ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 29, 2012

PATO LA MKOA WA MWANZA LAKUWA KUTOKANA NA SHUGHULI ZA UZALISHAJI KUSHAMIRI.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akiwasilisha Muhutasari wa Taarifa ya Utekelezaji mbele ya waandishi wa habari shughuli iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya mkuu wa mkoa.

Pato la Mkoa wa Mwanza limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka kulingana na ongezeko la uzalishaji katika sekta mbalimbali.

Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo wakati akiwasilishwa muhutasari wa taarifa ya kuhusu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya disemba 2005 hadi mwezi juni 2012 mbele ya waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kulingana na Takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu, wastani wa pato la mwananchi kwa mwaka limepanda hadi kufikia 924,536 kutoka 421,379.

Kwa wastani wananchi wa Mkoa wa Mwanza, wamevuka kiwango cha umaskini uliokithiri kwa watu wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

 Pia mkoa wa Mwanza umetajwa kuwa mchangiaji mkubwa wa pato la Taifa ambapo kwa mwaka 2011 Mkoa ulichangia asilimia 9  ukiwa ni Mkoa wa pili ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es Salaam uliochangia asilimia 16.6.
UTEKELEZAJI
 Jumla ya mashamba darasa 2,115 yalianzishwa na kuendelezwa Mkoani Mwanza ili kuwafikishia wakulima vijijini maarifa yanayohusu kanuni za kilimo bora.  
Moja ya shamba darasa la Pamba lililoko kijiji cha Solwe, Wilaya ya Kwimba, hali hii imefikiwa mara baada ya wakulima wa eneo hili kupewa maarifa ya jinsi ya kubotesha uzalishaji.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akiwasilisha Muhutasari wa Taarifa ya Utekelezaji mbele ya waandishi wa habari shughuli iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya mkuu wa mkoa.

MAPINDUZI YA UVUVI: (Ibara ya 41)
           Maelekezo ya Ilani:
Kuweka ulinzi madhubuti dhidi ya wavuvi haramu ikiwa ni pamoja na kukamata vyombo vyao vya uvuvi na kuwatoza fidia kwa mujibu wa sheria.

Uzalishaji:
Jumla ya shilingi billioni 250.2 zimeingia katika uchumi wa wananchi wa Mwanza.
Shilingi bilioni 3.6 zimelipwa kama sehemu ya kodi kwa serikali.

Utekelezaji:
Doria shirikishi dhidi ya wavuvi haramu zilifanyika zikihusisha vikosi vya doria vya Wilaya/Mkoa, jamii ya wavuvi (BMUs) na Polisi.   Watuhumiwa waliokamatwa ni 1,178, Zana haramu zilizo kamatwa ni Makokoro 5,971, Nyavu za Makila 37,980, Nyavu za dagaa (vyandarua) 992, Timba 9,317, kamba za kuvutia Makokoro mita 469,541, Samaki wachanga waliokamatwa ni Sangara wachanga kilo 220,021, sato wachanga kilo 59,596.
Zana haramu zilizokamatwa ziliharibiwa, Samaki wachanga kugawiwa kwenye vituo vinavyolea watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, Taasisi za Serikali, kwa idhini ya Mahakama. Aidha, Watuhumiwa wote 1,178  walifikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Moja ya boti za kisasa kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu, Wilayani Sengerema.
Upatikanaji wa samaki unapungua siku hadi siku hii imetokana na sababu zifuatazo:-
(a)   Uvuvi wa kutumia zana haramu kama vile makokoro, timba, Katuli, na nyavu za macho madogo.
(b)   Kufanyika kwa uvuvi kwenye maeneo ya mazalia ya samaki.
(c)   Kuendelea kupungua kwa kina na maji ya ziwa  Victoria kunakosababisha kuathirika kwa mazalia na makulio ya samaki.

Sensa ya uvuvi iliyofanyika mwezi Agosti, 2010 ilionyesha kwamba matumizi ya zana haramu yamepungua kwa kiasi kikubwa, kwa mfano matumizi ya nyavu za makila (gill nets) zenye macho madogo madogo yalikuwa yamepungua kwa asilimia arobaini na tano (45%).
Mkoa unaendelea kutoa elimu juu ya uvuvi endelevu, hivyo jamii inaombwa kushirikiana na Serikali katika kutokomeza uvuvi haramu.

Maelekezo ya Ilani:
Kuimarisha miundombinu ya uvuvi kwa kujenga mialo, masoko ya kisasa, vituo vya kutotolea vifaranga vya samaki na maabara.

Utekelezaji:
Ukarabati wa mialo tisa umefanyika katika Mkoa kwa mchanganuo ufuatao, Magu 2, Jiji la Mwanza 3, Sengerema 3,  na Ukerewe 1. Na ujenzi wa mialo 2, vituo 2 vya kupokelea samaki, Majengo ya Ofisi 2, Mabanda 2 ya kupokelea samaki yenye meza, Toshari za chuma 2, umefanyika kwa wilaya za  Magu (Kigangama)  na Sengerema (Kahunda), 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.