ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 30, 2012

SIKU MOJA KABLA YA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA MKUU WA MKOA WA MWANZA ATEMBELEA MAONYESHO: KESHO WAZIRI MKUU MH. PINDA KUFUNGA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza akiwa amebeba kombe la Ushindi wa Usafi kwa majiji lililotunukiwa kwa mkoa wake hivi karibuni kwa mwaka wa saba mfululizo, mkuu huyo akiwa ameambatana na Katibu wa CCM Mkoa bi. Joyce Masunga na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Polisaga amefanya ukaguzi leo kwenye mabanda ya maonyesho ya maadhimisho hayo yaliyopo ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kesho  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Pinda atafunga rasmi na kutoa zawadi kwa washindi. 

Injinia Ndikilo akipata maelezo ya viatu vilivyotengenezwa na ngozi asilia toka kwa moja ya wadau wa kutengeneza bidhaa zinazotumia ngozi.

Ni ramani za majengo matatu ya kisasa yatakayo jengwa ndani ya jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na Soko kuu, Jengo la kliniki kwa akinamama eneo la Utemini na Jengo la Idara ya Afya.

Wananchi wakipata maelezo  ya bidhaa za mikono.

Mdau akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lake.... "ulishawahi kula nsansa wewe?"

Nafaka zaweza kutumika kwa mapishi mengi .... "Ushawahi kula chapati za viazi wewe?"

Nafaka maonyeshoni.

Rozela inatumika kutengeneza wine (kama unavyoona pichani) wine iliyofull kiwango yenye manufaa kwa mwili kama kusafisha figo, kuongeza damu, kuburudisha akili na kuimarisha nguvu ya msisimko kwa mwili.

Mwananchi akijipatia yake moja kwaajili ya kujinafasi.

Afisa muuguzi bingwa wa magonjwa ya akili na kutoa dawa za usingizi toka Hospitali ya Wilaya ya Misungi, Bon Venture P. Michael akitoa maelezo kwa mwananchi.

Afisa nyuki mwandamizi toka wilaya ya Misungwi Thomas E. Mshana, akionyesha nta na mazalia ya nyuki yanayozalisha asali.

Benito Bernard Makombe kutoka Halmashauri ya jiji la Mwanza akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kushiriki zoezi la SENSA ya watu linalotaraji kufanyika mwezi agosti mwaka huu.

Eneo la tukio kwa chati na wana usalama.

Afisa uhusiano wa jiji la Mwanza Joseph Mlinzi akionyesha moja ya vikombe na vyeti ambavyo Halmashauri ya jiji imejinyakulia katika mashindano ya usafi na mazingira kwa mara ya saba mfululizo tangu kuanzishwa kwake, kesho Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo K. Pinda anatarajiwa kuhitimisha maonyesho hayo wananchi mnakaribishwa.
Kiingilio ni Bureeeeeee....

Friday, June 29, 2012

MTUKUTU BALOTELLI ALIPOIPELEKA ITALY FAINALI EURO


Mario Balotelli jana alifunga magoli mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza Ujerumani kwa kuifunga magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.

Akihojiwa mara baada ya mchezo huo.


Kwa mujibu wa mchambuzi wa soka nchini Tanzania Shaffi Dauda anasema kuwa "Kwa kuangalia rekodi yao nzuri kwenye EURO 2012 watu wengi waliamini kuwa Ujerumani wangekuwa na kazi rahisi ya kuwaondoa Waitaliano kwenye mchezo huo wa nusu fainali"
"Mario Baloteli amewafanya watu wengi jana kukosea utabiri wao na sasa Wajerumani na mashabiki wao wanajiuliza nini hasa kilichotokea" aliongeza Shaffi.

SAFARI YA KUKUZA VIPAJI VYA SOKA NCHINI INAANZIA MWANZA KUELEKEA NCHINI UJERUMANI



Ni mahojiano kati yetu na mkurugenzi wa kituo cha watoto wa mitaani KULEANA cha jijini Mwanza kilichojikita katika kuelimisha watoto malezi bora na suala la ukuzaji wa vipaji mbalimbali vya michezo nchini Tanzania hususani soka. Ndani ya filamu hii ya muda wa dakika 5 Mutani anatueleza mikakati na mipango kuboresha soka la nchi sanjari na mapokeo ya soka la vijana wake wa mitaani kwenye michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa mitaani.


Timu ya Vijana wenye umri wa miaka chini ya 20 ya Tanzania Soccer Academy (TSC) yenye maskani yake jijini Mwanza iko kambini kwa sasa ikifanya mazoezi makali kujifua kwaajili ya maandalizi yake ya mwisho kuelekea nchini Ujerumani ambako itashiriki michuano kadhaa ya soka la vijana wadogo.

