ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 23, 2013

KUMVUA UANACHAMA MEYA MATATA - CHADEMA YAANGUKA CHALI MAHAKAMANI, PINGAMIZI LAKE LATUPILIWA MBALI.



Meya Henry Matata (katikati) wakati akiendesha moja kati ya vikao vya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela, kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Zuberi Mbyana na kushoto ni Naibu Meya Dede Swila. PICHA NA MAKTABA G.sengo
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza leo imetoa hukumu na kutupiliambali pingamizi la Chama Cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) la kupinga kufunguliwa Kesi Namba 13/2012 ya kuwavua Uanachama Makada wake ambao ni Madiwani Mheshimiwa Henry Matata  (Kitangiri)na Mheshimiwa Adamu Chagulani(Igoma) iliyofunguliwa na Makada hao kupinga Kamatiku ya CHADEMA kuwavua uanachama.

Akisoma hukumu hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi katika Mahakama kuu hiyo Jaji A.N.M Sumari,Alisema kwamba katika pingamizi hilo lililowasilishwa katika Mahakama hiyo na Wakili Kimomogoro aliyeteuliwa na Chama hicho kuwasilisha kwa niaba ya Kamati Kuu Taifa ya CHADEMA chini ya Kiapo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini  ya Chama hicho na Mjumbe wa Kamati Kuu Slivestar Masinde aliyeteuliwa na Chama.

Utaratibu ulikiukwa kwa Wakili Methord Kimomogoro kujiandalia Kiapo hicho bila kukipeleka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini kukisaini na kula kiapo kisheria na badala yake kukiwasilisha Mahakamani hapo bila kufuata taratibu hizo za kisheria ambalo ni kosa kwa wakili kutengeneza kiapo na kukiwasilisha bila kumhusisha mtajwa katika kutengeneza kiapo hicho kisheria.

Jaji Sumari alisema kuwa kutokana na Mapungufu yaliyoonekana katika Kiapo hicho ambayo aliyaeleza kuwa ni pamoja na Kiapo alichoapa Masinde kilionyesha sahihi tu na Muhuri bila kuonyesha Jina la aliyetoa Kiapo hicho na kusema kwamba hilo ni pungufu la kwanza na kwa mujipu wa sheria hilo ni kosa na pili Pingamizi hilo liliwasilishwa Desemba 29 mwaka 2012 tayari muda ukiwa umepita wa kufanya hivyo.

Katika madai mengine katika pingamizi hlo yalidai kuwa Walalamikaji Mhe. Matata ambaye kwa sasa ni Meya wa Manispaa mpya ya Ilemela na mwenzake Mhe. Chagulani waliidanganya na kupotosha Mahakama hiyo juu ya kufutwa Uanachama kwa madai kuwa taratibu zote zilifuatwa huku bila kuonyesha ushahidi wa na utetezi wao  zaidi ya Wakili wao kusema pia hawakuwa na uhalali wa kufungua kesi hiyo.

Jaji Katika kunuku mifano ya kesi mbalimbali za aina hiyo na mapingamizi kwenye kesi za ndani na nje kwenye Mataifa ya nje kama ya nchini Uingereza  na ile ya Mhe. Mkosamali iliyokuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora aliyokuwa amewekewa pingamizi kama hilo alisema kuwa halikuwa na uhalali na kuamua kulitupilia mbali shauri hilo la pingamizi juu yake na hivyo linamhalalisha naye kufanya hivyo kama ilivyopendekezwa na mawakili wa walalamikaji.

Mawakili watatu maarufu Jijini Mwanza Salum Magongo, Boniphace Matata na Julius Mushobozi wanaowatetea walalamikaji katika kesi No. 13/2012 Mhe. Matata na Mhe. Chagulani walionekana kumzidi mbinu za kisheria Wakili Methord Kimomogoro na kumbana kila kipengele na hatimaye Pingamizi zake alizowasilisha kutupiliwa mbali na kuondolewa ili kutoa nafasi ya Kesi ya Msingi kuanza kutajwa na kusikilizwa.

