ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 22, 2013

YALIVYOKUWA MAZISHI YA GABRIEL ANDERSON MUNISSI HII LEO.














Marehemu Gabriel Anderson Munissi aliyefariki dunia tarehe 19 Nov 2013 amezikwa leo Nkokashi Masama wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro ambapo ndugu jamaa na marafiki aliofanya kazi nao enzi za uhai wake walisafiri toka pande mbalimbali hapa nchini wakiwemo wengi wadau kutoka jiji la Mwanza, kuhudhuria mazishi hayo yaliyokuwa yamegubikwa simanzi kubwa.

Gabriel alifariki dunia mara baada ya kujifyatulia risasi kichwani ikiwa ni kabla ya kufanya mauaji kwa watu wawili na kujeruhi wengine watatu wawili kati yao wakiwa taabani na kisha baadaye (jana) mmoja kati ya hao walio kuwa taabani (niki maanisha majeruhi Fransis Shumira) alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

Kufariki dunia kwa Francis kuna fanya idadi ya watu waliofariki dunia katika tukio hilo hadi sasa kufikia wanne (akiwemo gabriel) huku ikiacha majeruhi wawili mmoja Christina Alfred Newa ambaye ni mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.

Aidha mipango ya mazishi ya mtumishi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar es salaam, Alfa Alfred Newa inafanyika nyumbani kwao Ilala karibu na klabu ya wazee na maziko yakisubiri kutengemaa kwa afya ya mama mzazi.

Familia imekiri binti yao Christina na Marehemu Munisi kuwa walikuwa na mahusiano lakini ni zamani na walitengana kutokana na vurugu alizowahikumfanyia siku za nyuma.

Marehemu Alfa Alfred Newa pia alikuwa mfanyakazi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar, wakati Shumira ni Baharia.

WIKIENDI HII NJOO MWANZA.

Sun set at the area...jicho langu toka jiji la Mwanza twaita Rock City.
Yatch Club Mwanza.....
Jicho toka Yatch Club kuelekea ziwa Victoria.
Ni safari za kitalii.
Zaidi ya Utalii hapa...
Je unataka kupiga makasia kwa speed ya jet?
Yatch Club na yanayojiri ziwani.
Sasa tujumuike pamoja...
Shughuli imemalizika na sasa ni wasaa wa....
Hamia kisiwa cha saa nane mwendo mfupi toka mwambao huu.
Jionee maandari safi yenye wanyama wa aina kwa aina.
Maandari.
Staajabu mawe.
Hata miti pia ni sehemu ya utalii....

KAMATI KUU YA CHADEMA YAWAVUA UONGOZI ZITTO KABWE, DR KITILA MKUMBO NA SAMSONI MWIGAMBA

Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema imewavua Uongozi Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri uliowahusisha na mpango wa kukipasua Chama vipande vipande. Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini. Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao cha kamati kuu kulichokuwa kimefanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu amesema katika Waraka huo kulikuwa na mtu anayejukana kama MM ambaye ni Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya Chadema.


Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2. Mh Tundu Lissu amesema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA. 

Mh Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu. Mh Tundu Lissu Amesema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake


Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.


Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Lissu amesema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.

Wakati huo huo kamati kuu imemteua Mh Tundu Lissu kuwa Mwanasheria mkuu wa Chama.

PICHA YA WIKI.

Ni ya Salim Kikeke wa BBC Swahili 'Piga kalamu.. usipige risasi..'

WASHINDI WA CLEAN HOUSE WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO TOKA COLGATE PAMOLIVE

 Valarie Urio wa Dar es Salaam, anapokea jiko la Gesi cooker kutoka kwa Bi, Hytham Ahmed wa masoko Ltd kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.
 Abeid Semira wa kutoka Mwanza anapokea zawadi yake kutoka kwa Bi, Hytham Ahmed wa Masoko Ltd. kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.
Washindi wa Clean House wakabidhiwa zawadi zao toka Colgate Pamolive
Wakazi wa jijini Dar es salaam na mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya waliokuwa wakinunua bidhaa za  Sta- Soft  na Axion (sabuni ya kuoshea vyombo) zinazosambazwa na Colgate Pamolive wamekabidhiwa zawadi zao kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.

Kampuni ya Colgate Pamolive imekuwa ikiendesha promosheni  maalum ya CLEAN HOUSE kwa muda wa miezi miwili iliyokuwa na lengo la kuwafahamisha watanzania jinsi bidhaa zao za Sta- soft ambazo ni maalum kwa kufulia nguo na Axion maalum kwa usafi wa vyombo vya nyumbani. Bidhaa hizi ni maalum  kwa kufanya usafi kwa ufanisi mkubwa.

Akieezea bidhaa hizo Afisa Masoko wa Colgate Pamolive  Bw, Meshack Mdingi alisema “ Lengo la promosheni  hii ni kuwajulisha wateja wetu jinsi wanavyoweza kuepuka magonjwa ya ngozi kwa kufua nguo zao na Sta- soft inayotunza nguo zako na kuziweka laini  wakati wote na harufu nzuri na  kusafisha vyombo vya ndani.  Wateja wetu tunawashauri watumie  bidhaa yetu ya Axion inayofanya vyombo vibaki na mng’ao wake mzuri siku zote”

Walioibuka washindi kwenye promosheni ya Clean House ni wale wote walionunua bidhaa hizi kati ya September na Oktoba ambapo walichaguliwa kupitia droo maalum iliyofanyika wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar Es Salaam.

