ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 25, 2013

SERIKALI YAIPONGEZA TIMU YA WASICHANA AITEL RISING STARS

Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza timu akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt
katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt
Kocha wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria.  halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt
Wachezaji waliozawadia kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising stars  pamoja na captain wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi  Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho kushoto) katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Naodha wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka 17 Stumai Abdalah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada yakuwa mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.

Kaptain ya timu ya wasichana Stumai ……. Akikabithi cheti cha kushinda kwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada yakuwa mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Mchezaji wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya dolla 10,000 iliyokabithiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya kuibuka washindi wa michuano ya Airtel Rising stars Afrika Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Wachezaji wa timu ya wavulana wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya halfa ya kuwapongeza iliyofanyika katika hotelya Hyatti jijini Dar es salaam, pichani kutoka kushoto Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo, wakurugenzi wa Airtel , mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah pamaoja na Salim Madadi wa TFF

Serikali yaipongeza timu ya wasichana ARS

·         Yashauri sekta binafsi kusaidi katika michezo.
Mkurugenzi wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo ameipongeza timu ya wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika juzi nchini Nigeria.

Tanzania waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali, pia amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali. Mabingwa wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani 10,000.

Katika pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna ni Shelda Boniface na  mvulana  ni Athanas Mdamu na pia amempongeza mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .

Katika mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora kwa upande wa wasichana  magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli manne , mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu upande wa wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik) na kuondoka na mpira kila mmoja.

Kabla ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao , Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.

Akiongea kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema kua mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa , amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na  DRFA

Mkurugenzi wa masoko wa Airtel bw Levi Nyakundi ameahidi kuwa Airtel itaendelea kudhamini mpira hasa wenye umri mdogo na pia kuongeza mikoa ya ushiriki  wa mashindano ya Airtel Rising Stars 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.