Vijana wakijifua kikamilifu kwa ajili ya safari.

Road to German; Frank Sekule (kulia) anaye chezea timu ya Taifa U20 anatokea kituo hiki hivyo amekuja kujumuika na wenzie kwa safari hiyo.

The Trip to German ...Seleman na Timotheo.. vijana wadogo wa squad la TSC U20.

 Majuzi katika mechi za majaribio ikicheza soka la kuvutia timu hiyo ilikichabanga kikosi kipya cha Toto Africans mabao 3-0 dimbani CCM kirumba Mwanza. Timu hiyo rasmi itaondoka nchini mnamo july 14 mwaka huu.
Kila la kheri wana wa home kila lakheri soka la Tanzania.
By G. Sengo.

WALE WA GOTHIP'' DAWA YA NGUVU ZA KIUME HII HAPA

Mchuuzi wa tende katika kituo cha mabasi mkoani Dodoma, wengi hatujuwi kuwa  zao hili lina sifa nyinyi kwa matumizi ya mwanadamu...!!  
DAWA YA NGUVU ZA KIUME HII HAPA
Wakuu.
Tumekuwa tunajadili mambo mengi ya msingi kwa taifa letu na mara kadhaa tumekuwa tunajadili kwa umuhimu wa kipekee madhara ya ukosefu wa nguvu za kiume na sababu zinazopelekea tatizo hilo.

Mwanaume hasifiwi kupendeza kwa mavazi ya dhahabu, au suti za mikogo, lakini pia furaha ya mpenzi wake haiishii kwenye ununuzi wa vipodozi,  nguo za gharama au usafiri wenye viti vya manyoya.
Kwa heshima na taadhima naomba tupeane maarifa ya tiba mbadala ya kuongeza nguvu za kiume kwa juice ya tende.

 Mahitaji.
1. Robo kilo ya tende
2. Maziwa nusu lita
3. Blenda ya kusagia
4. Bakuli
5. Birauli

  Hatua
i. Ondoa kokwa za tende na tia kwenye blenda
ii. Changanya tende na maziwa.
iii. Blendi maziwa na tende kwa muda wa dakika 5 mpaka upate juice laini.
 Matumizi.
Kunywa birauli 1 hadi mbili mara 3 kwa siku kwa kiasi cha siku utakazo weza.

Sharti.
Usichanganye wala kuongeza sukari kwenye juice hiyo.

  Faida.
 i. Hutibu chango la kiume na kike (tumbo kunguruma na kujaa gesi)
 ii. Hutibu tatizo la choo ikiwa ni pamoja na wale wenye kutoa choo mithili ya mnyama mbuzi.
iii. Inaweza kutumiwa na mtu yoyote wa jinsia yoyote.

Wakatabahu.

MOUNT KILIMANJARO MARATHON NOTES – 2

Deidre Lorenz akimkabidhi picha ya  Ground Zero (New York) Rais wa Mt. Kili Marathon 1991 Onesmo Ngowi baada ya  kukimbia mbio hizo

DEIDRE LORENZ KAINGIA KWENYE MAPENZI NA TANZANIA

Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.

Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana Tanzania.

“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote” aliendelea kusema Deidre Lorenz.

Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana.

Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental Races.

Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.

Kwa kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.

“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.

Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.

Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.

Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.


Imetumwa na:
Grace Soka
Afisa Uhusiano

MT. KILIMANJARO MARATHON 1991

RAY AZINDUA FILAMU YA SOBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS

 Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.

 Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.

Msanii wa Filamu Nchini Visent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps.Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada ya lei kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre vilivyotolewa na Kampuni ya Steps wakati wa Uzinduzi wa filamu yao Mpya ya Sobing Sound.

MSANII wa filamu nchini Visent Kigos 'Ray' amezindua filam yake mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.

Filam hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua Ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filam hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5 kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam

Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha uku wengine wakiendelea kutahabika kitendo ambacho si kizuri.

Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atakuwa kila filamu anayotoa atakikisha japo kidogo kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima kwana awajapenda.


Alisema msaada uliotolewa kwa watoto yatima hautaishia kwao bali ataendelea kutoa kile atakachokipata kupitia filamu hiyo kuwasaidia na wale wasiojiweza amesema kampuni ya Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kutushawishi tuwe tunawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingila magumu.

Nae mmoja wa wakilishi wa Kampuni ya Steps Kambarage amesema swala la watoto yatima niletu sote na wala alichagui kwa kuwa tunawajibu na angalau kidogo tunachokipata kupitia filamu zetu tunarudisha kwa kutoa shukurani zetu.

