ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 21, 2012

KOZI YA MCHEZO WA NGUMI NI ZAMU YA MAKOCHA KUTUPIANA MASUMBWI

Kocha wa Tmu ya JKT, Saidi Omari 'Gogo Poa' (kushoto) wakioneshana ufundi wa kutupa makonde na Kocha wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' wakati wa mazoezi ya vitendo yanayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani leo kwenye kozi ya kimataifa ya mchezo wa ngumi.

Kocha mchezo wa ngumi wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' (kushoto) akitupiana makonde na kocha wa Mkoa wa Pwani, Gaudence Uyaga wakati wa mazoezi kwa vitendo kwa makocha hawo ambao wapo katika kozi ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi Duniani.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)


KOZI YA YA KIMATAIFA YA KUFUNDISHA MCHEZO WA NGUMI

Kozi ya Makocha wa Ngumi inayoendelea Kibaha, Pwani katika shule ya Filbart Bayi, inaendelea vema chini ya mkufunzi aliyeletwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Josef Diouf kutoka Senegal.

Ikiwa imefika siku ya sita makocha wanaohudhuria mafunzo hayo ya siku kumi, wamelizika na kiwango cha mkufunzi huyo kwa kusema kuwa mbinu za kiufundi na ujanja wa ufundishaji wa mchezo wa ngumi anazo wafundisha ni za kisasa na kwamba kwa sasa wameelewa msingi wa ufundishaji,hasa kwa kumwanzisha, kumwendeleza mchezaji hadi kufikia kuwa mchezaji wa kimataifa toufauti na awali ambapo walikuwa wanafundisha kwa mazoea bila kuwa na mbinu za kuwafanya wachezaji ili kuleta upinzani hasa katika mashindano ya kimataifa.

Lakini pia wamejifunza namna ya kuandaa ratiba za ufundishaji za siku kwa siku, wiki, mwezi na ratiba ya mashindano yanayowakabili

Kwa kujigamba Makocha kutoka mikoani wamesema ujuzi wao wataanza kuonyesha katika mashindano ya Taifa yatakayofanyika katikati ya mwezi wa February ya kuwa kutakuwa na ushindani mkali sana hasa kwa kuzingatia mikoa mingi makocha wake wamepata mafunzo hayo,na sasa timu za vyombo vya ulinzi na usalama na zile za Dar es salaam ziwe tayari kupata upinzani wa hali ya juu kwa kuwa sasa hata vilabu vya kutoka mikoani pia zina mbinu na ujanja wa ufundishaji kulingana na mabadiliko ya mchezo wa Ngumi Duniani.

Kozi hiyo inatazamiwa kumalizika tarehe 24/01/2012 na walimu watakaokuwa wamefaulu watatunukiwa vyeti vya kimataifa vya daraja la kwanza(level 1) na kuingizwa katika Database za Chama cha Ngumi cha Dunia AIBA na kwamba watakuwana haki ya kufundisha mchezo wa Ngumi popote Duniani

Wakati huo BFT kwa masikitiko makubwa inasikitika kupatwa na msiba wa bondia wa timu ya Taifa Godfrey Mbunda aliyefariki kwa kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki maeneo ya mbezi. Hakika hili ni pigo kubwa katika medani ya mchezo wa ngumi kwa kuwa bado mchango wake ulikuwa unahitajika kwa suala la maendeleo ya mchezo wa ngumi Tanzania

Makore Mashaga
KATIBU MKUU

Friday, January 20, 2012

BIBI MALAIKA ASHEREKEA KUFIKISHA MIAKA 75

Keki ya kumpongeza bibi Malaika kufikisha miaka 75.

Dada Cosmaya (wa pili kulia mwenye nguo nyeupe) akiwa na wifi yake Mama wa mitindo Asia Khamsin pamoja na marafiki zao wengine waliohudhurua katika maadhimisho ya miaka 75 kuzaliwa kwa mama yake mzazi Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Bibi Malaika (katikati) ambaye amefikisha miaka 75 akiwa na mwanae mama Khatibu pamoja na mke wa mwanae Mama wa mitindo Asia Khamsin.

Bibi Malaika akisalimia na Captain Mwaiki katika sherehe ya kumpongeza Bibi Malaika kufikisha miaka 75.

