ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 4, 2013

AJIRUSHA GHOROFANI BUGANDO NA KUFA.

Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Bugando lililopo katika vilima vya Bugando jijini Mwanza kama linavyoonekana hii leo tarehe 04/januari/2013, lina urefu wa ghorofa tisa.
Mkazi mmoja wa mtaa wa Kigongo Ferry katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Bi Tekila Daudi mwenye umri wa miaka 28 amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya nne katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) jijini hapa.

Kwa mujibu wa Afisa Muuguzi msaidizi wa Hospital hiyo Bi. Adera Buberwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Decemba 30, majira ya saa sita mchana.

Bi Buberwa alisema kuwa marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo tangu disemba 19, mwaka 2012, kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa uvimbe tumboni pamoja na tatizo la moyo.

"Marehemu alikuwa amelazwa wodi namba 4 ambapo tayari alikuwa ameshapatiwa matibabu ya upasuaji ya uvimbe tumboni" aliongeza Afisa huyo muuguzi.

Bi. Buberwa sanjari na hayo alisema kuwa marehemu alifikishwa katika hospitali hiyo baada ya kupatiwa rufaa kutoka katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.