ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 1, 2013

HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO KWA SERIKALI YA RAIS KIKWETE

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Musa Leonard Mdede (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa tamko kwa niaba ya wanachuo kuiomba Serikali kutoa udhamini wa ada kwa asilimia 100 kwani wanafunzi wengi wanashindwa kumaliza masomo yao kutokana na kujikita kwenye shughuli za usakaji pesa kwaajili ya malipo, nazo ada zikiendelea kupanda kila misimu huku Serikali ikiendelea kutoa ufadhili kwa asilimia ileile.

"Tunaiomba Serikali kuongeza kiwango cha ufadhili ili wanafunzi au vijana walio na nia ya kusoma fani ya udaktari wakiwa wanalenga kuokoa maisha ya watanzania watimize ndoto zao. Tunatambua kuwa nchi yetu ina upungufu wa asilimia 60 ya madaktari wa sekta ya afya"

"Na kwa takwimu daktari mmoja anahudumia zaidi ya wagonjwa 33,000 kutokana na idadi ya watanzania wote, sasa kuendelea kuwa na vijana wanaoshindwa kuendelea na masomo ya sekta ya afya kwa sababu ya kukosa karo, nikurudi nyuma na kamwe malengo hayatotimia" Alisema Musa Leonard Mdede

Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Atukuzwe Mordekai Gwihangwe (katikati) akitoa ufafanuzi jinsi ada kubwa inayotozwa kwa wanafunzi inavyokwamisha malengo ya wanafunzi wa sekta ya Afya nchini hali inayopelekea serikali kukosa wataalamu wa kutosha. Kushoto ni Rais wa CUHASSO Musa Leonard Mdede na kushoto ni Benjamin Thomas.



MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI                              30.09.2013
(PRESS CONFERENCE)
Ndugu wana habari,napenda kuchukua nafasi hii kama Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu katoliki cha sayansi ya Afya na Tiba(CUHAS-Bugando) kwa niaba ya wanazuoni wote wa chuo hiki na kwa niaba ya wanafunzi wa sekta ya Afya wa vyuo vikuu vyote visivyokua vya umma nchini(yaani vyuo vikuu vikuu vyote vya fani ya afya vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na mashirika ya watu binafsi).Kuweza kueleza kilio chetu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo mbalimbali vya kiserikali vyenye mamlaka ya kusimamia Elimu ya juu na vyuo vikuu nchini.
I:DHANA YA ASILIMIA MIA MOJA YA MKOPO.Watanzania wengi  wakiwemo ndugu na jamaa wa karibu wanaotugharamikia katika masomo yetu wanaelewa kwamba mwanafunzi anayesoma fani za Afya kama Udakatari,Ufamasia,Uuguzi na nyinginezo kama hizo analipiwa kila kitu na serikali kupitia bodi ya mikopo kwa hiyo hahitaji msaada wowote wa kifedha kutoka kwa wazazi au walezi kwa kua anjitosheleza kwa kila kitu.Dhana ambayo kwa mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu kisichokua cha Umma ni tofauti kabisa.Kwa kua asilimia mia moja inayoongelewa ni kama asilimia hamsini tu ya karo zinazotozwa katika vyuo hivi.Wanafunzi wote wa vyuo hivi vya fani ya Afya visivyokua vya umma tumekua tukipokea kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mbili na laki sita tu(Tsh.2,600,000/=)  toka bodi ya mikopo kama mkopo kwa ajili ya Ada.Kiwango hiki kipo hivo toka wakati huo ambapo katika vyuo hivi Ada ilikua inatozwa kwa kiwango hicho.Ni takribani miaka sita sasa kiwango hiki kimebakia kama kilivo bila kuongezeka.Wakati kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa taasisi hizi.Ada zimekua zikiongezeka mwaka hadi mwaka na sasa kufikia takribani milioni nne,na zaidi kama karo katika vyuo hivi mbalimbali Ikiwa ina maana kwamba kiasi kinachobaki baada ya Tsh.2,600,000/= kutolewa kama mkopo mwanafunzi mwenyewe inatakiwa ajilipie pamoja na gharama zingine ambazo si sehemu ya karo zinazohitajika kutolewa.Wanafunzi wengi katika vyuo hivi wanasoma na kuishi katika mazingira magumu sana kwa kua gharama anazotakiwa kuchangia binafsi ni kubwa kiasi cha kuwalemea wanafunzi wengi ambao wengi wetu ni watoto wa wakulima ila tukiwa na haki ya kupata Elimu bila kujalisha hali ya uchumi wa familia zetu.CHANGAMOTO;hali hii imepelekea wanafunzi wengi wanaochaguliwa kushindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizi,lakini pia imepelekea wanafunzi wengi kupoteza mda wao mwingi katika kufanya vibarua ili kupata kiasi cha kumalizia ada ambayo imepelekea ufaulu wao kushuka na wengine kupoteza kabisa nafasi ya kuendelea na masomo.OMBI LETU KWA SERIKALI;kwa kua tumejiunga na vyuo hivi kwa mfumo halali wa Tume ya vikuu Tanzania(TCU) ambao haukuangalia hali ya kiuchumi ya familia zetu kama tutamudu au hatutamudu kulipa gharama hizi,kwa kua tulijiunga na vyuo hivi kwani tulikua na vigezo vya kusoma fani hizi kama wenzetu wanaosoma katika vyuo vikuu vya umma na hata zaidi na kwa kua tukihitimu sisi wote yaani wenzetu wanaosoma vyuo vikuu vya umma na sisi tunaosoma vyuo vikuu visivyokua vya umma tunakwenda kuhudumia na kuokoa uhai wa watanzania walewale.Tunaiomba serikali iongeze kiwango hiki tunachopewa kama mkopo kwa ajili ya ada,ili hiyo Asilimia mia moja inayosemwa iwe na maana kwetu kwa kua kwa sasa ni kama nusu tu.Wengi wanashindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizo.Katika nchi yenye upungufu wa 60% ya madaktari na wataalamu afya kwa ujumla,pia katika nchi ambayo daktari mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 33 elfu.Si vema kuona vijana wenye dhamira na nia thabiti ya kuokoa maisha ya watanzania wanashindwa kutimiza ndoto hizo za kua wataalamu wa Afya ati kwa kushindwa kulipa karo.
Tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU):Upandishwaji Ada katika vyuo vikuu visivyokua vya umma usiofuata utaratibu na Kile kinchojulikana kama “List of Approved programme fees” ikiainisha gharama za ada zinazotozwa katika vyuo vikuu vyote nchini.Tume vya vikuu Tanzania imepewa mamlaka kisheria kwa mujibu wa sheria ya vikuu No.7,2005.Kusimamia kuanzia udahili na uendeshaji wa vyuo vikuu vyote nchini vya umma na visivyokua vya umma.Central Admission system
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII;Institute of Health and Allied Health sciences
Kumekuwa na changamoto kubwa katika gharama za ada, chakula na makazi kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya Afya hasa vile vya binafsi ambapo gharama za uchangiaji zinazidi kuwa kubwa ikizingatiwa kuwa wanafunzi hao hutejigemea kiasi kikubwa na kuwa serikali kupitia wizara ya afya imekua ikitoa fedha kwa ajiri ya wanafunzi hao.OMBI LETU:-Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuweka wazi ni kiasi gani inachangia kwa kila mwanafunzi mmojammoja wa stashada katika vyuo vya afya kwa kueleza mchanganuo halisi ili kuwawezesha wanafunzi hao kutambua ni kwa kiasi gani Serikali kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii inachangia kama ulivyo utaratibu wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa shahada .
 Vilevile kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya gharama za ada kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi hao hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kutoa gharama halisi ambazo wanafunzi wa stashada katika vyuo vya Afya watapaswa kuchangia katika vyuo mbalimbali ikiwemo vile vya binafsi.
Kulingana na changamoto mbalimbali zinazozidi kujitokeza kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya, Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha  mfumo wa uwezeshaji kwa wanafunzi wa stashada na kuweka mfumo na taratibu zitakazosimamia mabadiliko ya ada katika vyuo mbalimbali vya Afya ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza vyuoni hasa vya binafsi.
Kumekuwa na uchakavu wa miundombinu inayomilikiwa na wizara ya Afya katika vyuo vya afya na hivyo kupunguza ufanisi wa masomo kwa wanafunzi hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha miundombinu mbalimbali inayomilikiwa na wizara ya afya katika vyuo vya Afya vinavyotoa stashahada.

                                                                                                Ahsanteni

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.