Bibi Malaika akisalimia na Balozi mstaafu wa Ufaransa Mhando katika sherehe ya kumpongeza Bibi Malaika kufikisha miaka 75..

Bibi Malaika akimlisha keki mwanae Cosmaya.


...Utamu wa keki mpaka kaamua kufumba macho...

Bibi Malaika akimlisha keki mme wake mkubwa yani mume wa mjukuu wake wake wa kwanza Meline.

Chearsssss

Wageni waliohudhuria katika sherehe ya kuadhimisha miaka miaka 75 ya kuzaliwa Bibi Gonsaga Mwingira Shawa a.k.a Bibi Malaika iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Nawashukuruni sana kwa ushirikiano wenu, Mungu awabariki mabloger wote.
Cathbert Angelo Kajuna,

VITUKO VYA SLAA KWENYE MAZISHI YA MTEMA;

VITUKO VYA SLAA KWENYE MAZISHI YA MTEMA...”Mchumba” wake AMZUIA ASISALIMIANE NA JK, KISA? ITALETA MANENO…!
Mazishi ya Mbunge wa Chadema, Mheshimiwa Regia Mtema yamethibitisha kuwa vituko na vioja vya Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa Wilbroad Slaa na “mchumba wake,” Josephine Mushumbusi havijaisha hata kama sasa wanaishi pamoja.

Kwa namna ambayo sasa imethibisha nani hasa mwenye madaraka, mamlaka na kauli ndani ya nyumba yao, Josephine Mushumbusi amemzuia “mchumba/mume” kwenda kumpa mkono Kiongozi wa nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Mara baada ya Rais Kikwete kuingia katika makaburi ya familia ya Mtema mjini Ifakara kiasi cha saa tisa unusu mchana, Mheshimiwa Slaa ambaye alikuwa amekaa peke yake na Josephine pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema, alionyesha ishara ya kwenda kumsalimia Mheshimiwa Rais Kikwete ambaye alikuwa jukwaa kuu. Lakini Josephine Mushumbusi alimzuia mchumba wake asiende kumsalimia Rais Kikwete akimwambia, “usiende…italeta maneno ya bure.” Kwa namna inayothibitisha nani bosi ndani ya nyumba, Mheshimiwa Slaa alijikunja na kusalimu amri akisema, “haya bwana”.

Kila dalili za tukio hilo zimethibisha kuwa ubabe na ushujaa ambao Mheshimiwa Slaa huonyesha hadharani kwa kutukana, kukejeli na kuwashambulia wenzake katika siasa akiwamo Rais Kikwete ni nguvu za soda tu zisizotamba mbele ya Josephine ambaye alionyesha udhitibi na umwamba wake hadharani leo.

Lakini tukio la leo pia limethibitisha kwa mara nyingine kiwango cha kinyogo ambacho familia ya Slaa na mchumba wake wanayo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete tokea Rais alipowabwaga na kumsambaratisha kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, 2010.

Tokea wakati huo, Mheshimiwa Slaa hajapata kumsema vizuri Rais Kikwete, hajapata hata kumtambua hadharani pamoja na kujua kuwa alishindwa kihalali, hajapata kumsalimia wala kumpa Kiongozi huyo wa nchi mkono hadharani hata fursa inapojitokeza kama leo.
Kwa ufupi, tukio la leo na mengine mengi yalimtangulia limethibitisha kuwa Mheshimiwa Slaa ni kiongozi mwenye kinyongo na asiyekuwa na heshima kabisa.

Kama ambavyo wamepata kusema wengine hana sifa za kuwa na kiongozi mkuu wa nchi yetu hii inayoongozwa kwa misingi ya maelewano na siyo kwa misingi ya chuki ambazo anazionyesha Mheshimiwa Slaa. Kwa hili Dr. Slaa Kachemsha, kadhihirisha wazi kuwa hana siyo tu ukomavu wa uongozi bali pia ukomavu wa kisiasa. Sasa naelewa pia kwa nini Slaa upadre ulimshinda.