Awali  CHADEMA kupitia kwa Wakili wake huyo Kimomogoro waliwasilisha madai ya mapingamizi mengine matatu ambapo katika dai la kwanza walidai kuwa walalamikaji waliofungua kesi moja katika Mahakama mbili tofauti na hiyo walikuwa na nafasi ya kukata rufaa kwenye Chombo cha Baraza kuu la wajumbe wa Chama hicho lakini waliamua kukimbilia Mahakamani 

Dai la pili lilieleza kuwa CHADEMA ni Taasisi Binafisi inayojiongoza na kusimamia Mamlaka ya Umma ambapo mtu yeyote anayejiunga nayo ni lazima ukubaliwe na kudhaminiwa na Chama hicho kugombea nafasi ya uwakilishi wa wananchi ukiwa mwanachama wa chama cha siasa na si vinginevyo kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho.

Dai la Tatu Mahakama iliyofunguliwa kesi hiyo Haikuwa na Mamlaka ya kisheria kuiwezesha kusikiliza kesi hiyo hivyo ni vyema ukatupiliwa mbali na kufutwa kwa kuliondosha shauri hilo Mahakamani kwa kuwa waliofungua hawakuwa na uhalali huo.

Maandamano ya hivi majuzi kutaka kumng'oa Meya Matata.
Katika Majibu ya mapingamizi hayo yaliyowasilishwa na Mawakili hao watatu wanaowatetea Mhe.Matata na mwenzake Mhe.Chagulani  Kwanza:-majibu yake yalieleza kuwa Tayari shauri moja lilikuwa limeisha futwa na walalamikaji kabla ya Wakili wa CHADEMA kuwasilisha madai ya mapingamizi yake ya Chama na wateja wake na kunukuu kesi ya Mhe.Mkosamali iliyotolewa hukumu kama hiyo Mahakama kuu ya Tabora.

Pili:-Mahakama hiyo inayo Haki ya Kisheria ya kuiwezesha kusikiliza kesi iliyofunguliwa kwa kuwa taratibu za Taasisi ya CHADEMA hazikufuatwa za kuwavua Uanachama na kufanyika Kibabe kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA hivyo uhalali wa walalamikaji ni sawa kutafuta haki ambayo itapatikana kwa taratibu za kisheria kwa mujibu wa madai yao na Katiba ya Chama na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee.

Tatu:-Hati ya Kiapo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini nayo ilikuwa na mapungufu na iliwasilishwa nje ya muda wa kisheria uliokuwa unatoa nafasi ya CHADEMA na Wakili wao Kimomogoro kuwasilisha kabla walalamikaji awajafuta kesi hiyo waliyokuwa wameifungua katika Mahakama nyingine isiyokuwa na uwezo wa kuisikiliza kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Kama ilivyodaiwa na wakili wao wa CHADEMA awali, lakini walichelewa na tayari kesi hiyo ilikwisha  ilifutwa katika Mahakama hiyo nyingine na kuhamishiwa katika Mahakama hiyo ambayo inao uwezo wa kuisikiliza kisheria katika hukumu iliyosomwa na kuamuliwa na Jaji A.N.Sumari mwezi Juni 31mwaka jana.

Kufatia hukumu hiyo ya leo Mahakama hiyo kupitia Jaji A.N. Sumarikuwa Kesi ya Msingi na Mahakama hiyo  itaendelea sasa  na taratibu za kuipanga,kutajwa  na kuanza kuisikiliza baada ya kuwajulishwa Mawakili wote wa pande mbili kwa mujibu wa taratibu za kisheria za Mahakama hiyo na kumaliza kusoma hukumu hiyo iliyosomwa kwa dakika 45.

Baada ya kusomwa hukumu hiyo wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya na Makada wa Chama hicho waliokuwa wamejitokeza kwa wingi katika makundi  walijikuta wakitoka kimyakimya huku wengine wakidai kuwa Wakili wao Kimomogoro ameonyesha udhaifu na hakuwa makini dhidi ya Mawakili wa walalamikaji hivyo wakidai ni vyema akatafuwa wakili mwingine ambaye anaweza kuwasilisha upya pingamizi ndani ya muda uliotolewa na Jaji kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Kijiwe Maarufu Cha KEMONDO kinachojulikana kuwana watu wa kada tofauti na wenye ueledi mkubwa wa kuchambua mambo leo kilikuwa na watu wenye nyuso za huzuni kutokana na kile kilichoshuhudiwa na kufatiliwa kwa umakini Mahakamani wakati Jaji Sumari akisoma hukumu hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.