ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 4, 2013

UKATILI WA BABA WAKWAMISHA NDOTO ZA MSICHANA JULIANA.

Msichana Juliana  akiwa nyumbani  kwake  akiandaa  chakula  kwa ajili  ya wateja  wake 
Na. Revocatus Herman
Tumeshuhudia   jamii   ikikumbwa  na ukatili  wa  kijinsia   hasa kwenye  vipigo, lakini  kwa msichana  Juliana  mambo yalikuwa ni  tofauti  yeye  ni  mtu   aliyeonja  ukatili wa kijinsia  katika  Nyanja  ya  kielimu. Baba mzazi wa Juliana aliamua makusudi kuelekeza ukatili wa kijinsia  kielimu kwa binti yake, fuatilia  makala  hii  yenye  simanzi  na masikitiko.
Baba   hakutaka nisome  kabisa, kwani kila mara  nilipomwambia kuwa nahitaji  kusoma aliniambia  kuwa, kusoma kwa mtoto wa kike  hakuna  maana  yoyote mtoto wa kike  ana jukumu moja  tu, ambalo nikuolewa. Alisema Juliana alipokuwa akinisimulia  kisa  chake huku akitokwa na machozi.
Juliana  aliniambia kuwa  kila  mara  alijitahidi  kumshawishi Baba  yake  juu  ya  yeye  kupelekwa   shule  lakini  Baba yake    alilirudia  kauli  yake  kuwa, kusoma ni wajibu wa mtoto wa kiume. Baba  yake Juliana  alikuwa na watoto  wane, watatu  wakiwa wanaume, kwa upande wa  watoto wa kiume wote walipelekwa shule  kasoro ni  Juliana  tu  ambaye alinyima  haki ya  kielemu.
Ni ukweli  usiopingika  kuwa  kunyimwa   kwa fursa  kwa Juliana  kulimfanya Juliana  awepo  hapo nilipomkuta, nilikutana  na Juliana katika  standi kuu  ya  mabasi  ya Nyegezi   Jijini Mwanza akiwa  ameketi  kwa hudhuni huku pembeni yake  kukiwa na sufulia  la uji wa ulezi aliokuwa akiuuza.
Kutokana na kuwa mapema  sana  asubuhi wateja  walikuwa  hawajafika  eneo  hilo, hivyo basi nilipata  nafasi  ya kumuuliza juu ya  maisha yake   yaliyomfanya ajikute kuwa mama lishe  au ntilie , hapo ndipo aliporejea  historia  yake ya miaka  kumi  iliyopita iliyojaa  uchungu  na masikitiko  ya ukatili wa kijinsia  katika  Nyanja  ya  elimu.
Juliana alisema kuwa  kaka  yangu namini leo  hii  na mimi ningekuwa kama  mama  Anne Makinda ambaye ni spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanznaia,  endapokuwa  baba  yangu  hasingenitendea  unyama  wa kijinsia kwa kuninyima  haki  ya kuwa na elimu  basi  ningekuwa mbali  kaka  yangu, lakini  ndiyo  hivyo  tena naishia  kwenye kuuza uji.
Juliana    aliniambia  kuwa,   kaka yangu   makubwa yalinipata  kwani  nakumbuka  mara  kwa mara  nilikuwa  namkumbusha  baba  juu  ya  kiu  yangu  ya  kusoma, lakini  kuna siku  sitaisahau, kwani  nilipomkumbusha  baba  juu  ya  suala hilo, aliishia  kunipiga  huku  akiniambia  nishike  kichwa  changu kwa mikono  miwili  na kumzunguka  alipokuwa  amesimama  bila  idadi  ya mzunguko.

Ikumbukwe kuwa  katiba  ya  jamhuri  ya muungano wa Tanzania  ibara  ya  13: 6 inasema ni marufuku   kwa mtu  kuteswa, kuadhibiwa   kinyama  au kupewa  adhabu  au kumdhalilisha. Mimi  naamini  kama mwandishi  natumia  nafasi  hii  kupinga  ukatili   wa kijinsia  hasa kwa kutumia  mbinu  za   za kuripoti   ukatili  wa kijinsia   kama  TAMWA walivyoamua  kuwajengea  uwezo  waandishi wa habari  kuripoti  matukio  hayo.

Chama  cha  wanahabari  wanawake  Tanzania  (TAMWA)  kimekuwa  kikipiga  kelele    huu  ya  ukatili wa kijinsia , lakini  bado  kuna maeneo jamii    inaendelea  na vitendo  hivyo.  Ni wazi  kuna   Msichana  Juliana  alinyimwa  haki  yake  ya kusoma kwa kuwa  tu  yeye  ni  msichana, huo  ni ukatili  mkubwa wa kijinsia.

Kwa sasa  Juliana  anaendelea  na biashara  yake  ya  mamaNtilie  na  amejiwekea  malengo  ya  kukusanya  fedha  kidogo kidogo  na mwakani  ana  mpango wa kuanza  kujiendeleaza  kielimu  kwa kupitia elimu  ya watu  wazima.
Makala hii  imewezeshwa  na TAMWA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.