ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 1, 2013

MWANZA NG'ARING'ARI...WIKI YA USAFI YAZINDULIWA RASMI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo (wa 5 kutoka kushoto) akiongoza shughuli za usafi ndani ya jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa wiki hiyo ambayo itaadhimishwa kila mwanzo wa kila mwezi ndani ya jiji hilo ikiwashirikisha wananchi wote kwa kila kaya na kila mtaa.
HALMASHAURI ya JIji la Mwanza imewataka vijana na wananchi kuanzisha vikundi na kuvisajili kwenye halmashauri hiyo ili kufanyakazi ya kudhibiti wachafuzi wa mazingira.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa Injinia Ndikilo amesema kuwa kupitia mpango huo utasaidia Jiji la Mwanza kuendelea kuwa safi na kuendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje sanjari na kukabiliana na changamoto mbalimbali ili kulinda hadhi ya kitaifa na kimataifa.

“Tuendelee na utunzaji mazingira na usafi pia ili kuhakikisha Jiji hili linakuwa na muonekano na uhalisia kwa kuwavutia wawekezaji lakini pia tumeelezwa kuwa kupitia mpango unaoendelea wa Jiji ni kuhakikisha wafanyabiashara wadogo (MACHINGA) wanapangwa vizuri katika maeneo ya Mjini kati badala ya kuzagaa holela wakifanya biashara hadi maeneo hatarishi”alisema


Uzinduzi huo umefanyika leo katika eneo la Stendi ya zamani ya Tanganyika iliyopo Kata ya Pamba ambpo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa mwanza Injinia Evarist Ndikilo aliyeambatana na Meya wa Jiji hilo Stanislau Mabula (CCM), Naibu Meya John Minja (CCM), viongozi mbalimbali, wadau na Madiwani wa Kata zote za Jimbo la Nyamagana.


Wadau wa jiji dada na jiji la Mwanza kutoka nchini Sweden jiji la TAMPERE wakitoa utambulisho na pongezi kwa Jiji la Mwanza kwa hatua hii ya kuanzisha wiki ya usafi.


Rais wa chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Dovakimwene John Mcheshi akizungumza na wananchi waliohudhulria kusanyiko hilo la mazingira kuonyesha kuwa nao wako pamoja na uongozi wa mkoa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.


Afisa habari wa jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akiteta jambo na meneja wa SBC.


Injinia Ndikilo amewapongeza wananchi wake kwa kuwa mshindi kwa mara nyingine ya Tuzo ya Usafi na Mazingira ambapo jiji la Mwanza limeshinda kwa mara ya nane mfululizo ambapo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na madiwani,mkurugenzi na wadau mbalimbali wa usafi ili kuhakikisha Jiji hilo ikiwa ni pamoja na kulinda ushindi .


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo, pamoja na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula wakiiongoza meza ya viongozi kwenda kushiriki zoezi la usafi. 
“Wamiliki wa daladala,mabasi na wenye maduka kuhakikisha wanaweka vifaa vya kutunzia usafi na kwa kutumia sheria ndogo za usafi na mazingira ya mwaka 2010 Jiji limejipanga kutumia SHARREFF kutekeleza mpango huu hivyo ni fursa kwa vijana kuunda vikundi na kuvisajili ili kuwashughulikia baadhi yawatu wachache walio na tabia ya uchafuzi wa mazingira” alisisitiza mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza Mabula alisema kwamba Jiji hilo limeandaa mpango wa kuwapanga wamachinga katika maeneo yaliyoruhusiwa kufanya biashara na kuwaondoa wale ambao wako katika maeneo hatarishi ikiwemo kandokando ya barabara kuu na zile za mitaa.



Meya Mabula alisema kwamba baada ya ziara ya madiwani na watendaji katika Nchi ya Rwanda na tafiti mbalimbali Jiji hilo limeamua kuanzisha mpango huo ili kujizatiti zaidi huku pia likiwa limefanikiwa kupata magari mawili kutoka nchini Ujeruman ya kuzoa taka na kufagia barabara huku pia likipatiwa vifaa kupitia mpango wa mradi wa TSCP nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kushiriki kila jumamosi ya kila juma la kwanza la mwezi katika shughuli ya usafi kwenye mitaa na kata zote za Jiji hilo kuanzia saa 1:30 hadi saa 4:00 asubuhi na kuhakikisha wanaochafua mazingira wanakamatwa na kutozwa faini kutokana uchafuzi ili kukomesha vitendo vyote vinavyeneza uchafu.








Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.