Thursday, June 28, 2012

Airtel YACHANGIA DAMU KUOKOA MAISHA YA WATZ


 Bi Coletta Ndumbalo akijitolea damu katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na kuhusisha wafanyakazi wa Airtel kuchangia damu kwa mfuko wa taifa wa kuhifadhi damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu. Zoezi hilo la kuchangia damu lilifanyika jana siku nzima katika makao makuu ya Airtel Moroco.

 Meneja huduma za jamii bi Hawa Bayumi akijitolea damu katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na kuhusisha wafanyakazi wa Airtel kuchangia damu kwa mfuko wa taifa wa kuhifadhi damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu. Zoezi hilo la kuchangia damu lilifanyika
jana siku nzima katika makao makuu Moroco. akitoa huduma ni bi Selina Sahani kutoka kitengo cha damu salama cha taifa

Bi Helena Mteti Meneja Muhakiki wa Kodi Airtel akipata ushauri kutoka kwa muugizi Bi Elizabeth Mgaya kutoka kitengo cha damu salama cha taifa kabla ya kuanza zoezi la kuchangi damu lililoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel likishirikisha wafanyakazi wake Zoezi hilo la kuchangia damu lilifanyika jana siku nzima katika makao makuu
Moroco. 

Mfanyakazi wa Airtel Bwana Greyson Mapunda akijitolea damu katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na kuhusisha wafanyakazi wa Airtel kuchangia damu kwa mfuko wa taifa wa kuhifadhi damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu. Zoezi hilo la kuchangia damu lilifanyika jana siku nzima katika makao makuu Moroco. akitoa huduma ni Bwana James Semba kutoka Kitengo cha damu salama cha taifa

Press Release
Airtel yachangia damu kuokoa maisha ya watanzania Alhamisi, Juni 28 2012, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeandaa zoezi la kuchangia damu litakalohusisha wafanyakazi wake kuchangia damu kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu, hii ni moja kati ya shughuli za Airtel katika kusaidia jamii

Akiongea wakati wa zoezi la kutoa damu lililofanyika katika makao makuu ya Airtel Mkurugenzi Rasilimali watu Perece Kirigiti alisema” Airtel inandeleza dhamira yake ya kusaidia na kuchangia katika shughuli za kijamii na leo tunashirikisha wafanyakazi wetu kuchangia damu katika kukiwezesha kitengo cha damu salama cha taifa kuwa na hifadhi ya damu ya kutosha kukidhi mahitaji ya wagonjwa na kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa.
Tutakuwa na zoezi hili siku nzima ya Alhamisi hapa Ofisini makao makuu Dar es salaam ambapo madaktari kutoka kitengo cha taifa cha kutoa damu wataendesha zoezi la kutoa damu kwa wafanyakazi na wageni watakaojitolea kuchangia. Wafanyakazi wetu wanayofuraha kuona wanaokoa maisha ya watanzania nchini na kwa jinsi hiyo tunatimiza majukumu yetu katika kusaidia jamii inayotunzunguka.

Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamiii bi Hawa Bayumi akichangia kuhusu jitihada hizi alisema” hii ni moja kati ya jitihada zetu za kuwawezesha wafanyakazi wetu na wadau mbalimbali kuona jukumu lao katika kusaidia jamii, na kwa mwaka huu wito ni changia damu ili kuokoa maisha”
Zoezi zima la utoaji damu litahusisha kujaza fomu, mahojiano na uchunguzi wa afya utakaofanywa kwa kufata kanuni za tiba, kisha kufatiwa na utoaji damu utakaochukua takribani dakika 10 ambapo
mililita 450 za damu zinategeme kuokoa maisha ya mtu mmoja Tanzania inahitaji kiasi cha damu cha unit 350,000 kwa mwaka kwa ajili ya huduma za dharura za tiba ambapo kwa sasa kitengo cha damu salama cha taifa kinakusanya unit 115,000- 120,000 kwa mwaka hivyo kuwa na mapungufu ya kiasi cha unit 235,000.

Kitengo cha taifa cha kutoa damukitengo cha damu salama cha taifa wa damu kwa mwaka huu wa 2012 na kufanya juhudi za kukusanya unit 180,000, hivyo inatoa wito kwa watanzania wenye afya walio na umri kati ya 18 na 65 na uzito wa 50kgs kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu.

TAMASHA LA Serengeti fiesta 2012 LAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR.

Mmoja wa Waratibu wa maandalizi ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 (pili kulia) Sebastian Maganga akifafanua baadhi mambo mbele ya wageni waalikwa wakiwamo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha hilo uliofanyika kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinodoni jijini Dar leo,tamasha hilo linatarajia kutimua vumbi zake hivi karibuni katika mikoa mbalimbali,ambapo katika tamasha hilo mdhamini mkuu ni kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake Serengeti Premium Lager,Kampuni ya mafuta ya Gapco pamoja na Push Mobile.Kauli mbiu ya tamasha hilo ni "MUONEKANO MPYA-BURUDANI ILELE-BAAAS"! 
 Sehemu ya zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ikiwemo Magari aina ya Toyota Vitz kila moja yenye thamani ya shilingi milioni nane,Piki piki a.k.a Boda Boda 14 kila moja ikiwa na thamani ya shilingi milioni moja na nus na zawadi nyingine zikiwemo simu aina ya blackberry,Nokia.

