ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 16, 2012

MPC WACHAGUA SURA MPYA 2012

Akitangaza matokeo  Mwenyekiti wa uchaguzi huo bw. Robert Mkosamali (aliyesimama pichani) nafasi ya za Wajumbe watano wa kamati ya Utendaji zimekwenda kwa Rose Jackob na Grace Chilongola waliopita bila kupigiwa kura, wengine ni George Ramadhani, Atley Kuni na Kelvin Jilala.


Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa zoezi la uhesabu kura.

Nafasi ya Mweka hazina imekwenda kwa Fred Katulanda aliyepata kura 28 aliyewaangusha Paulina David aliyepata kura 25 na Clara Matimo aliyeambulia kura 1.

Makamu Katibu mkuu imetwaliwa na bi Sheila Sezy aliyepita kwa kura za NDIYO 39 na HAPANA 14.

Nafasi ya Katibu Mkuu imekwenda kwa Jimmy Luhende aliyepata kura 27 akiwashinda Felista Kulijila kura 22 na Nashon Kenedy aliyeambulia kura 7.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeenda kwa Flora Magabe aliyepata 29 dhidi ya wapinzani wake Rahabu Fred kwa kupata kura 27, ambaye hata hivyo hakuwepo uchaguzini kwenye mkutano huo  kutokana na kuwa na udhuru.


Mwisho nafasi nyeti ya Uwenyekiti ilinyakuliwa kwa kishindo naye Deus Bugaiwa aliyetikisa kwa ushindi wa kishindo kwa kuzoa kura 41  dhidi ya Osoro Nyawangah aliyepata kura 15 za wanachama walioshiriki uchaguzi huo. 


 Wadau wa habari katika moja ya meza za majukumu mkutanoni humo.

 Wanachama mkutanoni.

 Hapa wanachama walikuwa wakijinadi kupata ridhaa ya wadau kuwania nafasi tano za Ujumbe.
  

Wanachama wakifuatilia mkutano wa mwaka 2012.

WANAVIKUNDI WAMA WAKUNNWA NA HUDUMA ZA NHIF

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Eugen Mikongoti akizungumza na wanavikundi zaidi ya 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati wa akifungua mafunzo kwa wanavikundi hao juu ya utaratibu wa huduma zitolewazoto na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,katika ukumbi wa Mikutano wa Boma,Ilala jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Tabu Lokoko na katikati ni Ofisa anayeshughulikia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Rehani Athuman.


 Ofisa anayeshughulikia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani ambaye ndie mtoa mada mkuu katika mafunzo hayo,akifafanua jambo kwa wanavikundi zaidi ya 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati wa semina ya mafunzo kwa wanavikundi hao juu ya utaratibu wa huduma zitolewazoto na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, katika ukumbi wa Mikutano wa Boma,Ilala jijini Dar es Salaam leo.

 

Baadhi ya wanavikundi zaidi ya 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakifuatilia kwa makini mafunzo juu ya utaratibu wa huduma zitolewazoto na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, katika ukumbi wa Mikutano wa Boma, Ilala jijini Dar es Salaam leo.

===============================

Na Grace Michael
JUMLA ya wanavikundi 400 walio chini ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wameridhishwa na utaratibu wa huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hatua iliyowafanya kuahidi kujiunga mara moja ili wawe na uhakika wa kupata matibabu.
Hatua hiyo imefikiwa wakati wa mafunzo yaliyotolewa na NHIF kwa wanavikundi hao Dar es Salaam leo ambapo walielezwa faida wanazoweza kupata kupitia utaratibu wa kujiunga na Mfuko huo.

Kutokana na hatua hiyo, NHIF kwa kushirikiana na WAMA wataandaa utaratibu utakaowawezesha wanavikundi hao kuanza utaratibu huo mara moja ambao utawanufaisha na kuwapunguzia mzigo wa gharama za matibabu.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika sekta ya afya, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeendelea kuwa na dhamira ya kuwapatia watanzania wote utaratibu unaoeleweka wa huduma za afya na kuhakikisha wanachama wake wanapata huduma za matibabu kwa heshima inayostahili.

