ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 21, 2013

WAZIRI KOMBANI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI JIJINI MWANZA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Ompeshi Kombani akizungumza mapema leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania katika ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani amewapongeza wakaguzi hao kwa kuboresha usimamizi wa mapato na matumizi ya mali ya Umma, kwani matunda ya kazi za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yameijengea nchi ya Tanzania sifa nzuri siyo tu kwa raia wa Tanzania, bali mbele ya wadau wote wanaotakia mema nchi hii.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo kwa upande wake amelia na baadhi ya watendaji waliotajwa katika Taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kutafuna fedha za Umma huku wakiendelea na kazi bila hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao, ameitaka serikali kulitizama hilo kwa jicho la tatu na kuchukua hatua za haraka kusafisha waliobakizwa. 

Mkutano huu unatajwa kuwa ni wa pili kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013, Madhumuni yake ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ndugu ludovick S.L Utouh akimtambulisha Mkurugenzi wa jiji la mwanza Bw. Wilson Kabwe, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Tanzania katika ukumbi wa Benki Kuu Mwanza.

Wakaguzi hao walipata fursa ya kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi.

Meza  kuu nayo ilihusika na wimbo huo wa mshikamano.

Katika kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kupunguza suala la Ofisi ya Wakaguzi kutegemea Ofisi za Wakaguliwa jitihada zimeanza kufanyika na mpaka sasa Ofisi imeweza kujenga Ofisi zake katika mikoa ya manyara, Shinyanga, Singida,  Mbeya, Lindi, Kilimanjaro na Morogoro aidha Ofisi ilinunua jengo na kulifanyia ukarabati mkoani Arusha.

Mshikamano na Wakaguzi waliohudhuria mkutano wao wa Mwaka katika ukumbi wa Benki Kuu Mwanza. 

Moja kati ya Changamoto ambazo Afisi ya Mkaguzi wa fedha za Serikali bado inaendelea kukumbana nazo ni Idadi ndogo ya rasilimali watu ukilinganisha na ongezeko la ofisi kupitia Mikoa mipya, Halmashauri za wilaya mpya na ukaguzi wa Umoja wa Mataifa.

Picha namba moja.

Picha namba mbili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.