ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 22, 2013

MWAUWASA YAZIDAI TAASISI ZA SERIKALI JUMLA YA SHILINGI MILIONI 420: HAYO YABAINIKA KILELE CHA WIKI YA MAJI MWANZA

Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha akisoma hotuba kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maji.
Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza MWAUWASA inadai Taasisi za Serikali ankara za maji jumla ya Tshs Milioni 420.

Hayo yamethibitishwa leo katika hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza iliyosomwa kwa niaba yake na Diwani wa Kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha wiki ya maji yaliyofanyika viwanja vya Ghand Hall jijini Mwanza.

Amesema kuwa Mamlaka hiyo haiwezi kutekeleza wajibu wake wa kusambaza majisafi na kuondoa majitaka kwa wananchi wapatao 700,000 wa jiji la Mwanza wanaofikiwa na mtandao kama limbikizo la deni hilo na Ankara za kila mwezi havitalipwa kwa wakati muafaka.
Mkurugrnzi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Mwanza (MWAUASA) Eng. Anthony Sanga akihutubia umati wa watu waliofurika viwanja vya Ghand hall hii leo.
Mamlaka imefanikiwa kuhudumia shughuli za uondoaji wa majitaka kwa zaidi ya asilimia 15 katika maeneo ya jiji la Mwanza. MWAUWASA inaendelea kuongeza mtandao wa majisafi katika maeneo ambayo hayajafikiwa kwa wastani wa kilomita 15 kila mwaka kulingana na uwezo wa ndani.

Mahitaji ya kuongeza mtandao wa majisafi katika mji wa Mwanza unaokuwa kwa kasi yanakadiriwa kufikia kilomita 300 kwa gharama ya Tshs. Bilioni 5 kwa ajili ya mabomba, viungio na vituo vya kuongeza msukumo wa maji (Booster stations)
Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na maji taka jijini Mwanza MWAUWASA Mama Lopa akitoa changamoto zinazoikabili Malaka hiyo.
Pamoja na changamoto alizozitaja, Mamlaka imetoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga mradi mkubwa wa Majisafi na Majitaka jijini mwanza kuanzia mwaka 2008 hadi 2011.
Wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya maji Kusanyikoni.
European investiment Bank (EIB) pamoja na French Development Agency (AFD) ambao kwa pamoja wamekubali kuchangia jumla ya EURO 90 Milioni kwa ajili ya kufadhili miradi ya maji na usafi wa mazingira katika miji ya Mwanza, Musoma, Bukoba, Magu, Misungwi na Lamadi.
Sehemu ya wafanyakazi wa MWAUWASA.
Wananchi nao wameaswa kusimamia vyema suala la ulinzi na usalama kwa miundombinu ya maji kwenye maeneo yote wanayoishi ili kuiwezesha mamlaka hiyo kuwatumikia vyema.
Wiki ya maji pia inaenda na unywaji maji!!

Burudani na Kadogoli.

Burudani na Bujora wazee wa manyoka.


Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha akipata maelezo toka kwa wafanyakazi wa MWAUWASA kwenye maonyesho mabandani viwanja vya Ghand Hall Mwanza.


Burudani ikiendelea.


Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha akipata maelezo ya Ubora wa Maji toka kwa wafanyakazi wa MWAUWASA kwenye maonyesho mabandani viwanja vya Ghand Hall Mwanza.


Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha akisaini kitabu cha wageni  kwenye maonyesho mabandani viwanja vya Ghand Hall Mwanza huku akishuhudiwa na mmoja wa wafanyakazi wa MWAUWASA.

Kaulimbiu ya Wiki ya Maji mwaka huu ni "Mwaka wa Ushirikiano wa Maji Kimataifa" (International Year of Water Co-operation).
Mwaka huu, Wadau mbalimbali wa maendeleo ya chakula na maji duniani wameamua kushirikiana katika kuhifadhi na kutumia rasilimali maji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.