ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 30, 2013

MABONDIA JAPHET KASEBA, ALIBABA KUZIPIGA DESEMBA 21 FRIENDS CORNER HOTEL DAR.


Mabondia Japhet Kaseba wa jijini Dar es Salaam, na Alibaba Ramadhan wa jijini Arusha, wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 Decemba, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner hotel,kuzichapa katika pambano la ubingwa wa pst
Pambano hilo liloandaliwa na Promota Ibrahim Kamwe chini ya  BigRight Promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kama Karage Suba na Fadhil Awadh, watakaozichapa kuwania ubingwa wa Mkoa katika uzito wa wealter Kg66 pambano la raundi kumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe, alisema kuwa  zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa, pia mahasimu wawili wa uzito wa juu Lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku Kheri (ndota) ikiwa ni marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi. 

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni pamoja na Bondia Adam Yahaya (Baby Edo) atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku (Tyson) atacheza na Shah Kassim,  kukumbushia Enzi za akina Stanley Mabesi , Jocky Hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena Rajabu.

Wengine ni Issa Omar  atazipiga na Haji Juma wa Tanga, Moro Best atapigana na Shafii Ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengera. 

Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huo na wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.

Kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi kutoka Kampuni ya Kiwango Security na jeshi la polisi amblo limeahidi kutoa mchango mkubwa ili kufanikisha pambano hilo.

PIKI PIKI ITAKAYOGOMBANIWA NA MABONDIA NASSIBU RAMADHANI NA MOHAMED MATUMLA YAONESHWA

Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju. 

Mratibu wa mpambano wa ndondi Kaike Siraju akiojiwa akiwa juu ya pikipiki itakayogombaniwa na mabondia Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani siku ya Desemba 25. 
Bondia mkongwe nchini Rashid Matumla akihojiwa juu ya pikipiki itakayo gombaniwa kati ya mwanae Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani siku ya Desemba 25.

Friday, November 29, 2013

JOSE CHAMELEONE ASAINI KUPIGA SHOW MOJA TAKATIFU TAREHE 24 DEC 2013 MKESHA WA CHRISTMAS JIJINI MWANZA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone akisaini mkataba wa wa kupiga show jijini Mwanza itakayofanyika mnamo tarehe 24/12/2013 mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas kuanzia saa 12 jioni hadi majogoo, tukio linalotazamiwa kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Picha zaidi za Mwanamuziki mkali Afrika akisaini mkataba baina yake na viongozi waandaaji wa Show hiyo. Makubaliano haya ya kuweka mkataba yamefanyika jumatatu ya wiki hii tarehe 25/11/2013 jijini Kampalanchini Uganda.
Mwanamuziki Dr. Jose Chameleone (katikati) akiwa na Mapromota wa show itakayofanyika jijini Mwanza Dennis Mshema (Kushoto) na Mr. Ben Mwangi (kulia) mara baada ya utiaji wa saini wa kupiga show moja kali tena takatifu itakayofanyika mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Christmas katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
 Kwa mujibu wa moja wa Mapromota hao Mr. Ben amesema kuwa ile kiu ya mashabiki wa muziki wa ukweli toka kwa Mwanamuziki Jose Chameleone sasa inakwenda kupata dawa yake, kwani maandalizi mazuri yameanza kufanyika kuhakikisha kila kilichobora kina tukia kwenye jukwaa la burudani siku hiyo ya mkesha wa Christmas.

"Tutafunga sound mpya ya mtikisiko, tutajenga jukwaa kubwa bora tena la kisasa, tutafunga taa za kisasa pamoja na huduma nzuri kwa wateja watakaofika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, nia na madhumuni kuufanya usiku huo kuwa mkubwa, mzuri wenye mengi maajabu katika burudani" Alisema Ben.

 Ameongeza kuwa bado milango iko wazi kwa makampuni mbalimbali na sekta binafsi kushiriki katika suala zima la udhamini. Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0752813212.

Mbali na kuwa na masongi makali kama Bei kali, Kamila na kadhalika ambayo hadi sasa utamu wake uko pale pale Jose Chameleone kwa sasa anatikisa ulimwengu wa burudani ya muziki na ngoma zake kali kama Badilisha, Sumula, Valu valu, Tubonge na nyingine kibao... 

Thursday, November 28, 2013

KWA MARA YA KWANZA KOMBE LA DUNIA KUIKANYAGA ARDHI YA JIJI LA MWANZA KESHO.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza na mbele ya waandishi wa habari na kamati ya maandalizi juu ya ujio wa Kombe la dunia ambapo jiji la Mwanza limetunikiwa nafasi ya kwanza nchini kulipokea kombe hilo. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo na MNEC wa wilaya ya Tarime ambaye pia ni mkurugenzi wa Nyanza Bottling co. ltd, Christopher Gachuma. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza na mbele ya waandishi wa habari na kamati ya maandalizi juu ya ujio wa Kombe la dunia ambapo jiji la Mwanza limetunikiwa nafasi ya kwanza nchini kulipokea kombe hilo. 
Mwakilishi wa Coca Cola Nchini bw. Eyebolt Gretchen (katikati) akizungumzia madhumuni  ya ziara iyo yenye lengo la kukuza mchezo wa soka.  Coca cola imemekuwa mstari wa mbele kwenye jitihada za kukuza soka nchini ikiwa imewekeza pia kwa vijana kupitia mashindano ya Kopa Coca cola.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu amewahakikishia wanachi wote wa Mkoa wa Mwanza amani na utulivu, aidha amewaomba wananchi kutokuja uwanjani wakiwa na watoto wadogo ili kuepusha adha wanayoweza kupata watoto hao kutokana na msongamano.
Wadau wakiwa makini kusanyikoni.


Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia litapokelewa Mkoani Mwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba.
  
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, mbele ya waandishi wa habari na kamati ya maandalizi ya ujio huo katika ukumbi wa Mwanza Hotel hii leo.

Ndikilo amesema kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kombe hilo kugusa ardhi ya mkoa wa Mwanza hivyo amewataka wanachi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kunakshi na kutia mashamsham ya ujio wa kombe hilo lenye historia.

Naye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye yupo ziarani katika Mkoa wa Simiyu amekubali kuwa mgeni rasmi kulilaki kombe hilo litakalotua nchini katika ardhi ya mkoa wa Mwanza kisha jijini Dar es salaam.,

Amesema kombe hilo litawasili katika uwanja wa ndege wa mwanza majira ya saa tatu asubuhi na badae kupelekwa katika uwanja wa CCM Kirumba, ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya wananchi watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Coca Cola Nchini bw. Eyebolt Gretchen, amesema ujio wa Kombe hilo kwa mara ya tatu katika nchi ya Tanzania umekuja kutokana na utulivu na amani iliyotawala nchini sanjari na ukarimu wa watu wake, Miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimekuwa na utulivu hata kufanya kutembelewa na kombe la Dunia ni Tanzania, amesema na kuongeza kwamba, kama Coca cola wamekuwa mstari wa mbele kwenye jitihada za kukuza soka nchini ikiwapo mashindano ya Kopa Coca cola.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu amewahakikishia wanachi wote wa Mkoa wa Mwanza amani na utulivu, aidha amewaomba wananchi kutokuja uwanjani wakiwa na watoto wadogo ili kuepusha adha wanayoweza kupata watoto hao kutokana na msongamano.

Hii ni mara ya tatu kombe hilo kutua  nchini ambapo mara zote limekuwa likipokelewa na kulakiwa na wananchi waishio katika Mkoa wa Dar es Salaam. 

Ujio wa kombe hilo si tu kwamba linakuja kutazamwa na wananchi wa Mwanza bali pia ni fursa nzuri kwa mkoa huo kujitangaza kimataifa, kutangaza rasilimali zinazo patikana katika Mkoa huo na lakini pia ni chachu kwa vingozi kuona kuwa kuna umuhimu wa kuipa kipaumbele michezo yote. 

UMIA UJAE NA MAENDELEO YA JIJI LA DAR.

Hii ndiyo hali halisi hivi sasa jijini Dar es salaam.... Na hapa ni eneo la Posta ya zamani ambapo hivi sasa hakuna daladala linaloruhusiwa kuingia eneo la Posta ya zamani hadi Kivukoni, yote ni kipisha ujenzi wa njia za mabasi yaendayo kwa kasi,

Si unajua tena maendeleo huja na adha yake, takribani miezi mitatu itachukua kukamilika kijipande hiki kama ilivyoahidiwa na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi.
Shughuli ndiyo hivyo tena.
Kama Ulaya vile pakikamilika.
PICHA NA JIMMY JAM.

BONGE AINASA BAR INAYOTAPISHA MAJITAKA BARABARANI.

Mapema asubuhi ya leo yule Kamanda mbishi wa kuzibaini Kero na kuzitafutia uatatuzi nchini, Bonge wa kipindi cha Power Break Fast ya Clouds Fm, aliinasa bar ya mwananchi mmoja mfanyabiashara ikitiririsha barabarani maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi na kuruka naye live kupitia 'Fuka la Mbongo' (radio ya watu).

Ni bar inayopatikana barabara ya Bagamoyo karibu na maeneo ya Samaki Mbichi njia panda ya kuelekea Goba. Bar hiyo (jina limehifadhiwa) inayojihusisha na uuzaji wa vyakula na vinywaji inatajwa kuwa katika kipindi cha mvua au majira ya usiku au pengine alfajiri sana wakati barabara hiyo ikiwa na watu wachache ndipo wadau wa bar hiyo hufanya huo mchezo mchafu ambao umekuwa hatari kwa afya za majirani na wapita njia wa eneo husika .

Mpira ambao unasaidiwa na pump yenye jenereta katika kufyonza maji taka toka kwenye mashimo ya maji taka na kuyamwaga maji hayo machafu barabarani.

