ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 29, 2013

MCHEZO BAINA YA TOTO NA SIMBA MASHABIKI WAPANIANA

Shabiki wa Toto Africans na uchokozi wake.

Hapa kunamchanganyiko wa mashabiki wa Simba utawajua (nyekundu imehusishwa kwenye jezi zao) na shabiki wa Toto utamwona (jezi nyeusi na rangi fulani hivi...) Majibu jumamosi hii.

Kocha wa Simba akiwanoa wachezaji wake kwa mazoezi ya mwisho mwisho dimbani CCM Kirumba ambapo kesho (jumamosi) timu hizo zitashuka dimbani kumenyana.

Wachezaji wa Simba mazoezini dimba la CCM Kirumba Mwanza.

PAMBANO lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa kanda ya ziwa kati ya timu hasimu Toto Afrika ya jijini Mwanza na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Simba linatarajiwa kupigwa kesho jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba huku mashabiki wa kila timu wakijinasibu kushinda.

Simba SC ambao walipoteza mechi yao iliyopita mjini Bukoba baada ya kuchapwa bao 1-0 na timu ya Kagera Sugar wanaingia katika uwanja wa CCM Kirumba kesho huku wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa na Toto katika mechi ya kwanza katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa bao 1-0.

Kujua kilichojiri Sikiliza Taarifa ifuatayo:-

Hii ni big mechi, nyasi hizi zitawaka moto.

Katibu wa Chama Cha soka mkoa wa Mwanza Nasibu Mabrouk amevitaja viingilio  katika mchezo huo kuwa Jukwaa kuu ni shilingi 10,000/=, na shilingi 3,000/= mzunguko.
Kocha mkuu wa Simba akitoa maelezo kwa Ngasa kwenye mazoezi dimbani CCM Kirumba.

Zoezi la kutawala eneo la 18.
Mmoja kati ya makocha wa Simba Jamhuri Kiwelu akizungumza na waandishi wa habari.



"Tuacheni tutete wawili tu!"

Mashabiki wa Simba walimzonga kocha msaidizi Julio wakitaka kujua nini hatma ya timu yao mara baada ya kuonekana kusuasua katika ligi ikiwa nipamoja na kichapo mkoani Kagera. Hata hivyo julio alionekana kujibu kwa ufundi maswali yao. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.