Ni jambo la ajabu kuwa mfiwa kama alivyokuwa Slaa leo kwa sababu yeye amempoteza Mbunge anakataa vipi kwenda kumsalimia mwombolezaji ambaye amekwenda kumpa pole na kumjulia hali. Huu ni ubinadamu na uungwana kweli?

Mzee Slaa anashindwa na wadogo zake kama vile Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambao walipeana mikono na kukaa pamoja na Mheshimiwa Rais, kubadilishana mawazo na kuomboleza kwa pamoja.

Imetumwa na
Mtanzania mkweli
Naomba kuwasilisha.



RIHANNA NA VIBIKINI DAMU DAMU...!

Silver swimsuit

Monokini iliyobuniwa na mbunifu toka Australia Lisa Maree.

One of the teeny tiniest of her bikinis, Rihanna still looked amazing in a geometric print bikini while in Hawaii in 2010.

Bikini si ufukweni tu bali hata katika stage.

Rihanna wore a sexy, curve-accentuating monokini toka kwa mbunifu maarufu wa mavazi ya kuogelea Johnny Vincent.

Cute and casual

Thursday, January 19, 2012

JK KATIKA MSIBA WA MAREHEMU JEREMIAH SUMARY JIJINI DAR ES SALAAM LEO!

Jakaya Kikwete Akimpa pole mjane wa Marehemu Jeremia Sumary, Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha wa wa zamani aliyefariki leo asubuhi jijini Dar es salaam. Hapa ni nyumbani kwa marehemu, Mbezi Beach, Dar es salaam jioni hii.

Rais Jakaya Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo.

Jakaya Kikwete akiongea na ndugu wa marehemu pamoja na Spika Anne Makinda na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa ambaye ni mzazi wa binti aliyeolewa na mtoto wa marehemu Sumary.

Rais Jakaya Kikwete akitoa pole kwa wafiwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, Mama Miriam Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

AJIRA MPYA ZA WALIMU ZATANGAZWA MAJINA YATOLEWA

Kwanza Tunapenda wasalimu wakubwa wetu Shikamoo na vijana wenzetu Mambo vipi.. Tunatambua kuwa Wanavyuo wenzetu walimu walikuwa hawana kazi kwa muda mrefu Jambo ambalo liliwafanya wengi kuwa na wasi wasi na mwajiri wao. Tunapenda kuwapa tarifa kupitia mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo (www.tzwanavyuo.blogspot.com) kuwa, Walimu wahitimu wote Jana usiku majira ya sa saba Nafasi hizo zilitangazwa Rasmi, Pia sisi Tunapenda kuwasilisha majina ya wanafunzi ambao wamechaguliwa Tunaomba mchukue Muda wenu kutazama kwa umakini majina yenu yote yapo hapa. Hongereni sana.


Kutazama Majina ya walimu walio pata Ajira Bofya hapa http://www.tzwanavyuo.blogspot.com/

Imeandaliwa na,
Matukio na Wanavyuo Crew
www.tzwanavyuo.blogspot.com
twanavyuo@live.com

Wednesday, January 18, 2012

KULENI KUKU, MAYAI, MBOGA, SAMAKI ....

Msimu wa wakusoma mambo ya clubin kushoto

Kuku

Samaki fresh aina ya sato na sangara na wachuuzi wake kwenye soko la jioni Market street Mwanza.

Dagaa wa ziwa victoria

Mbogamboga na mizizi

Matunda

SHULE ZOTE MWANZA HILI LINAWAHUSU

kARIBu sAAANaaaa!!!!

