ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 19, 2012

TOTO PARTY NDANI YA CINE CLUB DESEMBA 25 NA 26, 2012

Hii ni mara ya tatu kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na itafanyika Krismasi na Boxing Day ndani ya Cine Club.
Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka la ufukweni, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi.
Aidha watoto hao pia wataweza kufunga akaunti ya benki kwa watoto inayojulikana kama ‘Pambazuka’ kupitia benki ya Ecobank.
Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.