“Utaratibu wa kupata tiba kwa kadi unao manufaa makubwa kwenu, kwani gharama za matibabu kwa sasa ni kubwa mno na kama mnavyoelewa ugonjwa haupigi hodi hivyo kwa kuwa na kadi itasaidia kupata matibabu wakati wowote hata kama hamtakuwa na fedha kwa muda huo,” alisema Mikongoti.
Mafunzo ya wanavikundi hao ni mwendelezo wa mafunzo yaliyotolewa na Mfuko kwa viongozi wa vikundi ambayo yalikuwa na lengo la kuwapa elimu juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

“Tuko hapa ili tuzungumze fursa na vikwazo vinavyoweza kuukabili mpango wa Bima ya Afya kwa Wajasiriamali,.. dhana hii bado ni ngeni kwa wengi lakini inaweza kuwa na manufaa kwa kuielewa na kuifanyia kazi na sisi kama Mfuko tumejipanga kuhakikisha huduma hii mnaipata kama inavyotakiwa” alisema Mikongoti.

Katika mkutano huo Ofisa anayeshughulikia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Rehani Athumani ambaye aliwasilisha mada iliyohusu huduma za matibabu za uchangiaji kupitia NHIF na CHF ikiwa ni pamoja na manufaa yake.

Rehani aliwaeleza wanavikundi hao kuwa endapo watajiunga na Mfuko huo watapata huduma za matibabu katika hospitali zote za Serikali na za binafsi ambazo zimesajiliwa na Mfuko huo.
Alisema kuwa katika kuhakikisha wanachama wa Bima ya Afya hawakumbani na tatizo la ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma, Mfuko pia umesajili maduka ya dawa ambayo mwanachama anaweza kupata huduma ya dawa kama atakosa huduma hiyo katika kituo cha matibabu alichokwenda.

Kutokana na hali hiyo, aliwaomba kujiunga na Bima ya Afya ili wanufaike na mtandao mkubwa wa huduma za matibabu.

Hata hivyo Rehani hakusita kuwakumbusha wajibu wa kuwa walinzi wa huduma za afya hasa pale wanapoona kasoro za kiutendaji katika vituo vya huduma za matibabu.

Kwa upande wa wanavikundi hao, waliweka wazi msimamo wao kuwa wako tayari kujiunga na utaratibu wa Bima ya Afya ili waweze kunufaika na matibabu hatua ambayo itawapa uhakika zaidi wa kuendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa kuwa mtaji wa masikini ni afya yake mwenyewe.




Kukubali kwa wanachama hao kujiunga na Bima ya Afya ni moja ya mafanikio makubwa ya WAMA ambayo lengo lake kubwa ni kuhakikisha inawaunganisha wajasiliamali hao na watoa huduma kama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

DIAMOND KUINOGESHA REDS MISS ARUSHA JUNE 23


Pichani wa kwaza kushoto ni mwalimu wa warembo wa jiji la Arusha, ambaye pia alishawahi kushikilia taji la Urembo Mbeya 2005 pamoja na kuwa mrembo wa nyanda za kuu kusini Enjo Justace katika kati ni mkurugenzi wa mwandago Investiment ambao ndio waandaaji wa shindano hili anayejulikana kama Faustini Mwandago na kulia ni meneja masoko wa hoteli ya Arusha Traveling ambapo ndipo warembo wameweka kambi hapo 

Picha warembo wanaoshindania urembo wa Arusha wakiwa katika pozi.

Picha ikionyesha warembo hao wakiwa wanafanya mazoezi ya kusoma (picha na libeneke la kaskazini)
Na Woinde Shizza,Arusha
Wakati wanyange wa kinyanganyiro cha Reds miss Arusha wakiingia kambini Jana msanii wa muziki wa kizazi kipya(bongo Flava)Naseeb Abdull alimaarufu Diamond anatarajiwa kupamba shindano hilo linalotarajiwa kufanyika June 23 jijini hapa.
 
Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa shidano hilo ambaye pia ni mkurugenzi wa mwandago investment ltd Faustoin Mwandago alisema kuwa shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mount meru hotel na litakuwa ni onyesho la kukata na shoka.

Alisema kuwa jumla ya warembo 20 kutoka vitongoji vinne vya mkoa wa Arusha wameingiaa kambini kujiwinda na shindano hilo ambapo alisema warembo hao ni washindi wa vitongoji vya Miss Arusha city centre,Njiro ,Sakina pamoja na monduli.

Aidha alibainisha kawa ampaka sasa warembo wote wameingia kambini na wameshaanza mazoezi mbalimbali na anaimani kwa mwaka huu mrembo wa Reds miss Tanzania atatoka mkoani hapa.
"kwakweli sio najisifu ila warembo wetu ni wazuri na naimani watashinda maana wanaelimu ya kutosha na maadalizi ni mazuri kingine kikubwa mwaka huu mashindano haya yatakuwa ya tofauti sana kwani tumejipanga vilivyo na atutaki kufanyakosa kwanini kila siku taji liende Dar na Mwanza safari hii nitahakikisha linakuja mkoa wa Arusha" alisema Mwandago.

Aidha alitaja baadhi ya vikundi ambayo vitatoa burudani kuwa ni pamoja na msanii mkubwa Diamond ambaye ndie amebeba tamasha katika burudani atayesindikizwa na kikundi cha ngoma na kucheza cha Boda 2boda cha mkoani hapa, msichana Sister P wa mkoa wa Arusha ambaye ni mwimbaji wa miondoko ya Reggae kutoka jijini hapa.

Aliwataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Tbl kupitia kinywaji chake cha Reds,Tdl kupitia kinywaji chake cha dodoma win,Tanzanite one,mogaben priter,libeneke la kaskazini blog,Arusha traveling logde ambo ndio wametoa kambi ya warembo. ''kwa upande wa viingilio kutokana na hadhi ya onyesho hili ambalo litakuwa la kihistoria kwani kwanza kabisa linafanyika katika hotel ya nyota tano na msanii anavuma ndo anakuja kwa mara ya kwanza kwaiyo kiingilio kitakuwa VIP 50000 huku kawaida shilingi 30000 ila napenda kuwapa ofa wanafunzi ambao watakuwa wamjikusanya kama kikundi na kutoa taarifa vyuoni kwao kutakuwa na punguzo cha zaidi tuwasiliane mapema ili wajue" alibainisha Mwandago

Kwa upande wake mwalimu wa warembo hao Enjo Justice ambaye alishawahi kuwa mnyange wa mkoa wa mbeya mwaka 2005 pamoja na mrembo wa nyanda za juu kusini alisema kuwa mashindano hayo yanamanufaa kwakuwa sanaa ya urembo inatanuka siku hadi siku na wengi wanaangalia mfano kutoka kwao lakini inaitajika nidhamu kujitambua wewe ninani na unawakalisha kanda gani na hivyo ndivyo moja ya vigezo vya kujua mrembo anavyotakiwa kuwa.

Alisemakuwa pia mlengo ya mashindano haya na kuwafundisha warembo hawa ni pamoja na kutambua wao ni warembo na wanatakiwa kujitambua na kuwaelimisha jinsi ya kuipeperusha bendera hii ya urembo itambulike sehemu mbalimbali.

MRUSI WA MATUMLA AKACHA BAADA YA KUONA REKODI YA MATUMLA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mrusi wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake ni kali. Wawili hao walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la “The Rumble on the Mountain” na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz ambaye atakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi tarehe 24 Juni mwaka huu.

