ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 11, 2013

TANZIA:- HUMPHREY SIMON KATUTOKA

Marehemu Humphrey Simon 
Ni vigumu kuamini lakini hii ndiyo hali halisi wapendwa kuwa Humphrey Simon amefariki dunia mapema leo asubuhi kiasi cha saa moja na nusu hivi mara baada ya kuanguka bafuni. Taarifa zinasema kuwa mara baada ya wana familia yake kuona kakawia kutoka bafuni ilibidi kwenda kugonga mlango, kimya kilipozidi bila majibu ndipo walipoamua kuingia bafuni na kumkuta sakafuni akihema kwa shida sana.

Huku huduma ya kwanza ikitolewa,,, Taarifa za haraka zilifikishwa kwa mjomba wa marehemu ambaye alifika eneo la tukio na kumkimbiza hospitali ya Aga Khan ili kujaribu kuokoa maisha yake na alipofikishwa hospitalini hapo wauguzi waligundua kuwa tayari amekwisha aga dunia ndipo taratibu zikafanywa mwili ukapelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando kwa hifadhi.

Merehemu kabla ya kuanzisha miradi yake binafsi ya ujasiliamali alikuwa mfanyakazi wa kitengo cha masoko cha Radio Clouds Mwanza.

Kesho ijumaa 12/07/2013 asubuhi mwili wa marehemu Humphrey Simon utatoka Hospitali ya Rufaa Bugando na kupelekwa nyumbani kwake Nyakato Sokoni ambapo taratibu za kuuaga mwili wa marehemu zitafanyika, mwili utalala hapo kisha jumamosi alfajiri safari itafanyika kuelekea mjini Musoma mkoani Mara kwaajili ya mazishi siku hiyo hiyo ya jumamosi.

Marehemu ameacha mke na mtoto mmoja.


BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.