw. Edwin Edmund Kajimbo mkazi wa Iringa aliejishindia tiketi mbili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’ kwenye uwanja wa Old Trafford, katika droo ya tisa ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. Wakati wa droo hiyo iliyochezeshwa jana, washindi 14 wa pesa taslimu ya zaidi ya Shilingi milioni 22 walipatikana. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Millao.
Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ yazidi kuwapa watanzania wengi faraja
  • Yatoa zaidi ya shilingi milioni 194 kwa washindi
  • Tiketi 18 za kwenda Old Trafford zatolewa
Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imeendelea kuwapa faraja washindi wake wa promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ kwa kuwazawadia zaidi ya pesa taslim shilingi milioni 194 na kutoa tiketi 18 za safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford nchini Uingereza.

Kampuni hiyo ya mawasiliano jana imetoa shilingi milioni 22 pesa taslim kwa washindi 14 na tiketi mbili za kwenda Old Trafford kuangalia mechi ya ligi kuu ya Uingereza moja kwa moja ‘live’, kwa mshindi mmoja wa kila wiki katika wiki ya tisa ya promosheni ya Mimi ni Bingwa iliyochezeshwa katika ofizi ya makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya droo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema promosheni ya Mimi ni Bingwa imekuwa ikiwapa faraja watanzania wengi ambao wamekuwa wakionyesha furaha zao za ushindi wa pesa taslim au safari inayogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford.

“Tumekuwa tukipokea maoni kutoka kwa washindi wetu, hususani wale waliojishindia pesa taslim, wakisema pesa waliojishindia toka promosheni ya Mimi ni Bingwa wameipata wakati muafaka wakihitaji zaidi msaada wa kifedha.

“Wanasema miezi iliyochaguliwa kwa ajili ya promosheni na pesa walizopokea bila jasho kutoka Mimi ni Bingwa promosheni, zimeweza kuwaongezea uwezo wa kifedha ili kupambana na hali ngumu ya kiuchumi katika miezi hii migumu inayohitaji fedha nyingi. Tumekuwa tukituma milioni moja (1m/-) kwa washindi wetu mara tu baada ya kuwatangaza kupitia Airtel money na kuweka shilingi milioni tano (5m/-) katika akaunti za washindi baada ya kupata taarifa zao za benki,” alisema Mmbando.

Aliongeza kuwa promosheni hiyo ya Mimi ni Bingwa iliyoanza mwishoni mwa mwezi wa Novemba mwaka jana, imelenga kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa jamii inayoizunguka na kuwaunganisha mashabiki wa soka na michezo ya kimataifa.
Alimtangaza Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa kuwa ni mshindi wa wiki hii wa tiketi mbili wa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi za klabu ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.

Bw. Kajimbo anakuwa ni mshindi wa tisa wa tiketi toka promosheni ilipoanza baada ya Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mwenyekiti wa Kijiji cha  Nang’olo katika wilaya ya Kilwa - Mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro mkoani Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini Dar es Salaam na Salma Juma Mughery kutoka Dar es Salaam, waliojishindia tiketi katika droo za kila wiki zilizopita.

Mmbando pia aliwatangaza washindi wawili wa shilingi milioni 5 kila mmoja wa wiki kuwa ni Bw. Uruma Samwel Mkongwa kutoka Usa River mkoani Arusha na Filemon Nathaniel Mgaya kutoka Dar es Salaam pamoja na washindi wengine 10 waliojishindia shilingi milioni 1 kila mmoja.  

“Zaidi ya shilingi milioni 324 zilitengwa kama zawadi ya pesa taslim kwa ajili ya promosheni ya Airtel ya Mimi ni Bingwa, inayowapa fursa washiriki wa Mimi ni Bingwa kushinda kila siku na kila wiki,” alisema.

Mmbando alisema kuwa mwenendo wa washiriki wa Mimi ni Bingwa kuendelea kujikusanyia pointi unazidi kutoa amasa.

“Bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa, ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50. Nawaasa wateja wa Airtel ambao bado hawajajisajili katika promosheni hii kuwa hawajachelewa; bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa. Ili kuingia katika promosheni hii mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BNGWA” kwenda namba 15656, kwa kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza kuwa mshindi wa milioni 50 au zawadi nyinginezo nyingi,” alisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.