ONYESHO MAALUM KUMUENZI MSANII ALIYEUAWA MWANZA KUFANYWA NA WASANII WA MWANZA JUMAPILI HII NDANI YA STONE CLUB

Kwanza kabisa naomba radhi wadau wote wa Blogu hii kwani nilishindwa kufikisha taarifa hizi mapema mtandaoni kutokana na kupigwa butwaa kwa msiba uliotokea, kwangu ilikuwa ngumu kuamini kuwa mdogo wetu katutoka... ingawa nilikuwa napata muda wakutundika taarifa nyingine mtandaoni lakini kwa hili moyo ulikuwa mzito.. mzito nikihisi ni kama mchezo wa kuigiza hivi... Kumbe kweli Mo-Chella hatunaye na leo imenibidi kuandika...Marehemu Mo-Chella katika safari yake ya mwisho.
KWA UFUPI.
Mwana bongo fleva wa hip hop toka Rock City Frank Buchella aka Mo-Chella alifariki dunia tarehe 12/jan/2012 kwa kuchomwa kisu cha chemba ya moyo katika eneo la mitaa ya Nera na jamaa mmoja dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Christopher au Alliance Tota au Baba Keja. Ili kuingiza matirio wakati alipokuwa akijisomea kwa mitihani aliamua kwenda kuamua ugomvi wa jamaa huyo aliyekuwa akizozana na mwanamke mmoja na ndipo mauti yalipo mkuta

Mo-Chella ambaye pia aliyekuwa mwanafunzi wa CBE Mwanza amezaliwa tarehe 10/march/1989 na kuzikwa tarehe 14/jan/2012, mazishi yake yalishuhudiwa na watu wengi akiwemo Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Queen Mlozi, Mbunge wa Ukerewe Salvatory Luyaga Machemli (CHADEMA), wasanii wenzake toka familia ya muziki wa bongo fleva Mwanza inayojulikana kwa jina la Mwanza Kwanza na wadau mbalimbali.


D-Malik(L) akiwa na marehemu Mo-Chella(R)
ONYESHO MAALUM LA KUMUENZI KUFANYIKA JUMAPILI HII
Kutokana na msiba huu wasanii wote wa Mwanza kutoka katika familia ya Mwanza Kwanza chini ya mwenyekiti wao Philbert Kabago watafanya Tamasha la kumuenzi marehemu Mo-Chella, litakalofanyika Jumapili 22/jan/2012 ndani ya ukumbi wa Stone Club kuanzia saa nane mchana hadi saa mbili usiku, kiingilio shilingi 2000/=

Mapato yote yatakayopatikana yatapelekwa kwa mama wa marehemu ikiwa ni kama njia ya kumfariji na kutambua mchango wake katika sanaa.

Alipokuwa akihojiwa studio za Passion Fm
Mo-Chella ambaye alikuwa akitegemewa kurithi mikoba ya wakali kadhaa wanaosikika na kutamba wakiwakilisha Rock City tayari alikwisha fanya ngoma zake kadhaa katika studio mbalimbali ikiwemo A2P, Mo-Records na Young Don Production atatakumbukwa kwa kuyatendea vyema majukwaa mbalimbali ya ushindani jijini, Mwanza show yake ya mwisho alipiga tarehe 31/dec/2011 usiku wa kuukaribisha mwaka mpya 2012 ndani ya Stone Club ambapo alipanda jukwaa moja na Suma Lee mara baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki wa 91.0 Passion Fm wiki moja kabla ya show hiyo.

UZOEFU NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAZEE KARAGWE NA MULEBA

MASHIRIKA yanayoshughulika na wazee wilayani KARAGWE (SAWAKA) NA KWA WAZEE MULEBA Yamefanya semina ya siku moja na waandishi habari mkoani Kagera kuona jinsi ya kushirikiana kufichua matatizo na kupata jinsi ya kukabiliana nayo kupitia vyombo vya Habari mkoani humo.

Akifungua semina hiyo Meneja wa mradi wa saidia wazee Karagwe Bwana Livingsote Bartholomeo Byekwaso, amesema lengo kuu ni kusaidia kufichua matatizo ya wazee pamoja na kutia chachu kwa serikali kutekeleza ahadi zake kwa wazee hao.

Naye Bi TEREZA EDWARD MINJA Mwenyekiti wa Tanzania Social Protection Netwaork akitoa tamko la wazee, katika semina hiyo amesema bado wazee wanalaumu serikali kutoweka sera ya wazee kisheria jambo linalosababisha matamko ya serikali kwa wazee hao kutotekelezwa kama matibabu bure na pensheni.

Mzee maarufu mkoani kagera na Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya kahawa Tanzania PIUS NGEZE amesisitiza kuwa serikali ijitahidi kuwajali wazee kwani wanapofika umri wa uzeeni afya zao zinakuwa na matatizo hivyo wasionekane bora wakiwa vijana uzeeni wakatengwa.

Wanahabari....

