ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 9, 2013

MWANZA YAONGOZA MBIO ZA BAISKELI ZA SAFARI LAGER KANDA YA ZIWA ZILIZOFANYIKA SHINYANGA.

Akinamama wakiwa tayari kuanza mbio zilizotia fora kuzunguka uwanja mara 10 wakiendesha baiskeli na ndoo za majikichwani.
Wanaume wakijipinda katika mbio za baiskeli kilometa 210 chini ya Udhamini wa Safari Lager. 


Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 210 wanaume Masunga Dubha kutoka mkoa wa Mwanza akifurahia kitita cha shilingi milioni moja alichotwaa mara baada ya kunyakuwa ushindi wa kwanza kwwenye mbio hizo chini ya Udhamini wa Safari Lager. 


Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 130 wanawake Matha Anthony kutoka wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza akifurahia kitita cha shilingi laki saba alichotwaa mara baada ya kunyakuwa ushindi wa kwanza kwwenye mbio hizo upande wa wanawake chini ya Udhamini wa Safari Lager. 


Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli walemavu kuzunguka uwanja mara 30 wanaume Ngalu Ngamba kutoka mkoa wa Shinyanga akipokea kitita cha shilingi laki moja alichokitwaa mara baada ya kunyakuwa ushindi wa kwanza kwwenye mbio za walemavu baiskeli za miguu mitatu kwa Udhamini wa Safari Lager. 


Mshindi wa akinamama waliokimbiza baiskeli kuzunguka uwanja mara 10 Eliza Shilu akipokea zawadi yake toka kwa mgeni rsmi wa mbio za Baiskeli za Safari Lager 2013 zilizofanyika mkoani Shinyanga.


Ilikuwa ni majira ya saa 1:30  asubuhi mbio za baiskeli za miguu mitatu zilitimua vumbi ndni ya uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga ambapo washiriki walizunguka uwanja mara 30.


Mbio za baiskeli miguu mitatu zilivyokuwa.


Hawa ndiyo washindi wa mbio hizo kutoka kulia ni mshindi wa kwanza Ngalu Ngamba, mshindi wa pili ni Peter Thomas na mshindi wa tatu Makende Ndelema.


Mshindi wa mbio za baiskeli kuzunguka uwanja mara 10 na ndoo kichwani Eliza Shilu (kushoto) akijitutumua katika raundi ya tisa ambapo hapa alikuwa tayari kesha wazidi wenzake raundi mbili hatimaye akamaliza mbio hizo akiwa mshindi.


Ni mbio za aina yake ambazo zilitia nakshi mashindano ya mbio za Baiskeli na Safari Lager mkoani Shinyanga.


Kadri muda ulivyokuwa ukisonga umati wa watazamaji ulikuwa ukiongezeka hatimaye ikafikia kipindi uwanja ukafunga kabisa na nyomi ya kutosha.


Macho yalielekezwa geti kuu.


Nyomi la wahudhuriaji mbio za baiskeli za Safari Lager 2013 mkoani Shinyanga.


Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 130 wanawake Matha Anthony kutoka wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza  akimaliza mbio...


Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 130 wanawake Matha Anthony kutoka wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza  hapa ni wakati akienda kukabidhiwa namba ya ushindi wa kwanza, pembeni yake ni mwandishi wa Star Tv Shinyanga Shahban Ley akichukuwa matukio.


Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 210 wanaume Masunga Dubha kutoka mkoa wa Mwanza akifurahia kumaliza mbio na ushindi alio upata kwenye mbio hizo.


Washiriki wengine mbio za baiskeli wanaume.


Meneja wa TBL Mkoa wa Shinyanga Robert Kazinza akizungumza na maelfu ya watazamaji wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Safari Lager 2013 zilizofanyika na kufana mkoani Shinyanga.


We ulikuwa wapi..?


Au hapa...?


Wadau wote wa nguvu wa TBL Kanda ya Ziwa wote waliweka maskani mjini Shinyanga.


Mambo ya Safari lager.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.