ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 5, 2013

UKATILI BADO UNAENDELEA KUITAFUNA JAMII YETU

Na Neema  Joseph

Mwanza

Baadhi  ya watoto  yatima  jijini Mwanza wameangukia  katika  janga  la  unyanyasaji wa kijinsia  bila  jamii  kujua   vitendo  vinavyoendelea  katika maeneo  ya  watoto  hao  wa mitaani  hali maarufu kama (Ghetto).

Ilikuwa ni  usiku wa saa  tano  hivi nilifanikiwa  kujichanganya  na kundi  moja  la watoto hao  wa mitaani, huku nami  nikijifanya  ni  muumini wa makundi  hayo, nakumbuka  ilikuwa ni   wa mtaa  mmoja   katika  barabra  ya  Nyerere,  kando  ya barabara  hizo  utakutana  na nyumba  za ghorofa, maeneo  hayo  ndiyo makazi  ya watoto  hao wa mitaani  pamoja na maeneo  mengine jijini Mwanza.

Wakati  nilipokuwa  katika kundi  hilo la watoto wa kike walishuhudia  mwenzetu  mmoja  akifanyiwa  unyama mkubwa, kwani lilitokea  kundi jingine  la wavulana watatu  na kisha  kusogelea  kundi  hilo  na kuamua  kumchukua  binti  mmoja  ambaye alikuwa  amekaa  karibu na barabara na kisha kuingia  naye  kwenye  uchochoro  na  baada  ya muda  ilisikika  sauti  ya  binti  yule  ikiomba  msaada.

Licha  ya  kelele  zile  zilizoashiria  kufanyiwa vitendo    viovu  vya  kubakwa, baadhi  ya watu  waliokuwa kipita  eneo  lile  waliendelea  na  shughuli zao  bila hata  kuona  huruma  kwa kwenda  kutoa msaada. Nafikiri  hali  hiyo  inatokana  na historia  ya  vikundi  hivyo  kuwa ni vya kinyama  na vinatembea  na silaha mbalimbali  vikiwemo  visu , nyembe  na hata panga.

Bila  shaka  unyama  huo aliotendewa  binti  huyo  kwa mujibu wa  Chama  cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), ukatili  huo   unaangukia  katika  kundi la ukatili wa saikolojia  na unaweza kusababisha  mhusika  kujinyonga.

Hapo  ndipo nilipomuuliza  mmoja wa marafiki  wale  niliokuwa nao  sehemu ile  naye  akiwa ni mtoto wa mitaani, aliniambia  kuwa hali  hiyo ni ya kawaida  katika maisha yake  ya mitaani na wao  wameyazoea . Hapo ndipo nilipotaka kujua  msaada  wowote  wanaoupata  hasa kutoka kwa askari wa doria, ndipo  binti  huyo  aliyejitambulisha  kwa jina  Mary , ikiwa ni jina  la  bandia  nililompa  aliniambia  kuwa   hakuna  msaada  wowote  wanaoupata  kwa askari wanaokuwa doria, pindi  wanapofanyiwa vitendo  hivyo  katili

Hapo nilizidi kupata  picha nyingine  tofauti  kwa kujiuliza  inakuwaje  hata mamlaka za  usalama  kama  jeshi la polisi   kutotambua unyama  huo wa watoto  wa mitaani  ?. Kimsingi    kunakuwa na makundi mengi  ya watoto  hao wa mitaani, wanazidiana  kwa rika  na  umri, hivyo wale  wakubwa wanakuwa na sauti  dhidi  ya wale wadogo wanaoingia  kwenye  maisha  hayo.

Pia  uchunguzi wangu ulibaini  kuwepo kwa vyeo  ndani  ya makundi  hayo, kuna wanaojiita  King, ikiwa ndiyo  viongozi wa makundi, na kuna wale  wa ngazi  ya  kati wanaotumwa  na viongozi  wao hasa kwenda kufanya  uhalifu  sehemu  fulani na kuleta  watakachokipata  huko.

Katika  ukatili wa jinsia  makundi  hayo  yanahusika kwa kiasi  kikubwa, kwani  king  au  mtawala  anapohitaji  kufanya  tendo  la  ngono, basi atatoa  amri  ya kuletewa binti  katika  maskani  yake  na wale  wa kati watatekeleza jukumu  hilo  kwa kuhofia  kupatwa  na  adhabu kama watashindwa kutekeleza jukumu hilo.

Ni muda  muafaka  sasa  jamii  kusimama  na kuungana  na  Chama  cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania (TAMWA )kupinga  ukatili  huo  wanaofanyiana  watoto  hao wa mitaani .

Nazo  takwimu  za benki ya  dunia  zinaonyesha  kuwa  wanawake  wenye  umri  wa kuanzia  miaka  15 – 44   wapo  katika  hatari  kubwa  ya   kubakwa kuliko  kuugua  saratani, kupata   ajali , vita   na mlaria.

Pia  licha  ya  sheria  ya  nchi  inayoeleza kuwa endapo  mtu  atabainika kuhusika  kufanya  ubakaji  atahukumiwa  miaka  thelathini  jela, lakini  bado  vitendo  hivyo  vinaendelea, lakini  swali la msingi ni  nani  anasimamia vitendo  hivyo   kwa makundi kama watoto wa mitaani? Je watoto hao wa mitaani  wamepewa  elimu    ya  kuripoti  vitendo  hivyo  vya kinyama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.