ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 5, 2013

"KWA HERI ALBERT MANGWEA"

Msanii Wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond akipita kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Albert Mangwea.
 Baadhi ya Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Wa Kwanza Kabisa ni Mkoloni akifuatiwa na Madee ambaye ni wa Tatu kutoka Mbele wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Albert Mangwea
Baadhi ya Wasanii wa Fani mbalimbali pamoja na ndugu,jamaa na marafiki wakipita pembezoni mwa jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Albert Mangwea na kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Albert Mangwea leo katika viwanja vya leaders

Msanii wa Muziki Keisha (aliyejifunga kiremba Cheupe) akifuatiwa na Noora wakiwa na nyuso za huzuni wakati wakipita kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho leo katika viwanja vya leaders
Wasanii wa fani ya Maigizo hapa Nchini Mzee Magari (aliyeshika Koti jeusi) akifuatiwa na Msanii Natasha Pamoja na Monalisa wakipita kwaajili ya Kutoa Heshima zao Za mwisho kwa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja vya leaders
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wakitoa Heshima za Mwisho

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu  Albert Mangwea likiwa juu ya meza tayari kwa Wakazi wa Jiji la Dar Kuanza kutoa Heshima Zao za Mwisho katika Viwanja Vya Leaders leo.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, utamaduni na Michezo Bi Lilian Bereko akitoa Salamu za Rambirambi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo katika viwanja vya leaders kabla ya Wakazi wa Jiji la Dar hawajaanza kutoa heshima zao za mwisho


Mmoja kati ya watu wa karibu wa Marehemu Albert Mangwea ambaye pia ni msanii wa muziki wa Kizazi kipya kutoka Katika Kundi aliloanzisha Marehemu Albert Mangwea Mez B akitoa historia fupi ya Kundi la Chamber Squade katika viwanja  vya leaders leo

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar pamoja na vitongoji vyake wakiwa wamekaa tayari kwa kusubiria shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Albert Mangwea leo katika viwanja vya leaders
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa na Nyuso Za Huzuni wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja vya Leaders

 Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho pamoja na kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja Vya Leaders

Askari Polisi wakijaribu kuweka mambo sawa ili kusudi wakazi wa Jiji la Dar pamoja na vitongoji vyake kuweza kuingia kwaajili ya kutoa heshima zao kwa utaratibu mzuri na kuepusha vurugu
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiwa wanatoka kutoa heshima zao za Mwisho

PICHA ZOTE NA LUKAZA BLOG

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.