Baadhi ya Wadau mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya lidaz Club,jijini dar.

Mmoja wa waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa umakini na kuweka misisitizo kwa Wanahabari waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha hilo. 

 Sebastian Maganga kutoka Clouds Media Group akiwatambulisha Wadhamini wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Kutoka kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya mafuta ya Gapco,Ben Temu,Meneja wa kinywaji cha Serengeti kutoka SBL,Allan Chonjo pamoja na muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile,Bw.Rodney

 Meneja wa bia ya Serengeti kutoka kampuni ya SBL,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2012,Allan Chonjo akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa wakiwemo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,uliofanyika leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,jijin Dar.

 Bw.Rodney ambaye ni muwakilishi wa kampuni ya Push Mobile akionesha moja ya namba zitakazotumika kutoa taarifa mbalimbali za tamasha hilo litakaloanza kutimua vumbi zake kuanzia hapo kesho katika mikoa ya Arusha na Mbeya na baadaye mikoa mingine.

 Pichani shoto ni Meneja mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti,Bw.Iman Lwinga akiwa sambamba na baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
 Wageni waalikwa wakiwemo wasanii kadhaa bia walifika kushudia tukio hilo kubwa la kihistoria katiak tasnia ya burudani hapa nchini.

Wakifuatilia kwa umakini zaidi.

 Kwa mshangao mkubwa wakishuhudia uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Lidaz Club.

 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo,akiwemo Shaffih Dauda mzee wa sports bar.
 Meneja wa vinywaji vikali wa SBL,Bw.Emillian Rwejuna akizungumza na Meneja wea kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

 Mtangazaji wa Clouds FM,Millard Ayo akifanya mahojiano mafupi na msanii wa muziki wa kizazi kipya,Mwasiti kuhusiana na tamasha la fiesta kwa ujmla.

Wadadazi nao walikuwepo kunogesha uzinduzi huo wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

PAMBANO JINGINE LA UBINGWA WA TAIFA

Kaike Promotion imeandaa pambano lingine la ubingwa wa taifa kati BAINA MAZOLA na JUMA FUNDI (ambae alishawahi gombea mkanda wa dunia nchini Philipines) litakalopigwa jumapili ya tarehe 15 mwezi wa saba,pambano hili ni mtiririko wa mapambano ya ubingwa wa ngumi na kuendeleza vipaji vya mabondia chipukizi na wale tunaowategemea kwenda kuchukua mikanda mikubwa ya dunia.
 
Inafahamika wazi kwa taifa letu, mchezo wa ngumi ni miongoni mwa mchezo unaopeperusha vema bendera ya Tanzania lakini ni mchezo usio na wafadhili wala wadhamini unajiendesha wenyewe kishidashida bila ya utaalam mzuri wa uongozi utaalam upo katika uchezaji na mchezo unaohitaji msaada wa hali ya juu sana kuinuliwa.
 
Wadhamini wangejitokeza kudhamini ngumi wangelisaidia sana taifa letu. Mchezo wa tarehe 15july utasimamiwa na TPBO na mapambano yamepangwa na Ibrahim Kamwe chini ya uratibu wa Kaike Siraju yataongozwa na mapambano ya utangulizi kati bondia anaechipukia kwa kasi Issa Omar (toka bigright boxing Mwananyamala) na Ramadhan Kumbele bingwa wa taifa toka kambi ya Matumla -Keko.

Anthony Mathias(aliyekuwa bingwa wa PABA) ataminyana na chipukizi Mwaite Juma (toka bigright boxing)

Mapambano mengine ni kama ifuatavyo hapo chini na katika picha ni Issa Omar akinolewa na mwalimu wake Ibrahim bigright
Bantam weight - Juma Fundi v/s Baina mazola - 10 round ,TPBO title
Fly weight- Ramadhan Kumbele v/s Issa Omar - 6 round
Bantam weight - Anthony Mathias v/s Mwaite Juma - 6 round
Super feather weight - Doi Miyeyusho v/s Shaban Mtengela 6 round
light weight - Bakari Mohamed v/s Sadiki Momba - 6 round

DATE; 15 / 07 / 2012
VENUE; DDC Kariakoo, Dar Es Salaam, TANZANIA
PROMOTER; Kaike Promotion
MATCHMAKER; Ibrahim kamwe
TICKETS; +255 715 707777