Deidre Lorenz anajulikana sana kwa sinema nyingi mojawapo zikiwa The Santorini Blue, Perfect Strangers, The Big Fight na nyingine nyingi. Hata hivyo Deidre Lorenz ataingia mjini Moshi akitokea nyumbani kwake New York , Marekani terehe 21 Juni tayari kikimbia mbio hizo za Mt. Kilimanjaro Marathon.

Bondia huyo wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana kama “Siberian Tiger” aliingia mitini kiaina baada ya kupelekewa tiketi za ndege ya shirika la Kirusi la Aeroflot yeye na kocha wake. Hii ni mara ya kwanza kwa mpambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondia mmojawapo kuingia mitini kwa woga.

Bondia Rashid Matumla anayejulikana kama Snake Boy ana rekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.

Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki na Kati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani (WBU). Akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasa ndiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa hali ya juu.

Hata hivyo Rashid Matumla amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusi huyo!

Imetolewa na:

Onesmo A.M.Ngowi
President IBF/USBA for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)

Director, BRAND-Africa
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education & Resources Network (iEARN) to Tanzania

MCHEZASINEMA MAARUFU TOKA MAREKANI KUKIMBIA MBIO ZA MT. KILI MARATHON

Deidre Lorenz
Mcheza sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz atakimbia mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 24 Juni mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi.

Mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.

Ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight, na nyingine nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika jiji la New York City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.

Eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards. Mcheza sinema huyu ataambatana na Wamarekani wengine kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka jana.

Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.

Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta 42. Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote wanaweza kukimbia.

Imetolewa na;
Grace Soka
Afisa Uhusiano wa Mt. Kilimanjaro Marathon

MWANZA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

Maandamano ya watoto kuelekea uwanja wa michezo wa Nyamagana yaliyofanyika asubuhi hii jijini Mwanza.

Historia
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa tarehe 16, Juni ya kila mwaka. Siku hii inaadhimishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mnamo mwaka 1976.
Lengo la Maadhimisho
Siku hii huadhimishwa kwa lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto nchini Afrika ya Kusini wakati wakidai haki zao za msingi, pia kuwakumbusha wazazi/walezi na jamii kwa ujumla juu ya haki na wajibu wa jamii katika kuwalea watoto. Aidha, hutoa nafasi ya kuwakumbusha watoto haki na wajibu wao kama watoto katika Taifa
Maandamano yakikatiza barabara ya Kenyata kuelekea uwanja wa michezo Nyamagana jijini Mwanza.

 Kusanyiko la watoto ambao ni wanafunzi ndani ya uwanja wa Nyamagana.

 Diwani ambaye pia ni makamu meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Mh. Chinchibela akimzawadia kiongozi wa uimbaji wa kikundi cha watoto toka shule ya watoto wenye mtindio wa ubongo.

 Banda la maonyesho kiwanjani hapo.

 Maskauti watoto waliojitokeza kusanyikoni.

 Meza za mbele kusanyikoni.

 Banda la maonyesho na picha za viongozi wa Baraza la Watoto.

 Engo ya maonyesho hayo na kazi za mikono ya watoto.

 Tafadhali kama unajali soma ujumbe huu.

Watoto waliojipanga vizuri kusanyikoni katika siku ya mtoto wa Afrika mkoani Mwanza.

Friday, June 15, 2012

DIWANI MATATA ATOA MSAADA KWA JAMII YAKE


Diwani wa kata ya Kitangili wilaya ya Ilemela jijini Mwanza leo ametoa msaada kwa jamii inayoishi kwenye mazingira magumu na wale wenye ulemavu na wasio jiweza.

Diwani Henry Matata wa Chadema amesema kuwa ameamua kutoa  msaada wa Nguo, Vyombo vya chakula, Mchele, Unga, Maharagwe, Viatu kutokana na ukali wa maisha unaowakabili baadhi ya wananchi wenye uwezo mdogo. 

