ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 14, 2013

WAKAZI WA MWANZA SASA KUTOKA PASIANSI HADI NYEGEZI KWA KUTUMIA KIVUKO CHA MWENDO KASI.

 BILIONI 1 KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA MABATINI NA UJENZI WA NJIA NNE BARABARA YA UWANJA WANDEGE WAJA.

WAKALA wa Barabara Mkoa wa Mwanza (TANROAD) kutumia iasi cha shilingi bilioni 1.3 kukamilisha ujenzi wa Daraja la juu kwa watembe kwa miguu eneo la Mabatini Kata ya Mbugani Wilaya ya Nyamagana  Mkoani hapa.

Hatua hiyo inatokana na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuri kumwaagiza Mkandarasi Kampuni ya Nordic Consstruction Ltd ambapo garama zote zimetolewa kiasi cha shilingi  milioni 888,530,039/= kwa ujenzi na Mkataba wa Usimamizi akilipwa kiasi cha shilingi milioni 135,350,000/=  na kufanya thamani kuwa bilioni1.

Akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi mbalimbali wa Mkoa ,Wilaya ya Nyamagana, Jiji la Mwanza leo kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi katika eneo la mradi huo, alisema kwamba Mkandarasi anatakiwa kutekeleza mradi huo kwa wakati na kuzingatia Mkataba wake kutokana na kulipwa fedha yote.

Dkt. Magufuri alisema kuwa serikali kupitia Wizara yake ya Ujenzi itaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 kwa uboresha wa miundombinu ya barabara na vivuko vya majini na watembea kwa miguu ikiwa ni madaraja.

“Tuliahidi na sasa tumetekeleza, mnaona leo tumeweka jiwe la msingi na kazi ya ujenzi inaendelea naamini kufikia Desmba 25 daraja hili litakuwa likifunguliwa na sherehe za Chrismas watu watapita hapa na kupata frusa ya kupiga picha kama wanavyofanya kwenye eneo la samaki ikiwa ni kuongeza ajira na utalii”alisema.

“Tumedhamiria kupunguza msongamano wa magari kuingia mjini na kupunguza vifo ambapo takwimu za ajari zinaonyesha zaidi ya watu 12 wamekufa na wengine 20 wamepata majelaha na vilema vya maisha hivyo serikali kuchukua hatua ya kutoa pole kwa waliopoteza maisha na kuwatakia majeruhi kupona haraka amina” alisema.

Aliongeza kuwa serikali sikivu ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete itaendelea kuboresha Miundombinu ambapo hivi sasa Mkandarasi yupo eneo la mradi wa Ujenzi wa barabara ya Lami ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita 17 kwa garama ya shilingi bilioni 17.9 zilizotolewa na serikali kwa asilimia 100.

“Tumedhamilia kuondoa msongamano wa magari na watu kulazimika kutumia barabara kufika miji tayari Wizara yangu tayari imeanzisha mchakato wa kujenga kivuko cha kisasa ndani ya ziwa Victoria ambacho kitatoa huduma ya usafiri kuanziaia eneo la Pansiasi kupitia maeneo ya Kirumba mwaloni hadi Nyegezi” alisisitiza

Huku pia akisisitiza kuweka kwenye mipango ya ukarabati wa ujenzi wa barabara za Isamilo, Mabatini hadi zahanati ya Kata ya Mbugani na maeneo mengine yaliyosahulika kwa kuongeza kwenye bajeti ya mwaka ujao kupitia fedha za mfuko wa barabara ili kuiwezesha halmashauri ya jiji kuzijenga na kuziboresha.

Awali Meneja wa Tanroad Mkoa wa Mwanza Injinia Leonarld Kadashi akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo alisema kuwa Mkandarasi kwa sasa ameisha tekeleza kwa asilimia 60 ya kazi yake na tayari fidia ya shilingi milioni 9.5 imetolewa kwa uhamishaji nguzo za Tanesco maeneo yote.

“Ujenzi wa daraja hili la kisasa unaenda sambamba na upanuzi wa njia tatu badala ya mbili kwenye barabara ya Nyerere kuanzia eneo la Nata hadi Buzuruga lengo ikiwa ni kupunguza msongamano wa magari kuingia mjini wakati wa asubuhi na kutoka jioni kwani mkandarasi yupo eneo la mradi na utatumia bilioni 2 kwa awamu ya kwanza”alisema na kuongeza.

Kuwa awamu hiyo ya kwanza itaishia eneo la Sinai na awamu ya pili itaanzia Sinai na kuishia kwenye daraja la Buzuruga ikiwa ni pamoja na kuweka taa za kuongozea magari na watembea kwa miguu eneo la makutano ya barabara ya Barnaba na Mahina kwa garama ya bilioni 2 na kufanya thamani kuwa zaidi ya bilioni 4.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula aliomba kwa Waziri Dkt. Magufuri daraja hilo kuwekewa uzio ili kuzuia watoto kuvuka kiholela hivyo kuhatarisha maisha yao na kumpongeza kwa juhudi kubwa ya kuendelea kusaidia Jiji la Mwanza ambapo kiasi cha bilioni 1 alichokitoa kwa jiji hilo kinatekeleza ujenzi wa barabara za mawe ambazo ni Mkuyuni-Nyakurunduma, Capil point-Idara ya maji, Sweya-Ihumilo, 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo ametoa ombi maalumu kwa Waziri Magufuri kuweka mkakati wa kuipanua barabara ya Makongoro inayouelekea Uwanja wa Ndege toka mjini kati kuwa ya njia nne kutokana na kujengwa jengo la kisasa la kitega uchumi la Kituo cha Biashara eneo la Ghana na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege unaoendelea kujengwa kwa sasa kuwa na hadhi ya kimataifa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.