ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 28, 2013

BONGE AINASA BAR INAYOTAPISHA MAJITAKA BARABARANI.

Mapema asubuhi ya leo yule Kamanda mbishi wa kuzibaini Kero na kuzitafutia uatatuzi nchini, Bonge wa kipindi cha Power Break Fast ya Clouds Fm, aliinasa bar ya mwananchi mmoja mfanyabiashara ikitiririsha barabarani maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi na kuruka naye live kupitia 'Fuka la Mbongo' (radio ya watu).

Ni bar inayopatikana barabara ya Bagamoyo karibu na maeneo ya Samaki Mbichi njia panda ya kuelekea Goba. Bar hiyo (jina limehifadhiwa) inayojihusisha na uuzaji wa vyakula na vinywaji inatajwa kuwa katika kipindi cha mvua au majira ya usiku au pengine alfajiri sana wakati barabara hiyo ikiwa na watu wachache ndipo wadau wa bar hiyo hufanya huo mchezo mchafu ambao umekuwa hatari kwa afya za majirani na wapita njia wa eneo husika .

Mpira ambao unasaidiwa na pump yenye jenereta katika kufyonza maji taka toka kwenye mashimo ya maji taka na kuyamwaga maji hayo machafu barabarani.

Maji hutuama hapa na kusababisha harufu kali kwa wapitao.
Hivi tunapokupa taarifa hizi vifaa vyote vilivyokuwa vikifanya shughuli hiyo chafu, nikimaanisha pump na jenereta vimekamatwa na Mwenyekiti wa Serikali za mitaa na kuhifadhiwa ofisini kwake ambapo kesho kupitia Power Break Fast mwenyekiti huyo atasikika na kuzibainisha hatua za kisheria zilizochukuliwa kwa mmiliki wa bar hiyo.
PICHA NA 'BONGE'

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.