Bw.Matata amesema kuwa katika kata 9 za wilaya ya Ilemela, Kata ya kitangili ndiyo yenye watu wengi wasiojiweza na waishio kwenye mazingira magumu yakiwemo makundi kama walemavu, wajane na waathirika waishio na virusi vya ukimwi.


Diwani akiendelea na zoezi la ugawaji.

Akinamama wakiwa kwenye mstari kupata msaada.

Moja ya masanduku ya nguo.

Nafaka kwaajili ya msaada.

Pamoja na kata ya Kitangiri kukabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za uhaba wa maji safi na salama, barabara nzuri kwa mitaa yake, madawati kwa shule zake, vyumba vya darasa kwa shule za msingi na umeme diwani huyo amesema kuwa bado ataendelea kuzitafutia ufumbuzi kwa kuhakikisha  zinatatuliwa kwa kipindi cha uongozi wake.

Wazee wakihusika na nafasi yao kupokea msaada huo.

Kusanyiko katika tukio hilo la ugawaji misaada katani humo.

AIRTEL RISING STARS YAZIDI KUSHINE

Mchezaji namba 7 wa timu ya Mbeya Stanley Kadumu akipokea zawadi ya mpira kutoka kwa msimamizi wa michezo ya Airtel Rising Stars kutoka DRFA Daudi Kanuti mara baada ya kufunga mabao 3 katika mechi ya nusu fainali thidi ya timu ya Ilala

Timu ya wasichana wa Mbeya wakifurahia ushindi katika mechi za nusu fainali za Airtel Rising Star zilizofanyika leo ambapo mbeya imeifunga Ilala kwa penati mabao 3-2 

Timu ya wavulana mbeya ikishangia ushindi baada ya kuifunga ilala mabao 5-2 katika mchezo wa nusu fainali ya michuano yaAirtel Rising Stars
Wachezaji wa timu ya mbeya wa michuano ya Airtel Rising Stars wakifurahia ushindi walioupata leo baada ya kuifunga timu ya Ilala

NUSU FAINALI YA MICHUANO YA AIRTEL RISING STAR KUFANYIKA LEO

 Picture 1353Mchezaji Goodluck Mabiriki wa Ilala (kulia) akigombea mpira na mshambuliaji wa timu ya ya Lindi Khalfan Malibiche wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam. (matokeo nitakutumia kwa sms baadaye)

 MchezaRashid Said wa Lindi (kulia) akigombea mpira na mshambuliaji wa timu ya Ilala Innocent Kapuya wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam. (matokeo nitakutumia kwa sms baadaye)

Mchezaji namba 7 wa timu ya Ilala wasichana Madeline Sliverster akikabithiwa mpira na Msimamizi wa michezo DFRA ya Airtel Rising star bw Daudi Kanuti mara baada ya kufunga mabao 3 katika mechi thidi ya Lindi ambapo Ilala ilipata ushindi wa mabao 3-0

 Kikosi cha timu ya wasichana Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza michuano ya Airtel Rising Stars ambapo katika mechi hiyo Mbeya iliifunga timu ya wasicha Arusha 3-2 katika mechi iliyofanyika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam

Kikosi cha Timu ya wasichan Arusha wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza michuano ya Airtel Rising Stars iliyofanyika katika viwanja vya karume jijini Dar es Salam

Nusu Fainali ya michuano ya Airtel Rising Star inafanyika Leo
TIMU za soka za mkoa wa Mbeya za wanaume na wanawake zimejihakikishia kucheza nusu fainali ya michuano ya kukuza vipaji wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza leo kwenye uwanja wa Karume, Jijini, Dar es salaam.

Timu hizo zimefuzu kucheza nusu fainali hiyo baada ya kumaliza katika makundi yao zikiwa zinaongoza. Kwa wanawake, Mbeya ilizishinda Arusha kwa bao 3-2 katika mechi ya ufunguzi kabla ya kuichakaza tena Mbeya kwa mabao 4-0, wakati kwa wanaume wao walianza kwa kuishinda Arusha kwa bao 2-1 na kasha kuichapa Kinondoni kwa mabao 1-1.

