ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 20, 2013

KWA HALI HII ZAO LA PAMBA LITAZIDI KUPOROMOKA KILA KUKICHA.

Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akifafanua uchafuzi unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito.
Ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba nchini DKT.FESTUS LIMBU katika kiwanda cha kuchambua pamba cha Birchand Oil mill inayomwezesha kujionea uchafuzi wa pamba unaofanywa na baadhi ya wanunuzi na wakulima kwa kuchang’anya pamba, maji, mchanga na mbegu kwa lengo la kuongeza uzito.
Mbegu zilizochanganywa kenye pamba kwa lengo la kuongeza uzito
Ukaguzi ukiendelea kwenye ghala la Pamba.
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akionyesha mchanga uliochanganywa na Pamba za moja wa wakulima waliokiuzia kiwanda chake.
Ukiitizama kwa harakaharaka pamba hii unaweza kuiona kuwa iko salama, ila ukichukuwa jukumu la kuigusa ndipo utagunduwa kuwa kunachembe chembe za mchanga na uchafu mwingine ndani yake.
Hili ni lundo la mchanga wa kilo 60,000 uliopembuliwa wakati wa uchambuzi wa pamba ya msimu huu na uliopita, kwa Kiwanda cha Bilchand Oil Mill ambacho kimepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 7 kutokana na uchafuzi huo wa kuweka maji na mchanga, hadi sasa Wahasibu wake wanne (hakuwataja) wafikisha polisi kwa tuhuma hizo.  
Meneja wa kiwanda cha Bilchand Oil Mill, Mohamed Gupta akielezea uchafuzi huo ndani ya Pamba.
Kwa ukaribu zaidi mchanga uliopatikana kwenye Pamba baada ya uchambuzi wa awali.

Na Peter Fabian
MWANZA.

TATIZO la kushuka thamani ya Pamba nyeupe ya Tanzania (Dhahabu Nyeupe) kwenye Soko la Dunia na kupelekea kuporomoka kwa bei maradufu kumeishitua seikali na sasa kupitia Bodi ya Pamba nchini (TCB)imeamua kuchukua hatua za kunusuru zao hilo kwa kutangaza kuwa kuanzia msimu ujao wa kilimo utakuwa wa Kilimo cha Mkataba katika Mikoa ya Kanda ya Magharibi.
Hatua hiyo inafuatia tamko la serikali lililotolewa kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba kutoka Mikoa kumi hapa nchini kilichofanyika mwezi Mei mwaka huu Jijini humo na lile la Rais Dkt. Jakaya Kikwete alilolitoa wakati wa majumuisho ya kuhitimisha ziara yake ya siku tano Mkoani Mwanza hivi karibuni.
Mwenyekiti Festus Limbu (katikati).
Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Dr.Festus Limbu (Mb) alisema kuwa uamuzi huu umepelekea Bodi hiyo kutoa tamko la Taasisi hiyo Muhimu nchini inayosimamia zao la Pamba hapa nchini kutangaza kuwa kuanzia mwezi Novemba mwaka huu utekelezaji wa Kilimo cha Mkataba utaanza kwa Mikoa kumi ya Kanda ya Magharibi inayojishughulisha na kilimo cha zao.
“Tumezamilia kurejesha ubora wa Pamba Nyeupe zamani ikijulikana ‘Dhahabu Nyeupe’ kwa kuhakikisha msimu huu wa Kilimo wa mwaka 2013/2014 unaoanza mwezi Novemba mwaka huu kila Mwekezaji na mnunuzi wa pamba kuanza kuwekeza kwenye Kilimo cha Mkataba ambacho kimsingi ndiyo kitakuwa suruhisho la Mkulima kunufaika na Mwekezaji huyo hali itakayosaidia pamba kurejea kuwa na thamani na ubora” alisema Dr.Limbu.
Mwanyekiti huyo  alisema kuwa utekelezaji wa Mkataba huo utakuwa ni kati ya Wanunuzi, Wamiliki wa viwanda vya pamba na wakulima ambapo watatakiwa kupeleka kwenye maeneo ya wakulima vijijini Pembejeo za kilimo ikiwa ni Mbegu za Quton, Mbolea na Madawa ya kuulia wadudu na kufunga Mkataba na wakulima huku viongozi wa serikali za vijiji na vyama vya msingi wakiwa mashahidi.
Dr Limbu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Magu Mkoani Mwanza, alisema  tamko la serikali juu ya uamuzi wake wa utekelezaji wa kilimo cha Mkataba katika tasnia ya Pamba pamoja na kuwa na tija ndogo katika uzarishaji ambapo uzarishaji kwa umekuwa wa Hekali moja kutoa kilo 300 ikilinganishwa na lengo la kuzalisha kilo 1,500 kwa Hekali moja ifikapo mwaka 2015 kote nchini.
“Tunazo changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa viwanda vya kuongeza thamani, matumizi madogo ya pembejeo, kutolewa kwa pembejeo muda ukiwa umepita, kilimo kutegemea mvua za msimu na wanasiasa kutumia mwanya wa kujipenyeza na kuwachezea wakulima jambo ambalo limeonekana kabisa kusababisha ubora hafifu unaosababisha pamba kuuzwe kwa bei punguzo na kumnyonya mkulima” alisema na kuongeza kuwa
Tasnia ya Pamba ni muhimu katika uchangiaji wa pato la taifa na tegemeo la asilimia 40 ya Watanzania, lakini kilimo cha zao hilo kimekuwa kikikabiliwa na matatizo mengi na changamoto mbalimbali hali inayoonekana kudidimia kwa zao hilo kila msimu hivyo kupitishwa kwa mswada wa sheria ya kuanzishwa kilimo cha umwagiliaji kutakuwa mkombozi kwa wakulima. 
“Sekta hiyo binafsi itabidi iwekeze katika kuwapatia wakulima pembejeo na huduma zingine, badala ya kusubiri kwenda kununua pamba kwa wakulima mwishoni mwa msimu, kwa sababu mfumo wa sasa wa mnunuzi kupewa jukumu la kukusanya fedha kutoka kwa mkulima na kuziwasilisha CDTF umeonekana kuwa na matatizo makubwa” alisema Dr. Limbu