Hawa ni waandishi Habari mambo kwa upande wao wamesisitiza ushirikiano wa mashirika ya saidia wazee Karagwe na Muleba kutoa ushirikiano na wanapokuta tatatizo sehemu wawe tayari kuwajulisha waandishi ili wayatangaze lakini kubwa zaidi washirikiane kuwezeshana kufika maeneo korofi.
PICHA na Nicolaus Ngaiza
Radio Kasibante.

KOZI YA KIMATAIFA YA UKOCHA WA NGUMI INAENDELEA KIVITENDO MKOA KIBAHA MKOA WA PWANI

Take one....!!!

Action....!!!
Baadhi ya Makochai wa Mchezo wa Ngumi nchini wakifanya mazoezi kwa vitendo wakati wa kozi ya kimataifa ya mchezo huo kwa makocha inayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Tuesday, January 17, 2012

MAANDALIZI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MHE. REGIA E MTEMA (MB), TAREHE 17 JAN VIWANJA VYA KARIMJEE NA MAZISHI IFAKARA, KILOMBERO

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiongoza kikao cha kamati ya Uongozi kujadili ratiba ya maandalizi ya mazishi ya Mhe. Regia Mtema katika ofisi za Bunge jana. walioko kulia ni Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb), Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William Lukuvi.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichokaa jana chini ya uenyekiti wa Mhe. Spika kujadili ratiba ya maandalizi ya mazishi ya Mhe. Regia Mtema katika ofisi za Bunge. Kulia ni Mhe. Zaituni Buyogela (Mb) na Mhe. Maua Daftrari. mwenye suti kushoto ni Mhe. William Lukuvi. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: MAANDALIZI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MHE. REGIA ESTELATUS MTEMA, (MB), TAREHE 17 JANUARI, 2012 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE NA MAZISHI IFAKARA, KILOMBERO, MOROGORO – TAREHE 18 JANUARI, 2012
UTANGULIZI
Marehemu Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema alifariki kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu, mkoani Pwani mnamo majira ya saa 5.30 asubuhi tarehe 14 Januari, 2012. Ofisi ya Bunge baada ya kuthibitisha kifo hicho kupitia Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani na baada ya Kuwasiliana na familia, mara moja ilituma Maafisa Waandamizi kwenda katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani kuuchukua Mwili wa marehemu na kuuleta Muhimbili kuhifadhiwa ikiwa ni pamoja na kufanya maandalizi ya mazishi. Baada ya maandalizi hayo na kwa ushirikiano na familia na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni yafuatayo yamekubaliwa kufanyika:-

MWILI KUAGWA NA FAMILIA TAREHE 16 JANUARI, 2012 KATIKA KANISA KATOLIKI SEGEREA
Familia imeandaa Misa ya Marehemu katika Kanisa Katoliki Segerea siku ya Jumatatu tarehe 16 Januari, 2012 kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 11 jioni. Mwili wa Marehemu utaondoka Hospitali ya Muhimbili saa 7 mchana na baadae kurejeshwa tena kwa hifadhi baada ya Misa.

MWILI KUAGWA RASMI KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE TAREHE 17 JANUARI, 2012
Ofisi ya Bunge imeandaa utaratibu kwa viongozi wa kitaifa, Waheshimiwa Wabunge, Wananchi kuuaga rasmi Mwili wa Marehemu katika viwanja vya Karimjee siku ya Jumanne tarehe 17 Januari, 2012. Shughuli hiyo inatarajiwa kuanza saa 3.00 asubuhi na kuhitimishwa saa 5.30 asubuhi (Ratiba imeambatanishwa kama kiambatisho A). Kama ratiba inavyoonesha, Mwili wa Marehemu utaondoka katika viwanja vya Karimjee saa 5.30 asubuhi mara tu baada ya kuaga katika viwanja vya Karimjee kuelekea Ifakara, Kilombero mkoani Morogoro kwa mazishi.

RATIBA YA MAZISHI YATAKAYOFANYIKA IFAKARA
Ratiba ya tarehe 18 Januari, 2012 ambayo ndio siku ya Mazishi nyumbani kwa Marehemu Ifakara, Kilombero Mkoani Morogoro imepangwa kwa kuzingatia mila na desturi za familia. Ratiba hiyo ni kama ilivyo katika kiambatisho B. Kwa ratiba hiyo, shughuli zimepangwa kuanza saa 5 kamili asubuhi na kukamilika saa 10.30 alasiri.