Timu nyingine ya mkoa wa Arusha nayo imefanikiwa kupitisha timu zake zote za wanaume na wanawake baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi A nyuma ya Mbeya.

Mbali na timu hizo, zingine zilizofuzu kwa upande wa wanaume ni Temeke ilioonyesha kuwa tishio katika michuano hiyo kwa kufunga idadi kubwa ya mabao. Ilianza kwa kuisambaratisha Lindi kwa magoli 12-2 kabla ya kuichakaza tena Ilala kwa mabao 3-0. Wakati wanaume wamefuzu, timu yao ya wanawake inasubiri matokeo kati ya Ilala na Lindi zilizotarajiwa kucheza jana.

Hata hivyo, kwa upande wa wanaume timu ya mwisho itakayoungana na timu hizo inategemea matokeo ya mechi za mwisho za makundi zilizotarajiwa kuchezwa baadaye jana, sambamba na kwa upnade wa wanawake.

Katika mechi zilizochezwa juzi asubuhi timu ya wanawake ya Temeke iliichapa Ilala kwa magoli 2-0. Maholi ya wafungaji yalipatikana katika dakika ya 12 kupitia kwa Madeline Sylvester kunako dakika ya 12 na la pili likiwekwa kimiani na Zuhura Selemani katika dakika ya 44.

Kwa upande wa wanaumke, Temeke iliendeleza mwendo wake wa kugawa dozi baada ya kuibugiza Ilala kwa magoli 3-0. Goli la kwanza la washindi lilifungwa na Khalid Mwenda katika dakika ya 28, la pili liliwekwa kimiani na Paulo Balama katika dakika ya 43 na la mwisho lilpatikana kunako dakika ya 87 kupitia kwa mshambuliaji wake hatari, Bakari Ally.

Katika mechi nyingine iliyochezwa jioni, timu ya Wanawake ya Arusha iliifunga Kinondoni kwa bao 2-0, Kupitia kwa Anitha Antony katika dakika za 2 na 35. Mechi ya mwisho ilikutanisha Kinondoni na Arusha ambapo zioliztoka sare ya bao 2-2. Wafungaji wa Arusha ni Nazir Abdul katika dakika za 22 na 82, wakati yale ya Kinondoni yaliwekwa kimiani na Omar Ramadhani na Jarufu Lutonga katika dakika ya 55.

Thursday, June 14, 2012

HATIMAYE BAJETI 2012-2013 YAWASILISHWA BUNGENI



 Waziri wa fedha na uchumi Dk William Mgimwa leo amewasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ambayo nin sh Trilioni 15 tofauti na ile ya mwaka unaomalizika ya Sh Trilioni 13.5

Bajeti hiyo ina vipaumbele 7 ambavyo ni Miundombinu, kilimo, viwanda, rasilimali watu, huduma za jamii, utalii, pamoja na biashara ya ndani na nje na huduma za fedha.


Moja kati ya mapendekezo ya udiferenti yasema kuwa :- Ukitaka kuweka jina kwenye gari badala ya Plate number itakugharimu shilingi milioni 5 nayo itadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Bajeti imelenga kuviwezesha viwanda vya ndani kuhimili soko la ushindani kwa bidhaa zake dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.


Bajeti imetoa pendekezo la kulinda kazi za wasanii kwa kusajili kazi hizo ili kuwaingizia faida ya kipato kitakacho wawezesha kunufaika na kazi zao.

Hayo ndiyo ya udiferenti lakini pia ukweli ni kuwa inaonekana kama bajeti haina vitu vipya sanaaa, na imekaa kimjini mjini (isiyona manufaa kwa walio vijijini ) na baadhi ya vipengele vyake ni kama kuna marudio ya vile ambavyo vimewahi semwa huko nyuma kama ya kutuchapa bakora kwenye vinywaji na vileo .