Baadhi ya walioibuka washindi  kupitia promosheni hiyo ni  Valeria Urio mkazi wa Dar Es Salaam, aliyejishindia Jiko la Gas cooker,  Abeid Semira mkaazi wa Mwanza aliyejishidia Jagi la Kuchemsha maji, Hassan Ibraim mkaazi wa Tanga kati ya wengine 50.

Bw, Mdingi alisema hadi kufikia mwisho wa promosheni  wameweza kuwaelimisha watu wengi kuhusiana na Usafi wa jamii, pia kurudisha faida wanazopata kwa jamii kwa kutoa zawadi ambapo jumla ya Majiko ya Gesi 3,Seti za Masufuria 8,  Seti za jagi za maji 8, pamoja na  mashine za umeme za kukausha mkate (Toaster) 8 za  kisasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na zawadi nyengine ndogo ndogo.

Kupitia bidhaa zetu bado tutaendelea kuwafikia wateja wengi kwa kufanya promosheni kama hizi huku tukitoa elimu kuhusiana na usafi kwa jamii na kutoa zawadi tofauti tofauti ili kuwafaidisha wale wote wanatumia bidhaa zetu za Colgate Pamolive, alimazia Bw, Mdingi

TAMPERE WAKABIDHI GARI LA ZIMAMOTO KWA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA.

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akihutubia wananchi na wageni waliofika katika viwanja vya Ghand Hall,  kushuhudia makabidhiano ya msaada wa gari la Zimamoto yaliyofanywa na jiji rafiki la Tampere toka nchini Finland kwa kukabidhi msaada huo kwa jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (kushoto) akikata utepe kwa kushirikiana na Bi. Kaisn Anttoncn ambaye ni Director Chair of PST wa jiji la Tampere.
Bi. Kaisn Anttoncn ambaye ni Director Chair of PST wa jiji la Tampere naye akikata kipande cha utepe kwaajili ya kumbukumbu huku akishuhudiwa na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akikagua ubora wa gari hilo toka katika uskani huku akiwa na Bi. Kaisn Anttoncn ambaye ni Director Chair of PST wa jiji la Tampere. Thamani ya gari hili ni zaidi ya shilingi millioni 500 za Tanzania.
Mstahihi Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akimkabidhi funguo Kaimu kamanda wa kikosi cha Zimamoto mkoa wa Mwanza Christon Mamyologa mara baada ya kupokea msaada huo toka jiji rafiki la Tampere toka nchini Finland.
 Kaimu kamanda wa kikosi cha Zimamoto mkoa wa Mwanza Christon Mamyologa akionyesha ufunguo wa gari hilo sambamba na kadi yake mara baada ya makabidhiano.
Sasa ni wakati wa majaribio...
Wafanyakazi wa zimamoto wakikimbilia eneo la tukio...!!
Stop..!! amri toka kwa kiongozi.
Zimamoto kikazi zaidi...!!
Picha ya pamoja ya wadau ofisi ya Halmashauri ya jiji la Mwanza pamoja na jiji rafiki la Tampere.

P-SQUARE WATINGA BONGO.

Wanamuziki wa kundi la P- Square Peter na Paul Okoye wakisalimiana na Mtangazaji wa kiruo cha Televisheni cha EATV, mapema baada ya kuwasili jana katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka katika bendi yao. Tamasha hilo limeandaliwa naEast African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mwanamuziki wa kundi la P- Square Peter Okoye akizungumza na waandishi wa habari, mapema baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka katika bendi yao.  Pamoja nao katika picha ni pacha wa msanii  huyo Paul Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P - Square Tamasha hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akizungumza na wasanii Peter na Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  na Afisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo  Ibrahim Kaude, wakiongozana na wasanii Peter na Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.
Mwanamuziki wa kundi la P - Square, Paul Okoye akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarake Nyerere, Tayari kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania, Msanii huyo aliambatana na Pacha wake Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P- Square. Wasanii hao wameambatana na wenzao 13 ambao watatoa burudani jumamosi ya tarehe 23 Novemba. Tamasha hilo limeandaliwa na East African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

SPACE AVAILABLE AT GEPF HOUSE

GEPF HOUSE
Building along Ally Hassan Mwinyi Road conveniently located at Victoria with a ten minute drive to city centre during low traffic time.
Space available for leasing
  1. Ground floor for Bank and shops
  2. 1st to 7th floor office block
  3. 10th floor conference space
We have space ranging from 130 sqm to 364 sqm on Wing A, Wing B and Wing C
Price per sqm is USD 16 on Ground floor and 15 on all other floors
Service Charge is USD 3.00
Services: Backup generator, 3 lifts, Water, Security, Ample Parking, Pantry on each floor/wing,
For space contact Property Manager TRUDE on TEL. +255 246 1105; or Mobile: +255 716 872 481 or email:trudehenryj@yahoo.com

Wednesday, November 20, 2013

HII NI YA SHARO MILLIONEA.



Hiki ni kipande kifupi ambacho kipo kwenye movie mpya aliyocheza marehemu Sharo Millionea na swahiba yake Kitale. Ukiangalia scene hii utaona marehemu alikuwa anaendesha gari speed ambapo alikuwa anagombezwa na Kitale kwanini anaendesha gari speed uswahilini, na gari hilo linaloonekana ni gari ambalo marehemu Sharo Millionea alipata nalo ajali akiwa anaelekea Tanga.