ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 28, 2013

MSIBA WA ALBERT MANGWEA WASABABISHA MWANA FA NA KALA PINA KUSIMAMISHA SHOW ZAO.

Ni vigumu kuamini lakini taarifa ambazo tayari zimethibitishwa kwa masaa sasa ni kwamba Rapper, Freestyler, Albert  Mangwea amefariki dunia leo hii katika majira ya saa 9 alasili.

Inatajwa kuwa jana mara baada ya kulala hakuamka tena na kifo chake kiligundulika leo mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya St Hellen iliyoko South Africa.

Mapema leo marafiki zake walijaribu kila hali kumwamsha lakini wapi hakuamka.

Pia kwa mujibu wa Taarifa zilizotufikia usiku huu inatajwa kuwa mmoja kati ya marafiki zake ambao walikuwa pamoja karibu naye nchini humo msanii wa Bongo flavour aitwaye M2 Tha P naye anatajwa kuwa yuko hoi katika hospitali ya St Hellen akipatiwa matibabu kurejea katika hali ya kawaida.


Sababu za kifo cha Ngwea bado hazijatajwa
 na bado hakijajulikana kitu gani kilichowasibu hata kutokea matukio hayo mfululizo.... Endelea kutembelea blog hii kwa habari zaidi.

FA, PINA WAAHIRISHA SHOW ZAO.
Wakati huo huo msanii Mwana FA ameahirisha show yake iliyokuwa ifanyike ijumaa hii jijini Dar es salaam, sambamba na msanii huyo Kala Pina Naye amesikika jioni ya leo kupitia Amlpifaya akitanabaisha kuahirisha show yake hadi pale itakapo tangazwa tena rasmi.

SIKILIZA KILICHO SEMWA   HAPA:- (BOFYA PLAY
Taarifa zaidi endelea kupitia mtandao huu kila mara.




Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.