Gharama za simu juu
Katika bajeti hiyo, Waziri Dk Mgimwa alisema muda wa maongezi (airtime) kwenye simu za mkononi umeongezeka kutoka asilimia 10 hadi 12. Alisema lengo la hatua hiyo ni kuoanisha ushuru wa bidhaa unaotozwa na huduma hiyo katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), kwa kipindi hiki ambacho nchi zipo katika Soko la Pamoja. Alisema hatua hizo za ongezeko la ushuru wa bidhaa kwa pamoja, zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh144,054.9 milioni.

Misamaha ya kodi ya magari

Waziri huyo alipendekeza kufanyika marekebisho kwenye sheria husika za kodi ya matangazo ya Serikali yanayotoa msamaha wa kodi kwenye magari kwa walengwa mbalimbali ili kuweka ukomo wa umri wa miaka minane kwa magari hayo badala ya miaka 10.

Alisema magari yenye umri wa zaidi ya miaka minane yatatozwa ushuru wa bidhaa wa asilimia 20. Lengo la hatua hiyo ni kupunguza wimbi la uingizaji magari chakavu na kulinda mazingira. Alitangaza pia marekebisho katika ushuru wa forodha, ikiwemo kufuta msamaha wa ushuru wa forodha katika vitu mbalimbali vikiwemo magari yenye ujazo wa CC 3000 huku pia ushuru wa forodha ukifutwa katika bidhaa nyingine nyingi muhimu.

Alisema katika kuhamasisha na kuchochea ukuaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki, vifaa vinavyotumika katika ufugaji na kurina asali vimepewa msamaha wa ushuru wa forodha vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi na wafugaji wa nyuki.

Msamaha wa ushuru wa forodha kwenye migahawa ya majeshi ya ulinzi utaendelea kutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja. Alisema kumefanyika marekebisho katika Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya mwaka 2004 ili kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwa wazalishaji wa vyakula vinavyotengenezwa mahsusi kwa lishe ya watoto wenye utapiamlo na watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

Katika Bajeti hiyo, pia wametoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi zinazotumika katika kutengeneza vifaa vya kufanyia uchunguzi wa magonjwa (medical diognastic kits) kwa kuwa vifaa hivyo hutozwa asilimia sifuri vinapoagizwa kutoka nje ya nchi.

Utatolewa msamaha kwenye mitambo (machinery) na vipuri vyake vinavyotumika kwenye uchimbaji wa madini lakini hautahusisha vipuri vya magari vitakavyoagizwa na makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini.

Katika bajeti hiyo, pia umetolewa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyuma vinavyowekwa kwenye kingo za barabara na lengo lake ni kutoa unafuu katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Alisema ushuru wa forodha umepunguzwa kwa ving’amuzi kutoka asilimia 25 hadi asilimia sifuri ili kuwezesha mabadiliko katika teknolojia ya analogia na kwenda katika teknologia ya digitali.

Ushuru wa ngano umeondolewa kuwa asilimia 0 badala ya asilimia 35 Serikali pia imesamehe VAT katika mashine za kutolea stakabadhi (electronic fiscal devices), ili kupunguza bei yake na kuwezesha wafanyabiashara wengi kuwa nazo, kuhamasisha matumizi yake na hivyo, kuongeza mapato ya Serikali.

Katika eneo hilo, Serikali imeondoa VAT kwa vifaa mbalimbali vya kuhifadhia, kusafirisha na kusambaza gesi asilia ili kuongeza matumizi ya nishati hiyo katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kwenye magari, majumbani na viwandani.

Kodi kwa wafanyabiashara
Wafanyabiashara ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 hawatalipa kodi kuanzia Julai Mosi, mwaka huu. Dk Mgimwa alisema mpango huo umefanywa kulinda mapato ya Serikali. Kabla ya msamaha huo, wafanyabiashara hao ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 walikuwa wanalipa Sh35,000. Marekebisho mengine ya kodi ya mapato ni kuwa wenye mapato kati ya Sh3 milioni –Sh7.5 milioni watalipa Sh100,000 badala ya Sh95,000.

