ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 18, 2013

UFUNGUZI WA VISIMA 30 KATIKA MAENEO YA WILAYA 6 KAME TANZANIA VILIVYOCHIMBWA KWA MSAADA WA SERIKALI YA MISRI WAFANYIKA WILAYANI MASWA.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Jumanne Maghembe (katikati) akishirikiana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed (kulia) kukata utepe kuashiria ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri uliofanyika jana katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu. Kushoto kabisa ni Mhe. Pascal Mabiti ambaye ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Tanzania Jumanne Maghembe naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Mbunge wa jimbo la Busega mkoani Simiyu  Titus Kamani naye akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama.

Mama Maria akiondoka kwenye eneo la bomba kuu la kutekea maji mara baada ya kutwishwa ndoo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed huku wananchi wengine wakipiga makofi kuashiria kufurahia tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu. .

Jiwe la Msingi.

Ni burudani ya ngoma ya kabila la wasukuma na wala si mchezo wa vita.

Meza kuu ikifurahia yanayojiri ya kiburudani katika kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri .

 Kwa upande wake waziri wa Maji na Umwagiliaji Nchini Prof. Jumanne Magembe amesema kuwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inapunguza kama si kuondoa kabisa tatizo la uhaba wa maji nchini Tanzania.
Bofya Play usikilize ..

Takwimu za upatikanaji wa maji katika Wilaya zilizochaguliwa kwenye mradi huo hadi mwezi Disemba 2011 katika wilaya zilizomo kwenye miradi zinaonyesha kuwa na hali ni ya mvua zisizoridhisha, hivyo kipaumbele katika mradi huu ni kusaidia kwanza maeneo yaliyo upande wa mvua kidogo ambapo matarajio ya serikali kwa miradi yote ikikamilika hali ya upatikanaji wa maji katika vijiji vyote itakuwa bora, suala ambalo linawezekana.

Nae Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed amesema kuwa serikali yake inajivunia msaada iliyoutoa wa kiasi cha fedha Dola milioni moja za Kimarekani kusaidia kukamilika kwa miradi ya maji nchini Tanzania kwani Misri inaamini kuwa hiyo ni moja kati ya njia ya kudumisha na kuendeleza ushirikiano uliopo.  


Msaada huo wa Misri si suala geni hapa nchini kwani tangu enzi za hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere, Tanzania na Misri zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja za siasa, maji, kilimo cha umwagiliaji, na Tanzania imekuwa ikipokea madaktari wakujitolea ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye hospitali za mikoa na kila mwaka Tanzania imekuwa ikipeleka wataalamu wake nchini Misri kupata mafunzo kujinoa katika taaluma hiyo.

Wananchi wa kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu wakisikiliza hotuba za viongozi kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri 
Pamoja na mradi huu, huduma ya maji imeendelea kuboreshwa kote nchini kupitia Program ya maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo ilianza kutekelezwa tangu mwaka 2006, kwa kushirikisha juhudi za wananchi wenyewe na washirika wengine wa maendeleo. Miradi inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za programu wilayani Maswa ni ; Miradi ya maji ya bomba ya vijiji vya Sayusayu, malampaka na Mwasayi; Miradi mipya inayokaribia kuanza kutekelezwa ni ya vijiji vya Njiapanda na Jija.

Lengo la Programu ya Maji ni kuwa kufikia mwaka 2015,huduma ya maji vijijini iwe wastani wa asilimia 65.
Wananchi wa kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu wakisikiliza hotuba za viongozi kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri 

Wito umetolewa kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo yote ya miradi nchini kuwa walinzi wa miundombinu ya maji. kutokomeza tatizo la miundombinu ya maji na vifaa vya maji kuhujumiwa na watu wabaya ambao huing'oa na kuuza kama chuma chakavu hivyo kila mwananchi awe mlinzi wa miundombinu hiyo kwa faida ya taifa na kwa kuzingatia maslahi ya walio wengi (kuwaepusha mama zetu na adha ya kusafiri umbali mrefu kusaka maji salama).

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.