MAANDALIZI MENGINEYO
Mpaka hivi sasa familia imearifu kuwa Msiba huo umepokelewa kwa hisia kubwa katika eneo alilozaliwa Marehemu Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema na kwamba tujiandae kwa ushiriki kwa wakazi wa Kilombero takriban 1000. Aidha, Ofisi inaendelea na Maandalizi ikiwa imejiandaa kwa ushiriki wa viongozi wa kitaifa Mkoani Morogoro.

SHUGHULI ZA KAMATI ZA BUNGE SIKU YA JUMANNE TAREHE 17 JANUARI, 2012
Kutokana na uzito wa tukio hili, Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia Umma kuwa shughuli za Kamati za Bunge kwa jumanne tarehe 17 Janauari, 2012 ambazo zinafanyika katika Ofisi ya Bunge , Dar es Salaam, zitasitishwa hadi jumatano tarehe 18, Januari, 2012

Ofisi ya Bunge inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mhe. Regia Estelatus Mtema, (MB) mahali pema peponi. Amina.

Imetolewa na,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
DAR ES SALAAM
16 Januari, 2012

Monday, January 16, 2012

KITAANI KWETU MAJI SPESHO HAYANA LADHA.....!

Maji haya yanahifadhiwa kwenye chupa za makampuni tofauti tofauti (dasano, kilimanjari, uhae, akwa roku na etc), chupa zinazokusanywa mara baada ya kutumika kisha zinafungwa vizuri bila 'sildi' nakuwekwa kwenye friji..dakika kadhaa kitu briiidi kinaingia sokoni...
Wakati yale spesheli @ chupa ni shilingi 500/= bei kwa chupa moja kwa maji haya ni shilingi 100/= hadi 200/= tu...!

Wateja wakuu wa maji haya ya kunywa ni madreva wa daladala, makonda, mamantilie na wateja wao magengeni, wachuuzi wa samaki na mbogamboga sokoni, wadau minadani, baadhi ya madreva wa pikipiki, makuli aka wabeba mizigo masokoni, wanafunzi wa shule za msingi na kadhalika....

Utayarishaji wa maji haya: hayachemshwi bali huwekwa water guard kisha yakachujwa, ukiuliza kwanini hayachemshi wadau wanasema kuni mzigo mmoja ni shilingi 1,500 na hazitoshi kuchemsha maji hivyo hutumia njia rahisi isiyo na gharama kuyasafisha kwa water guard.

Ila sasa kuna wengine hata hiyo water guard hawaweki bali huyachuja na kuyauza juu kwa juu...

Katika pitapita yangu nakutana na mjasiliamali huyu, muuza maji ya kunywa wateja wake wanasema maji ya kuchemsha "oooh... hayana ladha..." wengine "oooh... nikinywa maji ya kuchemsha tumbo linauma" MWINGINE akanigusa nikamwelewa Yaani nitoe 500/= kununua maji wakati kipato changu chenyewe kwa siku 500/=?

Sunday, January 15, 2012

KAFULILA KANSA NDANI YA NCCR MAGEUZI ASEMA MBUNGE WA KASULU MJINI MH. MOSES MACHALI

KATIBU Mwenezi wa NCCR Mageuzi Taifa Mbunge wa Kasulu mjini mh. Moses Machali amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa mbunge aliyetimuliwa uanachama hivi karibuni David Kafulila ndani ya NCCR Mageuzi ni sawa na kuilea kansa .Machali.
Machali ameyasema hayo jana katika mkutano wa NCCR Mageuzi uliofanyika katika uwanja wa Sahara jijini Mwanza uliokuwa na lengo la kuimarisha chama hicho.

Katibu huyo mwenezi wa NCCR Mageuzi amemtaja David Kafulila kuwa ni 'mpuuzi na kigeugeu' kwani ndiye aliye mshauri Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia kufungua kesi dhidi ya Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee aliyemtolea maneno ya kashfa kipindi cha mchakato wa uchaguzi na ndiye aliye mshutumu Mbatia kwa kufungua kesi hiyo dhidi ya Halima Mdee.


