ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 9, 2013

TOTO YAAMBULIA SARE NYUMBANI.

Toto Africans Football Club.
Jahazi la timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza limezidi kutoboka na kuwapa presha wakazi wa jiji la miamba kuhofia kukosa timu ya uwakilishi ligi kuu Tanzania bara kwa msimu ujao, mara baada ya matokea ya sare ya bila kufungana na timu ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa leo ndani ya dimba la CCM Kirumba Mwanza.

Licha ya Coastal kuichachafya ngome ya Toto kwenye kipindi cha kwanza lakini hadi dakika 45 za kipindi hicho zinamalizika ubao ulisomeka 0-0.

Dakika 20 za mwisho kwa kipindi cha pili Toto walijaribu kubadilisha mchezo na kuwapa matumaini watizamaji wake wachache waliohudhuria mchezo huo kuwapa sapoti kwa kuumiliki mpira  na kulisakama lango la Coastal Union, lakini mashambulizi yao hayakuwa na manufaa yoyote kwa timu hiyo ambayo tangu kuanza kwa ungwe hii ya lala salama, tofauti na mchezo wa leo haikufanikiwa hata kuambulia pointi moja.

Ni ndani ya dakika hizo timu hiyo ilipaswa kujilaumu kwa kushindwa kuondoka kifua mbele.
Hatimaye hadi mwisho wa mchezo timu zote zilitoka uwanjani zikiwa na sare ya bila kufungana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.