ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 2, 2013

WATEJA WAAIRTEL KUTUMA NA KUTOA PESA BURE

Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa , Meneja  masoko Airtel money Rwebu Mutahaba kwa pamoja wakionyesha Bango la hakatwi mtu wakati wa uzinduzi  wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini

Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini. Kushoto Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa (kulia) Meneja  masoko Airtel money Rwebu Mutahaba

Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa akiongea na wahandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure itakayo wawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure, pichani Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, 


Tuma na kutoa pesa bure kupitia huduma ya  Airtel money
·         Wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure
·         hakuna makato yoyote kwenye huduma ya Airtel money – “Hakatwi Mtu Hapa”

Dar es Salaam, Tanzania, Alhamisi 1st Agosti 2013
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma za mawasilino leo imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha ijulikanayo kama ‘Hakatwi mtu hapa’ inayowawezesha wateja wake nchi nzima  kutuma na kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel money bila makato yoyote.

Promosheni ya Airtel money Bure itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.

akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa  kuzindua promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya  kifedha nchi nzima”.

Kwa upande wake Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza  kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.

“Tunayofuraha kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo hapo awali.  Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.

Airtel kwa sasa inaendesha promosheni maalumu  kwa wateja  wake ya Airtel yatosha. promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’  ni msisitizo unaoonyesha Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na  kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote  nchini. Huduma ya Airtel money sasa  bila shaka Yatosha

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.