ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 3, 2013

AIRTEL YAZAWADIA WASHINDI WA MWEZI WA "AMKA MILLIONEA" PROMOSHENI SHILLINGI MILLIONI 30

Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya mwenzi  wa washindi wa Amka Millionea, Ambapo moja kati ya washindi ni  bw Rickson Richard kutoka Arusha aliyejishindia shillingi million 15. pichani  Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu


Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu wakitafuta washindi wa mwenzi wa promosheni ya Amka Millionea ambapo Ambapo moja kati ya washindi ni bw Rickson Richard kutoka Arusha ambaye amejishinid kitita cha shillingi million 15.  wakishuhudia ni waandishi wa habari , kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde

Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde akiongea na Mshindi wa Amka Millionea bw Rickson Richard (19) kutoka Arusha  mara baada ya kuibuka kuw mshindi wa shillingi million 15 wa promosheni ya Amka millionea, Katikati ni Meneja Bidhaa Francis Ndikumwami akifatiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Bahati nasibu ya taifa bw Sadiki Elimsu

TAARIFA ZAIDI.
Airtel yawazawadia washindi wa mwenzi wa “Amka Millionea” promosheni shilingi million 30
·         Washindi wawili wapatikan, Kila mmoja aondoka na kitita cha shilling million 15
2 January 2013  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo iwatangaza washindi  wa mwenzi wa promosheni “Amka Millionea” wa pesa taslimu  million 30 mara baada ya kuibuka washindi kupitia droo iliyofanyika leo asubuhi ambapo kila moja ameibuka na  kitita cha shilingi milioni 15 pesa taslimu.

Akitangaza washindi hao mara baada ya droo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania  kushiriki na Kushinda fedha taslimu kwa kupiti promosheni yetu hii kabambe ya “Amka Millionea” iliyozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December, mpaka sasa wateja zaidi ya 300 wamejishindia zawadi za pesa taslimu zenye thamani  zaidi ya shilingi million 120.  Promosheni ya Amka millionea inawazawadia wateja wa Airtel  Kila siku , kila wiki na leo tunashuhudia wateja wawili wa mwisho wa mwenzi wakiibuka kuwa washindi wa shilingi million kumi na tano kila mmoja.

Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Matinde.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.