ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 29, 2013

MAONYESHO YA NANE YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI KUANZA RASMI KESHO KATIKA VIWANJA VYA NYAMAGANA JIJINI MWANZA

Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo Elibariki Mmari (katikati)  akizungumza na vyombombalimbali vya habari kuhusu ujio wa Maonyesho ya nane ya Biashara ya Afrika Mashariki, kulia ni Muweka hazina wa TCCIA Mwanza Bw. Majid Igangula na kulia ni Makamu mwenyekiti wa TCCIA Mwanza Bw. Leopard Lema . 
Maonyesho ya NANE ya Biashara kwa nchi za Afrika Mashariki (EastAfrica Tarade Fair) yanayoandaliwa na TCCIA mkoa wa Mwanza yanataraji kuanza rasmi  tarehe 30/08/2013  mpaka tarehe 8/09/2013 katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza yakihusisha makampuni mbalimbali ya bidhaa ndani na nje ya nchi.

Licha ya Maonyesho hayo kutumika kama jukwaa kwa makampuni mbalimbali ya ndani  na nje kuonyesha shughuli na huduma wanazozitoa pia itakuwa ni fursa ya yatatumika kama fursa ya kuanzisha mitandao katika dhana ya usambazaji wa bidhaa.


Mbali na kushirikisha wadau wa biashara, viwanda na kilimo wa nchi za Afrika Mashariki pia maonyesho hayo yatashirikisha makampuni ya wadau wa nchi za Misri, Singapole na China.


Bidhaa na huduma zisizoruhusiwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na Silaha za aina zote, Risasi, Mizinga (Bidhaa za kivita), pamoja na huduma za masuala ya  kisiasa na kidini kwani ni Biashara na Uwekezaji tu ndiyo umezingatiwa na kamati ya maandalizi

Maonyesho hayo yatazinduliwa nnamo tarehe 2 September 2013, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.