ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 7, 2013

MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA 2014 YAPATIKANA.

Hapana shaka wapenzi wa soka barani Afrika pamoja na kuomboleza kifo cha Nelson Mandela wamekuwa wanafuatilia Droo ya kombe la dunia kufahamu nani wapinzani wa timu tano zinazowakilisha bara hilo.
Cameroon wamejikuta katika kundi gumu la A pamoja na wenyeji Brazil, Mexico na Croatia.
Dua ya Ivory Coast ya kuepuka kundi gumu sana wakati huu inaonekana imesikika, wako katika kundi C pamoja na Colomboa, Japan na Ugiriki.England watakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi D ambapo wapinzani wao ni Italia, Uruguay na Costa Rica.Mabingwa watetezi Uhispania watakuwa katika kundi B pamoja na Netherlands waliokutana nayo fainali kombe lililopita, na timu zingine ni Chile na Australia.
Kwenye kundi E Ufaransa inacheka usiku huu kwani imepangwa pamoja na Uswizi, Ecuador na Honduras.Mabingwa wa Afrika Nigeria wako katika kundi F pamoja na Argentina Iran na Bosnia Harcegovinia, ambayo inashiriki kombe la dunia mara ya kwanza.
Ghana ndiyo inayoonekana kuwa matatizoni miongoni mwa timu za Afrika. Wamejikuta katika kundi G ambapo watapamaba na na Ujerumani, Marekani na Ureno.Timu ya tano ya Afrika Algeria itakuwa kwenye kundi H na wapinzani hapo ni Ubelgji, Korea Kusini na Urusi.

MAKUNDI KWA URAHISI ZAIDI:-
Group A:
Brazil, Croatia, Mexico, Cameroon
Group B:
Spain, Netherlands, Chile, Australia
Group C:
Colombia, Greece, Ivory Coast, Japan
Group D:
Uruguay, Costa Rica, England, Italy
Group E:
Switzerland, Ecuador, France, Honduras
Group F:
Argentina, Bosnia-Herzegovina, Iran, Nigeria
Group G:
Germany, Portugal, Ghana, USA
Group H:

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.