ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 13, 2013

KULALA KIDOGO MCHANA

 Je, umewahi kulemewa na usingizi baada ya chakula cha mchana? Hiyo haimaanishi kwamba hukulala vyakutosha. Ni kawaida kusinzia wakati wa mchana kwa sababu joto la mwili hupungua wakati huo. Kwa kuongezea, hivi majuzi wanasayansi wamegundua kwamba kuna protini inayoitwa hypocretin, au orexin, inayotengenezwa na ubongo ambayo hutusaidia kuwa macho. Kuna uhusiano gani kati ya hypocretin na chakula?

 Tunapokula, mwili hutengeneza homoni inayoitwa leptin ambayo hutufanya tuhisi tumeshiba. Lakini homoni hiyo huzuia utengenezaji wa hypocretin. Yaani, kadiri leptininavyokuwa nyingi kwenye ubongo, ndivyo hypocretin inavyopungua na tunahisi usingizi zaidi. Labda hiyo ndiyo sababu katika nchi fulani watu hulala kidogo baada ya kula chakula cha mchana.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Rais kikwete huangalia mipira ya soka hadi usiku wa manane,huamka saa 4 na pia hulala kwa masaa mawili mchana.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.