Aliitaja Mikoa ya Kanda hiyo itakayo tekeleza kilimo cha mkataba kuwa ni Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Tabora, Geita, Singida, Rukwa na Kigoma na kwamba wadau wote walio na nia ya kununua pamba msimu ujao, waanze kusambaza mapema mbegu na pembejeo (Quton) kwa wakulima ili mwakani wanunue pamba kutoka kwao na si kuvamia kununua kiholela kama ilivyo sasa.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kampuni ya ununuzi wa pamba na kiwanda kitakachoshindwa kupeleka pembejeo za kilimo kwa wakulima katika utekelezaji wa Kilimo cha Mkataba kuanzaia mwaka huu wa msimu wa kilimo mwezi Novemba, mwakani waklati wa kuanza msimu wa ununuzi wa pamba haitapatiwa Leseni na Bodi ya Pamba na halitaruhusiwa kuvamia kiholela kununua Mikoa yote.

“Leseni za ununuzi wa pamba zitatolewa kwa kuzingatia kigezo cha uwekezaji wa kila mdau katika eneo husika na si vinginevyo na hakutakuwa na ujanja ujanja kwenye kufunga mkataba na wakulima wa zao hilo ieleweke na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Kampuni husika na wakulima hawataruhusiwa kuuza pamba yao kwa mtu ambaye hakuwapa pembejeo. 

Aidha Dr Limbu alisema kuwa katika kuhakikisha utekelezaji huo unafanikiwa Ofisi za wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zitasimamia kwa karibu utaratibu huo mpya wa kilimo cha mkataba ili malengo ya kuondokana na matatizo yanayoathiri kilimo hicho yafikwe huku wachafuzi wa pamba wakati wa msimu wa kuuza pamba wakiwekewa mwarobaini wa kuwadhibiti.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.