ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 8, 2012

WATU MAARUFU KUPANDA JUKWAANI KATIKA ONYESHO LA KANGA LITAKALOFANYIKA 23 NOVEMBER HII.



Mama wa Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia Kampuni yake ya Fabak Fashions wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale litakalofanyika Novemba 23, 2012 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Onyesho hili kubwa ambalo limekuwa likifanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Marekani, litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka sehemu mbali mbali ambao nao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.

Watu Maarufu hapa nchini watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha Mavazi ya Khanga za Kale kutoka kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ambapo fedha itakayopatikana kutokana na onyesho hilo itapelekwa kwenye Kituo cha Kulea watu walioathirika na Madawa ya Kulevwa kilichopo Kikale Wilayani Rufiji, Mkoani Pwani kwa ajili ya kumalizia ujenzi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.