Malengo ya Bajeti
Waziri Mgimwa alisema Bajeti hiyo imejielekeza katika Kukuza Pato la Taifa kwa asilimia 6.8 mwaka 2012 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.4 mwaka 2011. Malengo mengine ni kuimarisha miundombinu ya uchumi, ikijumuisha umeme, barabara, reli na bandari, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongezeka kwa mapato ya ndani yatakayofikia uwiano na Pato la Taifa wa asilimia 18 kwa mwaka 2012/13 kulinganisha na mwelekeo wa asilimia 16.9 mwaka 2011/12.

Dk Mgimwa alitaja malengo mengine kuwa ni pamoja na kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei ili urudi kwenye viwango vya tarakimu moja na kuwa na kiwango tengemavu cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha.

Malengo mengine ni kukuza mikopo kwa sekta binafsi kwa kiwango cha asilimia 20 ya Pato la Taifa ifikapo mwishoni mwa Juni 2013, sambamba na jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei, kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo na wa kati, kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta za huduma za jamii, kuimarisha utawala bora na uwajibikaji na kujenga uwezo wa nchi kukabiliana na misukosuko ya kiuchumi na kifedha pamoja na kushiriki kwa ufanisi katika ushirikiano kikanda na kimataifa.

Matumizi ya Maendeleo
Kuhusu matumizi ya maendeleo, Waziri Mgimwa alisema itazingatia vipaumbele vya miundombinu ya umeme - mkazo ukiwa upatikanaji wake kwa kuongeza uzalishaji, usafirishaji na usambazaji na jumla Sh498.9 bilioni zimetengwa.

Serikali pia itatekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa mkopo kutoka Benki ya Exim ya China wenye thamani ya Dola za Marekani 1.2 milioni utakaosimamiwa na TPDC. Kuhusu usafirishaji na uchukuzi, alisema mkazo katika sekta hiyo utakuwa ni kuimarisha reli ya kati ikijumuisha ukarabati wa injini na mabehewa ya treni.

“Kwa upande wa barabara, miradi inayopewa kipaumbele ni pamoja na barabara zenye kufungua fursa za kiuchumi. Katika usafiri wa anga na majini, miradi itakayotekelezwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege na uendelezaji wa gati ya Ziwa Tanganyika. Jumla ya Sh 1,382.9 bilioni zimetengwa katika eneo hili,” alisema.

Kuhusu maji safi na salama, alisema lengo ni - kuongeza upatikanaji wake mijini na vijijini na kwamba kiasi cha Sh568.8 bilioni kimetengwa. Kwa upande wa kilimo, uvuvi na ufugaji alisema katika sekta hizo, Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi itawekeza katika kilimo cha mpunga na miwa katika mabonde makuu ya Wami, Ruvu, Kilombero na Malagarasi pamoja na kuongeza tija na thamani, kubadilisha mfumo wa kilimo na kukuza kilimo cha misitu.

Kuhusu kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na kuhakikisha uhakika wa chakula, Serikali itaimarisha utekelezaji wa dhana ya Kilimo Kwanza kwa kuhakikisha nguzo zake zote zinaendelea kuzingatiwa.

Alisema mikoa inatakiwa kuendelea kutenga ardhi na vijiji kutakiwa kupima na kurasimisha ardhi kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na wa nje na kwamba kiasi cha Sh192.2 bilioni kimetengwa katika eneo hilo.

Ikizungumzia maendeleo ya viwanda, alisema Serikali inakusudia kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini; viwanda vinavyoongeza thamani ya madini; viwanda vikubwa vya saruji na viwanda vya eletroniki na Tehama pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji mijini na vijijini na kukuza ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.