Maji hutuama hapa na kusababisha harufu kali kwa wapitao.
Hivi tunapokupa taarifa hizi vifaa vyote vilivyokuwa vikifanya shughuli hiyo chafu, nikimaanisha pump na jenereta vimekamatwa na Mwenyekiti wa Serikali za mitaa na kuhifadhiwa ofisini kwake ambapo kesho kupitia Power Break Fast mwenyekiti huyo atasikika na kuzibainisha hatua za kisheria zilizochukuliwa kwa mmiliki wa bar hiyo.
PICHA NA 'BONGE'

INTRODUCING FAHARI HUDUMA FROM CRDB BANK

 
 
 
Mpendwa Mteja,
Furahia huduma za benki popote uendapo ndani ya Tanzania. Mtembelee wakala wa FahariHuduma alie karibu yako na uweze kufanya miamala yako ya kibenki kwa haraka na wepesi. Kupitia wakala wa FahariHudumaunaweza kufanya miamala ifuatayo:
  • Kuweka fedha kwa kutumia kadi au bila kutumia kadi
  • Kutoa fedha kwa kutumia kadi au kwa kutumia huduma ya Cardless
  • Kufahamu salio la akaunti
  • Kupata taarifa fupi ya akaunti
  • Kulipia bili mbalimbali
  • Kupata kadi ya TemboCard Fahari
  • Kufungua akaunti
FahariHuduma ni mfumo wa kwanza nchini Tanzania wa utoaji wa huduma za benki kupitia mawakala unao kuhakikishia urahisi wa kupata huduma za benki jirani nawe kupitia wakala wetu aliechaguliwa.
Sasa huhitaji tena kutembea umbali mrefu ili kulifikia tawi la Benki ya CRDB kwa kuwa mawakala wetu wanapatikana mahali ulipo.

Jinsi FahariHuduma Inavyofanya Kazi


  • Miamala yote inayofanyika hutoa matokeo sahihi kwenye akaunti ya mteja muda huo huo.
  • Miamala yote huunganishwa moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa Benki ya CRDB
  • Kila muamala unapofanyika huambatana na risiti mbili ambapo moja hubaki kwa wakala na nyingine hupewa mteja.

Namna ya kuwa wakala
Ungana nasi kupitia
  
Wasiliana nasi
Simu: +255 759 001 230 | 0222136232
Barua pepe: customer-hotline@crdbbank.com
 
 

BURIANI MSANIFU WA UHURU DUNIA MZOBORA.

Mwandishi wa siku nyingi na aliyekuwa Mhariri Msanifu (Sub-Editor) wa magazeti ya UHURU/Mzalaendo, Dunia Mzobora, amefariki dunia jana alfajiri katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikopelekwa usiku kwa matibabu baada ya kuugua ghafla shinikizo la damu.
 R.I.P Dunia.
BOFYA HAPA CHINI KUSOMA ZAIDI.
http://lukwangule.blogspot.com/2013/11/mhariri-uhuru-afariki-dunia.html

Wednesday, November 27, 2013

JAMII YATAKIWA KUTUMIA NAFASI ZILIZOPO KUPAMBANA NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

 Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu Ameitaka jamii na kila mtu kutumia nafasi alonayo kuzuia ukatili wa kijinsia ili kuboresha afya ya jamii.

Mangu ameyasema hayo katika uzinduzi wa siku 16 za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake uliofanyika juzi katika viwanja vya line polisi Mabatini jijini Mwanza.

“Uwepo wa matukio hayo unaleta haja ya walio katika nafasi kusimama na kuzuia vitendo vya ukatili” alisema kamanda Mangu

Mpaka sasa mkoani Mwanza matukio ya mauaji ya kishirikina yamefikia 40 na watu 44 wakipoteza maisha katika matukio hayo wanawake wakiwa ni 34 na wanaume 10 tu. Huku watuhumiwa 133 wakishikiliwa na jeshi la polisi.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI Bw. Ramadhan Masele amesema kampeni hiyo ya siku 16 inalenga kuamsha ari kwa watanzania kupambana na ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake na kauli mbiu ya kampeni hiyo ni “Funguka ! Tumia mamlaka yako, zuia ukatili wa kijinsia, kuboresha afya ya jamii.

Bw. Masele amebainisha kuwa kukosekana kwa sheria maalumu inayohusika na ukatili wa kijinsia, mitazamo hasi ya jamii dhidi ya wanawake, ukosefu wa huduma bora za afya na vitisho kwa wahanga wa ukatili ni baadhi ya changamoto zinazo wakabili katika harakati za kupambana na ukatili wa kijinsia.

Pia Diwani wa kata ya Mbugani Bw. Hashim Hassan Kijuu ameitaka jamii kushirikana katika ngazi zote toka familia, mtaa mpaka taifa kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Shirika la KIVULINI limekuwa likendesha harakati za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na siku ya Novemba 25 ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake duniani.

Awali kabla ya maadhimisho yaliyanyika maandamoano kutoka viwanja vya wa Ghand Hall hadi eneo la tukio uwanja wa Mabatini jijini Mwanza.
Ngoma asilia. 
Burudani kama sehemu ya kunakshi kusanyiko la maadhinisho hayo.