ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 22, 2013

CHINUA ACHEBE AFARIKI DUNIA



Mwandishi Maarufu wa vitabu duniani Chinua Achebe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Msemaji wa jimbo la Anambra nchini Nigeria Mike Uda ameiambia BBC kuwa wanaomboleza kifo cha wanayemwita mtoto wa taifa la Nigeria na Afrika kwa ujumla.
Chinua Achebe alizaliwa mwaka 1930, miaka 30 kabla ya Nigeria kupata uhuru.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake, imemwelezea Chinua Achebe kuwa mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu vya fasihi katika kipindi chake, ambaye busara yake ilikuwa kichocheo cha kumwiga kwa wale wote waliomfahamu.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo ya akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo. Alipata umaarufu mkubwa kutokana na utunzi wa kitabu chake cha kwanza cha fasihi kitwaacho 'Things Fall Apart', ambacho alikitunga mwaka 1958 kikizungumzia athari za ukoloni barani Afrika.
Kitabu hiki kiliuza zaidi ya nakala milioni 10. Things Fall Apart kimetafsiriwa katika zaidi ya lugha 50 na kuelekeza mtazamo wake katika jamii ya Wa-Igbo na mgongano wa kimaadili kati ya nchi za mgaharibi na kijadi.
Alipata ngazi ya uprofesa kutoka chuo kikuu cha Boston nchini Marekani mwaka 1970 ambapo katika siku za hivi karibuni alikuwa akikosoa baadhi ya mienendo mibaya ya serikali ya Nigeria.
Amekuwa akiishi nchini Marekani tangu mwaka 1990 kufuatia kujeruhiwa katika ajali ya gari.
Ameandika kazi za kitaaluma zaidi ya 20, baadhi zikikosoa vikali wanasiasa na uongozi mbaya nchini Nigeria.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema Profesa Achebe ataishi daima katika mioyo na akili za watu wa kizazi kiliochopo na vijavyo.
CHANZO: BBC SWA.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Appreciate this post. Let me try it out.

    Also visit my weblog how safe is quantrim

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.