ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 15, 2013

ASILIMIA 80% YA WANANCHI MKOA WA MWANZA WANA MINYOO: MKUTANO WA KUHAMASISHA UGAWAJI DAWA ZA TIBA NA KINGA WABAINI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akifunguwa Mkutano wa Semina elekezi kuhusu zoezi la ugawaji wa dawa tiba na kinga kwa magonjwa yaliyosahaulika kama minyoo ya tumbo,kichocho, trakoma, na usubi ambayo yamekuwa yakiathiri jamii na kuidhoofisha mkoani Mwanza. 

Dr. Upendo Mwingira.
ASILIMIA 80 ya wananchi wa mkoa wa Mwanza, wamebainika kuwa na ugonjwa wa Minyoo ya tumbo na kichocho, huku wilaya za Kwimba na Magu zikiongoza kwa ugonjwa wa Trakoma ukiwa ni utafiti wa mwaka 2004-2005 kutoka kwa Kituo cha Utafiti wa magonjwa ya Binadamu nchini (NIML)Jijini Mwanza.


Hayo yalibainishwa leo katika semina ya kuhamasisha viongozi wa mkoa, wilaya na Halmashauri za wilaya kuyapa kipaumbele Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele ili kufanikisha zoezi la ugawaji dawa za tiba na kinga  kwa jamii walio na magonjwa  aliyabainisha kuwa ni Minyoo ya tumbo, Trakona, Kichocho, ukoma, mabusha , tauni ,matende, usubi, homa ya dengi, homa ya ini na homa ya malale.

Akiwasilisha mada na kujibu maswali mbalimbali ya washiriki wa semina hiyo, Mratibu wa Mpango wa Taifa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Dr Upendo Mwingira ambapa alieleza kuwa kutokana na utafiti uliofanyika nchini mwaka 2004-2005 takwimu zinaonyesha Mkoa wa Mwanza wananchi wake kuathiliwa zaidi na ugonjwa wa miyoo. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kulia) na Katibu Tawala wa mkoa wakisikiliza kwa makini  wakati wa uwasilishwaji wa mada ya magaonjwa yaliyosahaulika.
Dr.Mwingira alisema kwamba semina hiyo imelenga kuwahamasisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugrnzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya kuweka kipaumbele kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa kuhakikisha wadau wote wanashirikishwa kwenye maeneo yao ili jamii iweze kushiriki kupata tiba na kinga za dawa hayo.


“Maeneo ya Kando ya Ziwa Victoria hususani Wilaya za Ilemela, Nyamagana, Ukerewe, Magu na Sengrema ni sehemu ambayo imetakiwa kuwekewa mkakati maalumu ili kuhakikisha magonjwa ya miyoo na kichocho yanadhibitiwa kwa kutolewa elimu na mafunzo, dawa za tiba na kinga”alisema .
Dr.Mwingira alisema kwamba zoezi la utowaji wa dawa litakuwa la siku mbili kuanzia Agosti 21 hadi 22 mwaka huu na kuwalenga watoto walio shuleni na nyumbani kuanzia umri wa miaka 5 kwa shule za awali na msingi ambao ndiyo huasiliwa zaidi ambapo kabla ya kumeza dawa hizo wanatakiwa kuwa wamekula na kushiba ili kuepuka kupata kizunguzungu na kuanguka hovyo.
Katibu Tawala wa mkoa Doroth Mwanyika (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Masenza huku wadau wengine kama Mkurugenzi wa Wilaya ya Ilemela Zuberi Mbiana na wadau wengine wa elimu wakifurahia jambo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Valentino Bangi akitoa ufafanuzi juu ya hali ya afya ya mkoa.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Merry Tesha (wa pili kutoka kushoto) akiteta na wataalamu wake.


Mkuu wa wilaya ya Kwimba Selemani Mzee (kulia) na wadau wa wilaya yake.
Wagonjwa wa Trakoma katika Wilaya za Magu na Kwimba wameombwa kujitokeza kwenda katika vituo vya afya na hospitali za Wilaya kwa lengo la kupatiwa tiba huku wale wa mabusha nao wakifanya hivyo na kupuuza na kuuondoa hofu ambayo imekuwa ikisambazwa na baadhi ya watu ambao hawana uwezo wa kitaalamu na kitabibu hasa wa vijijini na mitaani ili kupata tiba na kinga za magonjwa mbalimbali.
Mdau akichangia.

Wanahabari wakifuatilia yanayojiri.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akihutubia kusanyiko hilo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo lisisitiza kwa wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha wanajiandaa kusimamia na kutekelezwa kwa zoezi hilo kwenye maeneo yote ya Mkoa wa Mwanza.

“Mkisimamia vyema na zoezi likaenda kama ilivyokusudiwa tutakuwa tutakuwa tumetekeleza kwa vitendo sera ya kupata misaada ambayo imekuwa ikitolewa na wafadhili mbalimbali kwa serikali na Mkoa wetu ili kuona jinsi gani tunavyothamini na waokuendelea kutusaidia tena kila wakati”alisema 

Nyuzi bin Nyuzi....

Injinia Ndikilo ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza kuwapeleka watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano walio majumbani kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali kwenye maeneo yao ili kupata huduma hiyo huku pia akiwataka viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa wakiwemo wabunge kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi hilo na wale wanaoanza kujihisi kuwa na magonjwa hayo yaliyosahaulika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.