Akithibitisha kuwa Mbatia hakuwa na nia mbaya kufungua kesi kama inavyotajwa na Kafulila, Machali alisema kuwa kabla ya kufungua kesi hiyo Mbatia alimwambia Mdee "ukiniomba radhi na kunisafisha kwenye vyombo vya habari sina tatizo na wewe, Halima Mdee akajibu kuwa ukienda mahakamani nitakwenda kukuvua nguo huko huko.

James Mbatia kwa ushauri wa Kafulila akafungua kesi mahakamani lakini mara baada ya kufungua kesi Kafulila ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshutumu Mbatia kufungua kesi dhidi ya mpinzani mwenzake na kumtaja kuwa ni kada wa Chama cha mapinduzi (CCM)"

Katibu huyo mwenezi alisema kuwa Kafulila alishamwambia nia yake ya kuukwaa uenyekiti wa NCCR Mageuzi na kwa kuwa alikuwa na ajenda hiyo alianza kumzushia mambo mbalimbali bwana James Mbatia, jambo la kwanza likiwa ni kumtaka mwenyekiti huyo kujiuzuru kwa kushindwa kukiendeleza chama hali inayokifanya kizidi kudidimia.


"Nikamwambia Bunge la 9 lililoishia mwaka 2010 NCCR ilikuwa haina hata mbunge mmoja bungeni leo tuna wabunge wanne chini ya uongozi wa Mbatia, nao wananchi wa Kigoma wamekuamini kwa kampeni na nguvu za huyo huyo Mbatia"
"NCCR ilikuwa na madiwani 19 nchi nzima leo tuna madiwani zaidi ya 40 je haya siyo maendeleo?" alisema Machali kisha akaongeza...
"Nikamwambia, NCCR ilikuwa ikipata ruzuku ya shilingi milioni 1.2 kwa mwezi lakini leo kutokana na idadi ya madiwani kuongezeka tunapata shilingi milioni 12 kwanini tusiige mfano wa wenzetu CHADEMA kwa sisi wabunge wanne tukafanya kazi ya kuaminika majimbo mbalimbali tukaongeza idadi ya majimbo wewe unaanzisha chokochoko zisizo na tija bali kukivuruga chama?"

"Akaniambia 'Ndugu yangu, kaka yangu machali shida yangu ni Uenyekiti' "
"Nikamwambia uenyekiti hautafutwi hivyo subiri 2013 tutakwenda kwenye uchaguzi wa chama wanachama wakikuamini watakupa nafasi"

"Akaniambia 'Achana na mimi' " na ndipo alipoanza kuwarubuni makamishina mbalimbali akiwaambia kuwa ANATAKA KUFANYA MAPINDUZI NDANI YA CHAMA....


Akizianika nyaraka za Kafulila kuomba msamaha vikaoni.
Mh. Machali aliongeza kuwa zaidi ya mara 20 katika kipindi cha mwaka mzima 2011 chama hicho kimekuwa kwenye vikao kikijadili masuala ya Kafulila na mbunge huyo amekwisha onywa na kukiri mwenyewe kuwa amekosa na hatorudia kukivuruga chama lakini kila kiakao kinachoitishwa kimekuwa kikimzungumzia yeye.. Nyaraka za Kafulila kumuomba msamaha mwenyekiti wake James Mbatia kwenye baadhi ya vikao.

Wananchi wakiperuzi baadhi ya nyaraka zilizoanikwa kwenye hadhara hiyo alizoandika Kafulila kuomba msamaa kupitia vikao mbalimbali vya NCCR Mageuzi.

Hii kali zaidi....!!!!!!!!!!
"Chama kimeshindwa kufanya mambo mengi ya maendeleo kwa wananchi wake kwa kupoteza muda kumjadili mtu mmoja, tumekaa chini na kupima uwepo wake chamani na manufaa iwapo tutamtupa nje ya chama hivyo sote kwa pamoja tukasema TUMECHOKA" alisema kwa msisitizo katibu mwenezi huyo wa NCCR Mageuzi Mh. Moses Machali.